Wakili Dickson Matata: Hukumu inaweza kuwa batili, mahakama haikumsaidia mshitakiwa kuwaleta mashahidi wake.

Shahidi ambaye hata hamjuani? Unamwitaje kwenye kesi yako eti rafiki yangu mtu kakukataa big time kuwa siyo rafiki yake kifupi Jahazi limezama.
Sio Suala la kufahamiana ni Suala la una taarifa Gani muhimu ya kuweza kuamua kesi.
 
Bado tunaendelea kudanganywa asa wale wasiojua sheria vizuri.Kuongea nadharia bila kuweka ata kifungu cha sheria ni upepo tu,, Matata akasome CPA 145 na 150(O3)
Kingai hakufika mahakamani
 
Mnajitahidi nyie. Ila mnamwangamiza mwenzenu. Mana hamtaki kuamini naye ni binadamu na aweza kukosea.
Hivi mahakama ikitoa summons kwa shahidi na shahidi akagoma kuja kutoa ushahidi utamlaumu vipi mtuhumiwa? Punguzeni upofu wa uchama muangalie mambo kwa uhalisia.
 
Yaani huyo kubwa la majinga na majinga menzake yasipoelewa huu mchango wako, basi hayo hata yapelekwe motoni hayawezi tena kuhisi chochote.

Kongole kwa ufafanuzi ambao hata mjukuu wangu wa grade 6 anauelewa vyema sana.
 
Lissu ndiye alipeleka samansi!!??
 
Ni wapi Lissu alisema Kingai ni rafiki yake.?
Watu wengi hapa hawaelewi shahidi kisheria ina maana gani na aina tofauti za mashahidi.

Wanarukia mada tu kwa uelewa wao finyu wa sheria na mantiki.

Halafu Watanzania wengi wana tatizo la kujifanya wajuzi wa kila kitu.

Yani mtu hata hajui shahidi kisheria maana yake ni nini, halafu anataka kuikosoa strategy ya Tundu Lissu mwanasheria wa siku nyingi, aliyekuwa rais wa TLS, mwenyekiti wa chama cha upinzani.
 
Hivi mahakama ikitoa summons kwa shahidi na shahidi akagoma kuja kutoa ushahidi utamlaumu vipi mtuhumiwa? Punguzeni upofu wa uchama muangalie mambo kwa uhalisia.
Shahidi amekuja na Lissu mwenyewe kakiri. Au Lissu kaidanganya Mahakama?
 
Wewe umeitwa na mahakama ila siku ya kesi hutokezei unaishia nje. Huo ni mtego kwa mahakama iliyomuita. Sema tu mahakama zetu ni za kijinga
Lissu keshawatetea mashahidi na ameridhia maelezo yao.
Wa kumlaumu hapo ni Mwenyekiti wenu aliyekubali.
 

Naam, na kupitia hivyo Lissu aliligundua hili tangu siku ya kwanza akawasuprise waliotunga kesi hii kwa kuamua kujitetea mwenyewe.

Lissu anatumia muda wake kusoma akiwa gerezani nadhani wengine hawalijui hilo nakumbuka hata mwanafalsafa alisema gerezani ni sehemu ambayo huzaliwa fikra mpya nyingi , hili wengi hawalielewi .

Lissu anapata muda mwingi kupitia vitu vingi wao pasipo kujua wanamunderrate wakifikiri anahitaji internet pekee.

Lissu hadi sasa amenyimwa kuonana na ndugu na mawakili wake mara nyingi tu ila bado kesi inawaelemea hao jamhuri hadi leo wanarukaruka tu na kushindwa kuthibitisha wanachokiita uhaini.
 
Kuna milayman mingine ina akili mbovu sana, nani kwakwambia shahidi lazima awe rafiki yako na lazima aje kukutetea? Shahidi hapaswi kukutetea anapaswa kueleza ukweli na uhalisia kwa facts ambazo ni relevant na admissible ili ziweze kuiongoza mahakama kubaini ukweli na hatimaye kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria.

Lissu kuwataja DCI, IGP na CDF hakuwa amekosea, sababu kuna mambo Lissu alitaka waje wahojiwe waelezee ambayo ni relevant kwenye kesi yake, unapozungumzia uhaini ni suala la usalama ambapo vyombo vya serikali kama majeshi vinahusika.

Mahakama ilipima na kuona ushahidi wa wakuu hao ni comptent witness ndomana ikatoa summons, hivyo hata huo wito hukutolewa na Lissu bali ni mahakama ndiyo iliyowaita kwa wito wa Lissu, hivyo mashahidi walipaswa kureport kwa aliyewaita (mahakama) chini ya kiapo na kuexpress dhamiri yao ya kutokutoa ushahidi ambapo pia ni kosa.

Lissu kufunga ushahidi haimaanishi kuwa DCI na wenzake wapo sahihi, bali mahakama ndio mmiliki wa wito huo ndio inapaswa kujiongoza na kufanya maamuzi. Kwani mtuhumiwa akifunga ushahidi sio ticket ya DCI na wenzake kupona kuwajibika, na tutashangaa sana huku ya kesi hii ikadeclare lissu kuwa na hatia ilihali fairness ya haki ya kusikilizwa kupitia mashahidi haikuwa granted.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…