Wakili Mgongolwa: Katiba inamruhusu Rais kumuongezea muda Jaji Mkuu

Awamu ya tano ndiyo iliyosimika upuuzi huo wa kutengeneza watu maarufu wa kutetea upuuzi wa watawala. Mifano michache inafaa. Uteuzi wa Katibu wa Bunge ulipolalamikiwa kuwa unavunja sheria Mzee Msekwa alikwenda kuchukuliwa kuja kutetea kuwa sheria haijavunjwa kwa kutumia uzoefu wa kipindi chake cha Uspika! Makanisa yalipokosoa mwenendo wa uongozi wa nchi, msomi mmoja mhadhiri wa chuo kikuu alitumika kuandika barua ya kujibu na kukosoa mamlaka ya kanisa lake kwa kitendo hicho.
 
Mgongolwa ni mlamba matako wa CCM, hawezi kusema kitu chochote cha tofauti na hiki.
 
Kuna msemo UNASEMA HIVI" Mchungaji akisema NG'OMBE kafia machungani, ATAKUWA kafa kweli".jaji mugasha ni mchungaji na katiba ni..........
 
Huyu wakili anabembeleza teuzi, ndiye aliwadanganya yanga watashinda kesi dhidi ya Morison CAS lakini wakaangukia pua.
Aendelee hukohuko TFF lakini akija mahakamani atabwagwa vibaya.
Tatizo Mawakili wakiishasikia zimwi limeingia nchini basi hata Mawakili uchwara wanatafuta kiki humo humo.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo viongozi wote ataowaapisha kuanzia sasa ni viongozi batili siyo?

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Katiba inasema "...Jaji wa mahakama ya rufani aliyetimiza umri wa miaka 65.....".

Hapa katiba haisemi "......Jaji mkuu aliyetimiza umri wa miaka 65...". Na tumbukeni kuwa "u - Jaji mkuu" ni cheo cha madaraka.!!

NB:
Ni kweli Prof. Ibrahim Juma ni Jaji wa mahakama ya rufani lakini alikuwa na madaraka ya "u - Jaji Mkuu wa Tanzania"...

Kwa hili katiba iko very clear, yaani anapaswa kustaafu na kuacha madaraka ya "ujaji mkuu" with immediate effect ili mwingine ashike madaraka hayo...

Baada ya hapo kama Rais anataka, kumwongezea muda zaidi ili aendelee kuwa "Jaji wa mahakama ya rufani " tu, anaweza kufanya hivyo!!
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Kwahiyo kuendelea kuwa JAJI anaruhusiwa ila KUWA JAJI MKUU HARUHUSIWI KISA UMRI?
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Kwahiyo kuendelea kuwa JAJI anaruhusiwa ila KUWA JAJI MKUU HARUHUSIWI KISA UMRI?
Absolutely, Yes..

Sio mimi. Ila katiba ndo inasema hivyo

By the way, hivi mtu umefikisha umri wa miaka 65 bado unang'ang'ana na purukushani za kwenye maifisi, ya nini hayo yote?

Kwani asipumzike na kulea wajukuu? Ina maana katika majaji wote tulio nao Tanzania, hakuna anayefaa uwa Jaji Mkuu iipokuwa Prof. Ibrahim Juma pekee??

Na hivi huyu ni Mzanzibari au Mtanganyika.??
 
Ccm irekebishe katiba ili RAIS ARUHUSIWE KUJIONGEA MUDA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…