Wakenya Tupeni Uzoefu Wenu Kuhusu Passport

Jambo Moja ni muhimu kuzingatia, passport lazima ilindwe na kudhibitiwa Ili iweze kuheshimika duniani, tukifanya mchezo itatuwia vigumu Sana kitembea nchi za watu, itafika wakati huko nje ukijulikana tu wewe ni mtanzania, watu wanatukimbia
Tanzania inawafungia ndani watu wake mithili ya mbuzi wezi, lakini Kenya imewapa uhuru wa kwake kutoka kwa kuwa inawaamini watu wake. Kwa nini basi, pamoja na Tanzania kuwafungia ndani raia wake na Kenya kuwaruhusu wa kwake kutoka, passport ya Kenya inaizidi ya Tanzania?

Unafahamu Kenya inajulikana zaidi duniani kuzidi Tanzania?

Bora tu ukomunisti na ujamaa zilikufa. Ni laana. Ni masalia ya mitazamo yake ndiyo inayoitesa Tanzania.
 
Unasema Kenya imeathirika negatively kwa sababu ya raia wake wengi kwenda nje? Ni mtazamo wako lakini si sahihi. Ili kupata mzania sahihi, orodhesha hasara zote na faida zote, kama hutabaini kuwa faida ni nyingi kuzidi hasara.

Usipoona faida, basi uanze dozi ya kula biringanya, nanasi, ndizi mbivu na mbegu ya maboga kwa ajili ya kurejesha afya ya ubongo.
 
Mkuu, unaishangaza dunia kwa huo mtazamo. Ni North Korea pekee ndiyo inaweza ikakubaliana na mtazamo wako, kwa kuwa haipendi raia wake wajue jinsi Dunia inavyoenda. Kule watu "wanafugwa" na "kutumikishwa" kwa maslahi ya watawala.
Mkuu, wewe ndio unawashangaza watu, inaonekana hujatembea na Wala hujui jinsi nchi zonavyojiendesha duniani, hakuna nchi yoyote inayotoa "Government documents" kwa urahisi, Wacha passport, hata leseni ya udereva tu kuipata ni ngumu Sana.

Hebu nenda Ulaya ukaombe leseni ya udereva uone hilo sakata lake. Kwahiyo mkuu, hizi serikali zote zinazodhibiti passpot zao unadhani ni wajinga au hawajui kitu, ila ninyi watu wachache ndio wenye akili?.

Mkuu, tatizo hujazunguka Dunia, na Wala hujui "International diplomacy" inavyofanya kazi. Passport ni document yenye kubeba utu wa Taifa nje ya nchi, mtu yeyote aliyebeba passport ya nchi lazima apewe heshima inayoendana na nchi yake huko ktk nchi anakokwenda, ni wajibu wa balozi zetu huko nje kuhakikisha mtu yeyote mwenye passport ya Tanzania anatetewa na kulindwa haki zake, huwezi kuwapa watu wa hovyo hovyo passport.

Mkuu, Kama nilivyokijibu hapo juu, huu uamuzi wa kuidhibiti passport umepitishwa na kukubalika hapa nchini na kupitishwa na vyombo vyote vyenye majukumu ya kusimamia Sheria za nchi na haki za binadamu. Sasa Kama wewe unadhani una akili nyingi kuwazidi hao wote waliopitisha na kusimamia jambo hili, basi Tanzania sio nchi sahihi kwako. Ila unayo haki ya kutoa mawazo yako, na serikali inayo haki ya kufanya vile inavyodhani ni sahihi.
 
Mkuu, inaelekea hata Kenya bado hujafika. Hakuko hivyo kama unavyofikiri. Ina wasomi wa kutosha na ziada, ndiyo maana Serikali yake inafanya jitihada kuwatafutia raia wake kazi katika mataifa mengine.
Mkuu, kwa akili ya kawaida tu jiulize, Kweli Kenya inaweza kuwa na wasomi wengi kuzidi Japan na Ujerumani?. Eti Kenya inawatafutia kazi wasomi wake kwenda kufanya kazi Ujerumani, hicho ni kituko Cha mwaka.

Nchi kuwa na wasomi wengi lazima ionekane kwa vitendo, hivi ni jambo gani linakuonyesha kwamba Kenya Kuna wasomi wengi?. Uchumi inazidi kuporomoka, umasikini unaongezeka, ukabila inazidi kukomaa, viwanda vinafungwa, uzalishaji wa bidhaa viwanda I unapungua, kilimo kinakufa kwa kukosekana mifumo ya umwagiliaji, magonjwa ya kuambukiza Kama kipindupindu ndio nyumbani kwake, hao wasomi Kenya wanafanya nini zaidi ya kutoroka nchi Ili kutuma remittances?
 
Kenya imekuwa ranked poorly kwa sababu inapakana na Somalia,
Somalia kila siku ni vita na mashambulizi ya al shabaab
Kwanini Ethiopia au Djibout hazina hilo tatizo la usalama na zimepakana na Somalia?
 
