Wakili Kibatala anajua sana alifanyalo. Ni lazima akuchanganye tu

Wakili Kibatala anajua sana alifanyalo. Ni lazima akuchanganye tu

Mbowe kutoka tu sio suluhisho la tatizo lilipo, yashatokea mengi na yataendelea kutokea mengine.
Sasa kama tunaona akitoka Mbowe kwa hayo maswali ya Kibatala ndio suluhisho basi sawa tuendelee kufurahia maswali ya Kibatala.
Hujatoa solution ya nini kifanyike sasa. Maana so far kesi ipo mahakamani na hamna kingine kinaweza fanyika zaidi ya kusubiria hakimu akiona kesi ni ya kujibu au laah. Wacha tuendelee na kumsifu kibatala maana kwa sasa hatuna lingine la kufanya
 
Ana upeo mkubwa sana, akikuuliza swali lake usipojibu anavyotaka atamuongezea part B,C, na D ndani ya muda mfupi bila shahidi kutegemea mpaka aingie kingi.

Huyu mtu ni mbaya sana kwa hawa jamaa zangu waliokaririshwa majibu ya kutoa mahakamani, kwa hali hii wataugua sana bora wakubali yaishe.
Acha inyeshe Ili matobo yanayovuja ya zibwe mwisho was siku🤸🤸🤸🤸.
 
Ila Jeshi la polisi lina wapelelezi duni sana !
kuna haja ya serikali kuchunguza elimu zao , Kumbukeni kwamba hawa waliopangwa kutengeneza kesi ya Mbowe ndio wapelelezi Nguli kabisa wa Jeshi la Polisi Tanzania , hawa akina Swilla , Ndowo na timu yao , yaani hapa polisi ndio wamevunja kabati yaani !

Sasa angalieni utopolo wanaoutoa Mahakamani , Kwa kweli ni aibu kwa Nchi
 
Walishathibitisha kuwa hawahitaji wenye uelewa kwani hawapo tayari kubeba magobori😄😄 .
 
Hii ni mbinu sahihi kabisa na imefanywa makusudi kwa sababu hizi;
1. Urio ndio alikuwa mtoa habari mkuu wa kesi nzima.
2. Mkaguzi Swila ndiye aliyekuwa mpelelezi wa kesi hii. Yeye ndio aliyefungua kesi, kupewa maelekezo na Kinga, kuomba vyombo vya uchunguzi kufanya kazi zake na hata kumhoji mtoa taarifa na hata kuandika maelezo ya Kingai.

Baada ya watu hawa, kesi itakwenda haraka sana ili utetezi nao ulete mashahidi wao. Ninahofia kuwa kutakuwa na mashahidi wa utetezi wengi waliohusishwa na Kaaya, Urio na kesi ya ugaidi kuliko Mbowe. Nina dhana kuwa uchunguzi dhidi ya makomandoo inatokana na zile mambo za Kibiti - Mbowe aliingizwa tu baada ya kuona amewasiliana na Urio ambaye alikuwa na kazi ya kuchoma makomandoo wote wasio kazini!!
Uwezekano mkubwa watakuwa hawana kesi ya kujibu baada ya Jamhuri kumaliza ushahidi.
 
Hujatoa solution ya nini kifanyike sasa. Maana so far kesi ipo mahakamani na hamna kingine kinaweza fanyika zaidi ya kusubiria hakimu akiona kesi ni ya kujibu au laah. Wacha tuendelee na kumsifu kibatala maana kwa sasa hatuna lingine la kufanya
Sio kwa sasa tu hamjawahi kuwa na la kufanya, Lissu yule pale katiwa kilema kuna ambalo mlifanya? Ila kama ulivyosema tuendelee kufurahia maswali ya Kibatala na huyo Mbowe muache aendelee kukonda sasa akihukumiwa kabisa sijui itakuaje.
 
Ushahidi wa kujifunza dawa yake ndiyo hiii...ni lazima ujichanganye tu na ndiyo maana mawakili wa Serikali wanakuwa na objection nyingi kujaribu kuokoa mtiririko wa ushahidi mzima wa kesi usiharibike.

Ila washashindwa..hamna kesi humo, TZ hatuko serious, wastage of our nation resources sababu tu za kukomoana kisiasa.
Hahahaa,eti "wastage of our nation resources"
Na wewe unajiita msomi. Unachekesha kweli.
 
Sio kwa sasa tu hamjawahi kuwa na la kufanya, Lissu yule pale katiwa kilema kuna ambalo mlifanya? Ila kama ulivyosema tuendelee kufurahia maswali ya Kibatala na huyo Mbowe muache aendelee kukonda sasa akihukumiwa kabisa sijui itakuaje.
Mungu amefanya kubwa sana. Kuna adhabu kubwa duniani zaidi ya kifo?. Wote waliopanga mauwaji ni marehemu na wengine hawako kwenye nyadhifa zao.
Damu ya mwanadamu haipotei kama Mungu alivyomwambia Kaini.
Waziri wa ulinzi, Katibu mkuu kiongozi, rais kwa mara ya kwanza katika nchi yetu vyote vilitokea. Bado huna la kujifunza?
 
Back
Top Bottom