Natabiri kesho Inspekta Swila hatatokea mahakamani kwa maelezo kuwa hali yake sio nzuri hawezi kusimama au kukaa kuendelea kutoa ushahidi ili wapate nafasi ya kujaribu kujipanga na kutafuta shahidi mwingine. Kwa hali ilivyo Insp. Swila ameelemewa!Mbaya zaidi huyu ndiye aliyefungua jalada la kesi. Huyu anatakiwa ahojiwe hadi kieleweke. Jamhuri hapa wana hali ngumu sana na hii kesi. Naona hata Jaji kishaona muelekeo wa maji.
Ni aibu sana hii kesi, sijui kwa nini DPP hadi sasa yuko kimya, labda wanaogopa aibu ya "Kutokua na nia ya kuendelea na kesi" ukichukulia maelezo ya IGP Siro kwamba wana ushahidi mzito, ambaye nadhani ndiye alimuaminisha Chief kwamba kuna kesi ya ugaidi.
Tusubiri kesho tuone kama Inspector Swila atapanda kizimbani.