Mkuu, ni mtu mjinga pekee atakayewekeza pesa nyingi katika elimu nchini kwake, Kisha akasherehekea Wasomi wake kwenda kufanya kazi nchi zingine.
Passport siyo kwa ajili ya anayetaka kwenda kufanya kazi nje tu, mwingine anaweza akahitaji kwa ajili ya kwenda kutembea.

Mkuu, inaonekana hujawahi kuvuka mpaka wa Tz kwenda nchi nyingine.

Au ulitumia kikaratasi chenye muhuri wa Mwenyekiti wa Kitongoji chako?
 
Serikali haisomeshi, bali inatoa mikopo tena kwa baadhi tu.

Kuna wengine, wengi tu, walisoma kwa kujilipia au kulipiwa na wazazi au walezi wao.
Ukisoma kwa mkopo wa serikali ndio kusomeshwa na serikali, hivi serikali ikiacha kutoa mikopo Kuna mtu ataweza kwenda kupata mikopo Bank na kujisomesha?. Kwa hapa Tanzania 98% husomeshwa na serikali kwa kupitia mikopo.
 
Nitajie hizo Serikali, ukiacha Tanzania, zinazodhibiti utoaji wa passport kwa raia wake kama unavyosema, kama hutaona kuwa hakutakuwepo hata na Serikali Moja ya watu wanaojitambua yenye ukiritimba wa hovyo kama huo.
 
Mkuu, Cape Town nimefika, nilikaa Century City kwa miezi mitatu. Century City ndio kuna Canal Walk Grand Mall.

Hamna mtu ameshawahi idhalilisha nchi ya ya Tanzania 🇹🇿 pale.

Nchi zote duniani kuna mazuzumagic, Marekani kuna ombaomba,UK 🇬🇧 pia. Nimekaa The Hague miaka miwili, ombaomba walikuwepo.

Watanzania watoke nje ya nchi wakatafute riziki CCM acheni utaahira wenu. Jifunzeni kutoka Kenya 🇰🇪
 
Marekani kuna Wajapani wengi wanaofanya kazi huko, unataka kutudanganya kuwa Japan ina wasomi wengi kuizidi Marekani?
 
Serikali ni jukumu lake kuwapa elimu watu wake, elimu ni haki ya raia. Hivi kwanini mnahusisha Sana elimu na ajira?, kwani wakulima, wavuvi, wafanyabiashara na wafugaji hawapaswi kupata elimu?.

Lengo la serikali ni kwaelimisha raia wake wote Ili wafanye kazi zao kwa tija na ufanisi, 70% ya watanzania wanajihusisha na kilimo. Achaneni na mawazo ya kitumwa kwamba Kila aliyesoma lazima apate kazi ya kuajiriwa.
 
Unazungumzia wasomi majobless? Yaani mtu amalize chuo leo, halafu amsubiri mwekezaji miaka minne bila ajira..!!!
YOU NEED TO CHANGE YOUR THINKING KWENYE JAMBO HILI..!!
Wewe ambaye Hadi Leo unayehusisha elimu na kazi ya kuajiriwa ndiye unapaswa kubadili mawazo yako, unasikia huo mpango wa BBT unaosimamiwa na Hussein Bashe?
 
Ingelikuwa ni mamlaka yangu, ningeagiza, hata kama hupendi, ushikilie nafasi ya UKAMISHNA UHAMIAJI, hata kama ni kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.

Naamini, ndani ya miezi mitatu kungeweza kupatikana ahueni kubwa sana.
 
Kumbe unafahamu hilo. Inawezekana na wewe uko kwenye system. Kama kuna mahali mmekwama, mseme msaidiwe. Kuna Watanzania wengi wenye mawazo mbadala na wako tayari kuyatoa bure, bila kudai malipo yo yote.
Soma umalize hiyo paragraph, nimekutega na wewe unaingia kwenye mtego wangu. Nimekuambia Kuna watu wengi wenye akili na wameamua hivyo, kwahiyo haupo peke yako, usidhani kwamba wewe ndiye mwenye akili.

Ukidhani wewe pekee ndiye mwenye kujua kuwazidi watu wengine, basi hilo ni tatizo la akili, lazima ujitathimini upya.
 
Ukisoma kwa mkopo wa serikali ndio kusomeshwa na serikali, hivi serikali ikiacha kutoa mikopo Kuna mtu ataweza kwenda kupata mikopo Bank na kujisomesha?. Kwa hapa Tanzania 98% husomeshwa na serikali kwa kupitia mikopo.
Serikali inatoa wapi hela kama siyo kwa wananchi wake? Serikali kuwadumia raia wake si fadhila, ni wajibu. Pesa iliyopo Serikalini ni ya wananchi.
 
