John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Mgogoro wa kuwani eneo uliopo kati ya Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabishara maarufu Ghalib Said Muhamed (GSM) unaendelea na hadi sasa kila upande unavuta upande wake ukiamini wenyewe ndiyo una umiliki halali wa eneo hilo.
Tayari GSM kupitia Mwanasheria, Alex Mgongolwa ameshajitokeza hadharani kuweka wazi kuwa GSM ndiye mmiliki halali wa eneo hilo licha ya kuwa hakuna sehemu waliyotaja jina la Makonda, wakati ambapo RC huyo wa zamani amesikika kupitia ‘clip’, mitandao ya kijamii na kunukuliwa na gazeti akimshutumu mfanyabiashara huyo.
Wakili Bashir Yakub anafafanua baadhi ya mambo kisheria kuhusu mgogoro huo baada ya kuulizwa kuhusu ufafanuzi wa kisheria:
Kisheria kosa hadi mgogoro umeanza limeanzia wapi?
“Ukinunua ardhi (nyumba, kiwanja, shamba) hakikisha unafanya transfer (kuhamisha umiliki kutoka aliyekuuzia kwenda jina lako mnunuzi) mara moja kadiri uwezavyo.
“Wengi mkinunua kwa sababu hakuna anayekulazimisha kufanya transfer kwa haraka basi mkishakabidhiwa hati na mikataba ya mauziano mnakaa nazo hata miaka 2 au 3 mkisema nikipata hela ndio nitafanya transfer. Usifanye hivyo.
“Mjue kuwa kama hujafanya transfer uwezekano wa aliyekuuzia kukuzunguka na kukuchezea ni mkubwa sana.”
Unahisi Makonda aliuziwa lakini hakufanya transfer ya documents zake?
“Siwezi kusema aliuziwa au la lakini kwa mujibu wa maelezo yao inaonekana kama kulikuwa na makubaliano au mauziano baina ya pande mbili, hiyo ni kwa tathimini ya mkataba niliouona.
“Unakuta inaweza kutokea mazingira kama hayo, mfano mmoja ni kuwa, aliyekuuzia anaweza kutoa taarifa ya kupotelewa na hati na hivyo kupatiwa taarifa ya kupotea (lost report).
“Kisha, akafanya tangazo gazeti la kawaida na lile la Serikali (GOVERNMENT GAZETTE@GN).
“Kisha, akafanya maombi ya kupatiwa hati mpya kupitia Form No. 3 Chini ya Kifungu cha 38 cha Sheria ya Usajili wa Ardhi, Sura ya 334. Kisha, atapatiwa hati nyingine mpya.
“Kwa hiyo kutakuwa na hati mbili katika ardhi moja, ile aliyokupa we mnunuzi na hii mpya ya kwake, huu tayari ni mgogoro mkubwa kwako mnunuzi usiye na hatia (Bonafede purchaser).
“Akishakuwa na hati hayo mengine anaweza kuyakataa kirahisi, na pengine watu wa namna hii hata zile saini anazokuwa amekuwekea kwenye nyaraka nyingine zinakuwa siyo zake.
“Lakini mbaya zaidi ni kuwa, usipofanya transfer na wakati umeshanunua, shughuli zote zinazohusu ardhi hiyo, mfano kulipia kodi za ardhi, vibali vya ujenzi, tathmini, tozo na kila kitu kinaendelea kusoma jina la aliyekuuzia na kinafanyika kwa jina la aliyekuuzia.
“Maana yake ni kwamba, ushahidi wote wa risiti na nyaraka nyinginezo unaendelea kumtambua aliyekuuzia kuwa mmiliki halali ambapo anaweza kutumia ushahidi huo dhidi yako, ndiyo inawezekana imekuwa hivyo kwa Makonda na GSM kwa mujibu wa mazingira yanavyoonekana.
“Ataonesha risiti zinamsoma yeye na atasema nilikuwa nilipia, atachukua hata kibali cha ujenzi bila we kujua na atakionesha kinamsoma yeye nk, nk.
“Ninachotaka kuwashauri mkafanye transfer haraka mnaponunua. Najua mnaogopa gharama hasa Capital Gain ambayo ni 10%, lakini hii mbona inazungumzika na huwa inapungua.
Umesema mkataba umeuona, umeuona wapi na ni halali mkataba kuonyeshwa hadharani?
“Mkataba wa mauziano baina ya pande mbili kati ya mtu na mtu huwa ni siri lakini mimi nimeona mtandaoni hivyo kuna mmoja kati yao au wote waliamua kuvujisha.
“Pia, mkataba huo unaweza kupatikana masjala, yeyote anaweza kwenda kuomba kuuona kwa faida yake au jamii hasa kama suala lenyewe limekuwa na mgogoro kama hivyo.
Mkataba uliouona hakukuwa na mashahidi?
“Mkinunua hakikisha mikataba yenu inashuhudiwa na mawakili. Nimeona ule wa Makonda na Gharib ulishuhudiwa na Wakili aitwaye Ibrahim Shineni. Huyu kwa sasa ni nguzo muhim mno, yaani mno katika huu mgogoro.
“Katika mkataba niliouona kuna jina la Wakili Ibrahim Shineni. Kunapokuwa na mchakato wa kusaini mkataba kama huo huwa kunatakiwa kuwa na mashahidi wa pande mbili, lakini mkataba niliouona unaonyesha shahidi wa kisheria alikuwa mmoja tu ambaye ni huyo Ibrahim.
“Huyo ndiye mtu muhimu zaidi kwa pande zote, Wakili kwa cheo chake ni afisa wa viapo (Commissioner for Oaths), ni Mthibitishaji wa Umma (Notary Public) na pia ni Afisa wa Mahakama.
“Akiwa kwenye mkataba wako wa manunuzi ya ardhi ni mtu muhimu mno na shahidi wako muhimu anayeaminiwa sana na Mahakama.
Wakili huyo umuhimu wake ni upi katika sakata hili?
“Umuhimu wa huyu Wakili ni mkubwa sana, huyu ndiye ambaye anaweza kutoa majibu kwa mahakama kama kweli mkataba huo ulikuwepo na Makonda aliuziwa.
"Kama Wakili huyo akiamua kusimama upande wa GSM inamaanisha itakuwa ngumu zaidi kwa Makonda kushinda na kama akisimama upande wa Makonda inaweza kuwa ni faida kubwa kwa Makonda kama kesi itafika Mahakamani.
Vipi kuhusu mjengo ulipo katika kiwanja?
“Kiukweli kuna vitu ambavyo naona vinachanganya, kwa kuwa mwanasheria wa GSM alizungumzia kuhusu eneo katika maelezo yake, lakini katika ile clip inayosambaa Makonda anasikika akisema kuwa hata lile jengo ni la kwake.
“Hivyo, inachanganya kidogo je, wanagombea eneo pekee au wanagombea pamoja na jengo lililopo, na je, kama mgogoro wao ni wa kiwanja kwa nini Makonda katika ile clip anazungumzia kuhusu jengo lililopo pale!
Atakayeshinda kama hausiki na jengo lililopo, kisheria ipoje?
“Sheria inasema kuwa ikitokea mtu kashinda katika kesi ya ardhi chochote ambacho kitakuwepo katika eneo husika ni mali yake, anaweza kuamua kuvunja au kuendeleza.”
Pia soma >>>

- Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma
- Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake
- Makonda: Baadhi ya Askari Polisi jijini Dar wanawalinda wafanyabiashara matapeli wanaodhulumu mali za watu
- Makonda: Ghalib usinilazimishe kusema uozo wako, achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua