TANZIA Wakili Alute Lissu Mughwai (kaka wa Tundu Lissu) afariki Dunia

TANZIA Wakili Alute Lissu Mughwai (kaka wa Tundu Lissu) afariki Dunia

Wakili Allute Lissu Mughwai ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amefariki usiku wa kuamkia Leo Novemba 1, 2026.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Dada yake aitwaye Rose Masesa pindi alipozungumza na Jambo TV.

Jambo TV ilipotaka kufahamu chanzo cha kifo chake Rose ametueleza kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza lolote huku akitueleza kuwa msiba upo jijini Arusha.

"Ni taarifa za kweli msiba upo Arusha na mimi naelekea huko" alisema Rose kwa ufupi.


===
Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, Brenda Rupia amethibitisha kutokea kwa msiba huu, amesema "Ni taarifa ya kweli, msiba umetokea na sasa viongozi wetu wanaelekea gerezani kuonana na Mwenyekiti baada ya hapo tutatoa taarifa rasmi na kamili"
Sa100 amepeleka uchungu na vilio kwenye familia nyingi sana za watu...
 
Pole sana kwa familia ya Lissu, ndugu zake huyu mzee...

Siku nilipomtazama na kumsikiliza mzee Allute kwenye yale mahojiano na yule muandishi kama chotara wa Kiarabu, kuna kitu kiliniambia moyoni kwamba huyu mzee hana siku nyingi (pengine ni kutokana na uzoefu wa kesi mbili tatu za kukaa na watu wanaokaribia mauti).

Hata hivyo nilipuuzia fikra hizo kwa nguvu zote, na kama hiyo video ingelikuwa ipo hapa labda ningeliandika ila kwa kuwa nilitazama youtube basi nikajiambia huku YT anonymity sio kama JF, hivyo tufanye haya ni mawazo tu...

Sasa muda huu naingia JF, nakutana na hizi habari za mauti yake dah!

Anyway, wanasema "Kifo kinajua mahali unaishi"
 
Wakili Allute Lissu Mughwai ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amefariki usiku wa kuamkia Leo Novemba 1, 2026.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Dada yake aitwaye Rose Masesa pindi alipozungumza na Jambo TV.

Jambo TV ilipotaka kufahamu chanzo cha kifo chake Rose ametueleza kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza lolote huku akitueleza kuwa msiba upo jijini Arusha.

"Ni taarifa za kweli msiba upo Arusha na mimi naelekea huko" alisema Rose kwa ufupi.


===
Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, Brenda Rupia amethibitisha kutokea kwa msiba huu, amesema "Ni taarifa ya kweli, msiba umetokea na sasa viongozi wetu wanaelekea gerezani kuonana na Mwenyekiti baada ya hapo tutatoa taarifa rasmi na kamili"
Inauma..pole lisu
 
Tundu anapitia kipindi Kigumu mno.
1. Kumpoteza kaka yake yeye akiwa Gerezani.
2. Kushushiwa Mvua ya Risasi.
3. Kupewa Kesi za Kijinga na Uongo.
4. Hali ya kisiasa nchini.
5. Kuwa mbali na Familia
6.
Wasaliti ndani ya Chama chake.

Kifo hakina mwenyewe mkiona wengine wanakufa
Msifanye dhihaka na kifo.

Kifo hakina kutafuta wale wewe ndio chaguo lako wafe
Kinaenda kwa yoyote kinachukua mnabaki kushangaaa
Nayeye pia kaenda ✍️
 
Back
Top Bottom