Wakili Kibatala anajua sana alifanyalo. Ni lazima akuchanganye tu

Wakili Kibatala anajua sana alifanyalo. Ni lazima akuchanganye tu

Huyu bwana stahili yake ni kukuhoji kwa muda mrefu sana. Yaani kielelezo kimoja kinaweza kwake kikawa na maswali Zaidi ya 25. Ana utaratibu wa kuhoji mpaka kufikia muda wa kuhairisha ili siku inayofuata aje na nguvu mpya na mawazo mapya. Amekuwa sana na utaratibu huo ambao kwa kweli umekuwa ukiwachanganya sana mashahidi.

Shahidi wa leo Swila ambaye leo ilikuwa siku yake ya tatu kuhojiwa tayari ameshachoka sana kwani hakumbuki tena aliyoyaongea juzi wakati akihojiwa na mawakili wengine, leo amekuja tayari kishasahau kila kitu utafikiri hakufanya rehearsal, hii ni ajabu sana.

Baada ya kuona leo anazidi kulemewa ilibidi Wakili wa Serikali anayeongoza jopo lao amsogelee na kumwelekeza amwombe Jaji kuhairisha kwa ajili ya tatizo la kiafya - Shahidi mwenyewe inaonesha alikuwa ana uwezo wa kuendela lakini wakili wake kaamua kuingilia kati ili wakampe nafasi ya kujipanga upya kutokana na namna ambavyo ameshavurunga!

Kibata Mwenyezi Mungu azidi kukubariki sana. Hukumu ya Mahakama ikitofautiana na umma tunavyoona basi Jaji huyu atakuwa na roho ngumu sana.

Anyway Acha Ibaki Hivyo!
Mungu wetu yu mwema, jana, leo, kesho, na hata milele. Kupitia kwa Mawakili wa upande wa utetezi tunauona utukufu wake
 
Kuna suluhisho zaidi ya kuweka mawakili mahakamani ili kuhakikisha kesi inaendeshwa kwa haki? Hii njia yako nyingine ni ipi? Alafu unaposema wanafurahia, kwani hawa wana Jf ndio waliomfunga Mbowe. Busara nzuri na kama kweli unamuonea Mbowe huruma, ongea na waliomtubumu waondoe kesi mahakamani.
Mimi nilitaka wamfikirie mwenzao kule anakonda na wafikirie ni jinsi gani ya kupata suluhisho la kuondokana na haya manyanyaso yote haya ila ajabu ndio kwanza wanafurahia maswali ya Kibatala.
Hata kama hawana la kufanya ila ndio wafurahie maswali ya Kibatala wakati mwenzao hadi sasa keshakonda na wakiamua wanaweza kumfunga na hayo maswali ya Kibatala ndio yatakuwa na msaada upi sasa?
 
N
Ukiona shahidi anahojiwa hadi anapata homa mahakamani ujue hapo hamna kesi!
Na likely, anadanganya.

Kila shahidi ana haki ya kuaminiwa, ila kuaminiwa kunapunguzwa na hali zao kisaikolojia mfano kusahau alichokisema awali, na kikubwa zaidi kushindwa kusimamia kwenye point ya msingi yaani kujichanganya. Kuumwa kichwa n.k
 
Kiukweli huyu jamaa anasababisha nijiulize kwanini sikusomaga Law yani dah! lakini basi ntaendelea kumuelewaga sana tu, PK yuko vizuri zaidi ya kawaida na sana
 
Kuna suluhisho zaidi ya kuweka mawakili mahakamani ili kuhakikisha kesi inaendeshwa kwa haki? Hii njia yako nyingine ni ipi? Alafu unaposema wanafurahia, kwani hawa wana Jf ndio waliomfunga Mbowe. Busara nzuri na kama kweli unamuonea Mbowe huruma, ongea na waliomtubumu waondoe kesi mahakamani.
Wote tunajua kwamba wakitaka kumfunga kivyovyote vile watamfunga bila kujali mmeweka utitiri wa mawakili, hayo ndio mazingira halisi tuliyonayo na hakuna asiyejua ila tizama ni nini sasa kinaendelea? Jibu ni kwamba ndio kwanza mnafurahia maswali ya Kibatala, Mbowe akifungwa mtakuja mtapiga kelele humu mwishowe litapita kama yalivyopita mengine kama ya akina Lissu na tutasubiri tukio lengine. Halafu mtu anauliza sasa tufanye nini? Utajua cha kufanya pale utakapochoshwa na yanayoendelea ila kwa sasa tuendelee tu kukoshwa na maswali ya Kibatala.
 
Tanzania ina wajinga wanaumita wakili msomi kisa anatetea upinzani maswali ya kitoto na ujinga anauliza anachukua neno ya kiingereza anataka maana ya kiswahili mtu anayemchukia askari wa la saba huyo wakili ana akili timamu kweli

Sijaona ujanja wake ujinga mtupu
Mkuu we huburudishwi na maswali ya Kibatala? Utakuwa unakosa burudani, nashangaa Mbowe anakonda kule wakati huku watu huku wanaongeza siku za kuishi kwa furaha wanayopata kwenye maswali ya Kibatala. Hakika Kibatala anatoa burudani.
 
Ifike mahali waweke kigezo cha kuwa askari lazima kuwe kiwango cha elimu atlist Degree moja, sasa hawa darasa la saba wanatusumbua sana
Acha kudharahau darasa la 7, Mahita alisema ana Elimu gani? Jumanne na Kingai? Elimu na uongo vinaingilianaje?
 
Kwahiyo unashauri watu wafanyaje ili mbowe atoke?
Mbowe kutoka tu sio suluhisho la tatizo lilipo, yashatokea mengi na yataendelea kutokea mengine.
Sasa kama tunaona akitoka Mbowe kwa hayo maswali ya Kibatala ndio suluhisho basi sawa tuendelee kufurahia maswali ya Kibatala.
 
Hii ni nchi yetu sote,haijalishi una wadhifa gani muhimu wote ni waTanzania.

Nimekuwa nikifiatilia kesi ya ugaidi inayoendelea katika mahakama chini ya majaji watu katika nyakati tofauti tofauti na sababu mbali mbali.

Wakili Kibatala anastahili lawama,aina ya maswali ambayo amekuwa akiuliza mashahidi upande wa Serekali hayakustahi kuulizwa. Mashahidi wana familia,wana ndugu jamaa na marafiki kisa cha kuuliza maswali magumu,chokonozi na dadisi ni nini ?

Nashauri mamlaka husika ikiwezekana au hata kulazimisha goal za mkono Wakili Kibatala afutwe Uwakili.

Mashahidi wanaomba Ruksa za kujisaidia hovyo hovyo.Mashahidi wanakasirika bila utatatibu, mashahidi wanaugua magonjwa ambayo hata WHO hawayajui.

Naomba kuwasilisha.

Ngongo kwasasa Mwembekiuno.
 
Tena kama inawezekana mahakama itoe amri ili aww anawapa maswali yake kabla ili waandae majibu. Maana si kwa kujinyea kule. Yule bwana shahidi ndie alikuwa mtesi wa ndugu luteni na wenzake lakini leo kageuka kituko.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
1644428435813.png
 
Sheria zina udhaifu sana kwenye hilo swala wakili anaweza kuongea maneno makali na ya kuudhi na ikawa sawa tu.
 
Back
Top Bottom