Kenya imekuwa ranked poorly kwa sababu inapakana na Somalia,
Somalia kila siku ni vita na mashambulizi ya al shabaab
Sahihi na hata Nigeria ni kwa sababu ya boko haramu

Lakini passport kuwa ranked poorly sio kuwa raia wote nchi hiyo hawaruhusiwi kuingia bali ubalozi unatakiwa kuwa careful kwenye kutoa viza hasa kwanwatu kutoka eneo lenye utata kwenye husika

Mfano wasomali wengi sana Kenya ambao ni wakenya kwa kuzaliwa na raia wa Kenya wakienda kuomba Viza ubalozi mfano wa Marekani ngoma nzito

Lakini wakenya wengine hawawi strict kivile

Nigeria pia iko hivyo mtu.kama.anatokea majimbo ya kaskazini kwenye harakati kubwa za boko haramu viza yake kupata screening.yake sio ya kitoto

Lakini kwenye kutoa passport wanigeria hutoa bila longolongo na urasimu sababu wanajua kumpa passport raia sio kuwa atasafiri.bado kuna kikwazo cha kupata.Viza huko.aendako anachotakiwa kupambana nacho.Huko.wanamwachia mwenyewe.ahangaike nako ila passport wameshampa.Mengine ya kwake

Swala la kusema ohh mtu aweza enda nje akafanya uhalifu .Ni mawazo mgando.Akifanya uhalifu nchi za watu polisi wapo mahakama zipo atakiona cha mtema.kuni huko huko alikoebda kufanya uhalifu

Kwani sisi wageni wa nchi zingine wakifanya uhalufu hapa si huwa tunawakamata na kuwaburuza mahakamani mahakama.zetu na kuwafunga nk.

Nchi za wenzetu watoa passport bila vikwazo wanaamini dola za nchi zingine kuwa nao wana vyombo vya dola na mahakama.na jela pia.Sisi ni kama hatuamini nchi nyingine kuwa sisi ndio.tuchuje yupi aende nchi zao na yupi asiende!!! Tunajipa shida bure
kujiongezea majukumu yasiyo.ya lazima.Mpe raia wako passport waache wenyewe kwenye balozi anakoenda kuomba biza ndio wachuje nani aingie nchi yao na nani hawamtaki

Tanzania kuchujana kunaanzia kwenye kupeana passport sio sahih kuuliza kuwa eleza unaenda kufanya nini nchi unakoenda? Hayo maswali mwache akaulizwe ubalozini au mipakani na nchi husika anayoenda.Wewe toa passport mengine mwachie
 
Unafahamu kuwa Tanzania kuna maelfu ya watu ambao tokea wahitimu Vyuo zaidi ya miaka kumi iliyopita, hawajapata ajira mpaka sasa?

Unafurahia unapowaona wakitembea na bashasha za khaki huku viatu vimeisha soli kwa kusaka ajira?
Mkuu, huko nje hawaendi hao watu waliokosa ajira hapa Tanzania, kawaida huko nje huchukua "top cream" ya wasomi huku Africa, wanatuachia vilaza ndio tuwaajiri hapa nchini.

Kama wewe ulipita chuo kikuu, nitajie wangapi kati yenu waliopata ajira nje ya nchi, na kati Yao wangapi walifauli kiwango Cha chini?.

Kibaya zaidi, wengi wanaokwenda huko nje ni madaktari na Engineers waliokua wameajiriwa serikalini na ni madaktari bingwa, sio "fresh from school".
 
Mambo muhimu kwa binadamu ni
1)Usalama
2)Chakula
3)Maji safi na salama
4)Makazi
5)Afya
6)Haki na utu wa binadamu.

Katika vigezo vyote hivyo, Tanzania Iko mbele Sana ya Kenya. Ni mtu mjinga peke yake atakayedhani kwamba Kenya inaizidi Tanzania kwa kutumia kigezo kimoja pekee Cha GDP.
 
Mimi nimeweka sababu zonazoonyesha athari mbaya ya Kenya kutokana na kuruhusu raia wake kwenda nje ya nchi kwa wingi, Sasa wewe onyesha faida ambazo Kenya inazipata Ili tulinganishe.
 
Uongo

Tuekeze kwa nini basi Kenya inayoachia.wananchi we wengi kwenda nje na kutoa passport kirahisi kuwa eanakosea tueleze kwani pesa ya Kenya ona nguvu kuliko pesa ya Tanzania? Na kwani uchumi wa Kenya uko juu kuliko wa Tanzania tunaofungia wananchi na kuwabania passport ili tubaki na hao wenye akili nyingi?

Kwa maelezo yako ingekuwa hivyo badi uchumi wa Tanzania ungekuwa juu kuliko.wa Kenya na pesa yetu Ingekuwa na nguvu kuliko ya Kenya

Miaka 60 tunabania passport mbona hatupiti Kenya kiuchumi na nguvu ya pesa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…