Wakili Kibatala anajua sana alifanyalo. Ni lazima akuchanganye tu

Kibatala kumshinda kwake ni uwe unasema ukweli pindi anapokuuliza maswali yake. Sasa kama ukweli wenyewe ndo unakufunga basi itakula kwako
 

Man of the match
 
Ukiona shahidi anahojiwa hadi anapata homa mahakamani ujue hapo hamna kesi!
Mbaya zaidi huyu ndiye aliyefungua jalada la kesi. Huyu anatakiwa ahojiwe hadi kieleweke. Jamhuri hapa wana hali ngumu sana na hii kesi. Naona hata Jaji kishaona muelekeo wa maji.

Ni aibu sana hii kesi, sijui kwa nini DPP hadi sasa yuko kimya, labda wanaogopa aibu ya "Kutokua na nia ya kuendelea na kesi" ukichukulia maelezo ya IGP Siro kwamba wana ushahidi mzito, ambaye nadhani ndiye alimuaminisha Chief kwamba kuna kesi ya ugaidi.

Tusubiri kesho tuone kama Inspector Swila atapanda kizimbani.
 
Mwenzenu anasota kule nyie mnafurahia maswali ya Kibatala, wabongo ni shida sana Tundu Lissu nusu afe ila wabongo waliishia kuongea tu kama hivi na story imeishia hapo hivyo hata ikitokea Mbowe akafungwa hakuna wabongo watakachofanya na hizi sifa za maswali ya Kibatala yataishia hapo hapo.
 
Nafatilia nondo za Kibatala, ningekua mimi shahidi ningetoroka na singerudi tena mahakamani
Aisee, hii kesi inaonyesha kwamba kweli nchi ahitaji tena askari mbumbumbu wa kuitikia kila kitu.

Tunahitaji askari weledi, wanaojua nini walifanyalo, watenda haki, ambao akili zao ziko sharp
 
Na huyu wa leo wa tatu kuugua,
Na cha ziada yeye hujisikia haja mara kwa mara.
 
Aisee, hii kesi inaonyesha kwamba kweli nchi ahitaji tena askari mbumbumbu wa kuitikia kila kitu.

Tunahitaji askari weledi, wanaojua nini walifanyalo, watenda haki, ambao akili zao ziko sharp
Ifike mahali waweke kigezo cha kuwa askari lazima kuwe kiwango cha elimu atlist Degree moja, sasa hawa darasa la saba wanatusumbua sana
 
Mimi siyo Mwanasheria lakini kwa mwenendo wa kesi hii Mbowe na wenzake naona bado wako salama. Serikali ilitakiwa wangoje mpaka wafaye kitendo cha kulipua vituo vya mafuta au kumdhuru kiongozi yeyote ili sasa waanzie pale. Hapo pangeonekana kuna exhibit. Lakini kwa mambo ya hearsay Mhe. jaji najua atatoa hukumu ya haki. Majaji wanatoa sana hukumu ya haki. Ngoja tusubirie.
 
Hivi suppose ni kweli awe anaumwa halafu mara kesho tunasikia ameenda zake hapo itakuwaje?
 
ACHA IBAKI HIVYO HIVYO. Inakuuma nini sasa?
 
Wanakwena kunenepesha ng'ombe siku ya mnada🤣
 
Shida ya kukaririshwa majibu hiyo, anaamgiwa ukiulizwa hivi we jibu hivi, lakini anashangaa anakutana na lundo la maswali na hakupewa majibu ,lazima ashindwe .

Kuutolea ushahidi kitu ulichoshuhudia ni rahisi sana kuliko kitu usichokijua
 
Wale waliohukumiwa vifungo vya maisha katika kesi ya uhaini kipindi cha Nyerere waliwai kufanya walau jalibio moja la kuua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…