Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Soma vizuri maoni ya Jaji Mugasha yameandikwa kwa Kiswahili utaelewa. Kama huna kopi sema nikutumieWapi wamesema ISIPOKUWA JAJI MKUU? unacho hiko kifungu ambacho kinasema JAJI MKUU HARUHUSIWI KUONGEZEWA MUDA?
Kwanini majaji wakuu waliopita walisema hay?Pamoja na yote aliyoandika Jaji Mugasha ukweli unabaki palepale Katiba imempa Rais mamlaka ya kumuongezea muda JM
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Kwahiyo kuendelea kuwa JAJI anaruhusiwa ila KUWA JAJI MKUU HARUHUSIWI KISA UMRI?
MKURYA sasa sijui ni MZANZIBAR AU NI MTANGANYIKA BROAbsolutely, Yes..
Sio mimi. Ila katiba ndo inasema hivyo
By the way, hivi mtu umefikisha umri wa miaka 65 bado unang'ang'ana na purukushani za kwenye maifisi, ya nini hayo yote?
Kwani asipumzike na kulea wajukuu? Ina maana katika majaji wote tulio nao Tanzania, hakuna anayefaa uwa Jaji Mkuu iipokuwa Prof. Ibrahim Juma pekee??
Na hivi huyu ni Mzanzibari au Mtanganyika.??
Jaji Ramadhani alistaafu Tar ngapi? Unajua?Kwanini majaji wakuu waliopita walisema hay?
10. Nilibahatika kupata nakala tajwa kupitia kwa Mhe. Jjaji Mkuu Augustino Ramadhani na ilikuwa hivyo kwa Majaji wengine waliokuwepo wakati huo. Vilevile, katika mkutano wa Majaji wote uliofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto, Arusha, mnamo Septemba 2007, Mhe. Jaji Mkuu Augustino Ramadhani (Hyt) alibainisha kuwa, yeye mwenyewe atastaafu katika nafasi ya Jaji Mkuu atakapotimiza umri wa miaka 65 na hataongeza hata nusu saa kwa vile Katiba hairuhusu nyongeza na akatuasa tujiandae kuwa na Jaji Mkuu mwingine.
Hahahaaaaa. Nikumbushe tafadhari.Jaji Ramadhani alistaafu Tar ngapi? Unajua?
Japo mimi ni wakili, ila mimi sio wakili msomi, mimi ni wakili mtangazaji.
Katiba yetu iko wazi kabisa kwa teuzi zote za rais, akiletewa majina, akaona wote hawatoshi, ana mamlaka ya kumuongezea muda aliyepo kisha kutafuta wa kutosha. Hili limekuwa likifanyika siku zote na hakuna tatizo lolote!.
P
Kwa hiyo kati ya hayo MAONI ya MAJAJI na KATIBA TUFUATE KIPI?Kwanini majaji wakuu waliopita walisema hay?
10. Nilibahatika kupata nakala tajwa kupitia kwa Mhe. Jjaji Mkuu Augustino Ramadhani na ilikuwa hivyo kwa Majaji wengine waliokuwepo wakati huo. Vilevile, katika mkutano wa Majaji wote uliofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto, Arusha, mnamo Septemba 2007, Mhe. Jaji Mkuu Augustino Ramadhani (Hyt) alibainisha kuwa, yeye mwenyewe atastaafu katika nafasi ya Jaji Mkuu atakapotimiza umri wa miaka 65 na hataongeza hata nusu saa kwa vile Katiba hairuhusu nyongeza na akatuasa tujiandae kuwa na Jaji Mkuu mwingine.
Unaposema Jaji wa Mahakama ya Rufani lakini sio Jaji Mkuu unamaanisha nini, unafaham Jaji Mkuu anatokana na Majaji wa Mahakama ya Rufani, na ndiye Jaji wa Rufani namba 1 (JR1)? Unafahamu kwa sababu hizo unapotaja Majaji wa Mahakama ya Rufani JM ambaye ni JR1 ni sehemu ya hilo kundi?Kweli wewe ni mtangazaji, jambo la kustaafu sio la dharura mkuu.
Mara tu Jaji Mkuu anapoteuliwa lazima kuwe na pool za potentials CJ.
Unawaza vipi kama jaji mkuu akifa, au ndo mambo ya kukaimisha?
Afu huyu mgongolwa atambue Jaji wa mahaka ya rufani lkn sio Jaji mkuu. Hiko kifungu ni kama huna kofia ya ujaji mkuu.
Wewe ni wazi hujasoma sheria na hujui muundo na composition za Mahakama hasa Mahakama ya Rufaa ambayo ndio inatoa Jaji Mkuu, nakushauri kasome kwanza kuhusu JM na JR1 ndio urudi kuchangia tena, usiivue nguo kiasi hiki hadharaniJaji Mkuu ni nafasi ya uongozi. Hivyo imewekewa ukomo kikatiba wa umri wa kustaafu wa jaji wa rufani ambao ni miaka 65.
Umesoma kwanza barua ya Jaji Mugasha?Wewe ni wazi hujasoma sheria na hujui muundo na composition za Mahakama hasa Mahakama ya Rufaa ambayo ndio inatoa Jaji Mkuu, nakushauri kasome kwanza kuhusu JM na JR1 ndio urudi kuchangia tena, usiivue nguo kiasi hiki hadharani
A simple logic is that huweze Kuwa JM bila kuwa JR? ni akili ndoogo tu ya kutumia hapaKatiba inasema "...Jaji wa mahakama ya rufani aliyetimiza umri wa miaka 65.....".
Hapa katiba haisemi "......Jaji mkuu aliyetimiza umri wa miaka 65...". Na tumbukeni kuwa "u - Jaji mkuu" ni cheo cha madaraka.!!
NB:
Ni kweli Prof. Ibrahim Juma ni Jaji wa mahakama ya rufani lakini alikuwa na madaraka ya "u - Jaji Mkuu wa Tanzania"...
Kwa hili katiba iko very clear, yaani anapaswa kustaafu na kuacha madaraka ya "ujaji mkuu" with immediate effect ili mwingine ashike madaraka hayo...
Baada ya hapo kama Rais anataka, kumwongezea muda zaidi ili aendelee kuwa "Jaji wa mahakama ya rufani " tu, anaweza kufanya hivyo!!
Jaji wa Rufaa no 1 sio JMYaani wewe ni Wakili msomi lakini hujui JM ndiyo JR1, au uliiba mtihani Law School?
Naona umeamua tusielewane basi tukubaliane kutokukubaliana.Jaji wa Rufaa no 1 sio JM
Ni sawa na J1 sio JK
Hizo no ni seniority tu. Na Jaji wa Rufaa no 1 ni the most senior kwa maana ndo aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa siku nyingi kuliko majaji wenzake wa Rufaa
Same kwa Jaji wa Mahakama Kuu no 1 yaani J1 huyu ndo anakuwa the most senior kwa wenzake wote yaani kwa tarehe ya kuteuliwa.
Mahakama ni muhimuli unaoheshimu sana seniority. J34 hawezi kuondoka kwenye kikao kama J10 amekaa na hata kama ana udhuru lazima amuombe udhuru huyo J10