Wakili Mgongolwa: Katiba inamruhusu Rais kumuongezea muda Jaji Mkuu

Lete kifungu sio porojo tu
 
Sijui kwanini hili limekuwa controversial... mbona hizi power anazo muda mrefu tu. Labda kama hajafanya kama katiba inavyomtaka.
 
Pasco uwe unafanya research kabla ya kuandika unajua kuna watu wengine wanarely sana kwako.Usije ukawalisha matango pori
 
Rais ana mamlaka makubwa sana hata akiamua kujiongezea muda wake hakuna wa kupinga tutaishia kulalamika tu na hatuna cha kumfanya.

Jaji kuongezewa muda au kutokuongezewa sisi huku kwetu misigiri maisha ni yaleyale tu.
Hata na sisi wa huku Ulemo maisha yanaenda tu !!

Kila siku watu wanaambiwa Katiba tuliyonayo imempa madaraka makubwa kweri kweri Mkuu wa Nchi lakini bado watu wanahoji na kujidanganya eti Mkuu kuna mahali amevunja katiba !!

Labda aje Mwanasheria kutoka sayari ya mars ndio atagundua ipo sehemu Katiba imevunjwa !!
 
So Rais anaijua vyema katiba ya Nchi hii kuliko wanasheria wenyewe? Kuna wapumbavu na vyeo vyao wanafanya ubumbavu kuliko ule upambavu aliyofanyiwa kwa imani ya ki kristu na Yuda .
Bear in mind URais ni Taasisi !! Tena ni Taasisi kubwa Kweli Kweli iliyosheheni wabobezi wa fani zote zinazohitajika kumfanya Mkuu afanye maamuzi yasiyo ya kukurupuka !!

Watu wengi hujifanya wanajua kuliko wanavyojua ndio maana kelele nyingi huwa zinapigwa lakini baada ya muda mfupi utasikia kimyaaaa !!
 
ibara ya 120 inaongelea jaji wa mahakama ya rufaa (sio jaji wa mahakama kuu). CJ ni jaji wa mahakama ya rufaa na hata sasa anakaa kwenye jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufaa kuamua kesi za rufaa. Kuna vitu viwili, cheo cha jaji wa mahakama ya rufaa na cheo cha CJ. kawaida CJ Ni jaji wa mahakam ya rufaa sawa tu na wezake ila yeye anacho cheo kingine cha ziada ambacho pia ni cha kikatiba, cheo cha CJ. kumbuka kwamba, sio majaji wote wa mahakama ya rufaa ni maCJ, cj ni mmoja tu anayeteuliwa miongoni mwa majaji wa mahakama ya rufaa. ibada ya 118 inaleta ukomo wa cheo cha CJ that means akitaka kuendelea kuongezewa muda hataongezewa muda wa UCJ kwasababu katiba haijatoa huo mwanya, bali ataongezewa muda wa kuendelea na cheo kile kingine cha jaji wa mahakama ya rufaa ambacho ibara ya 120 inaruhusu kuongezewa muda.

hivyo ni vyeo viwili tofauti vinavyotolewa na ibara mbili tofauti na vyenye masharti mawili tofauti. kilichoruhusiwa kuongezwa ni cheo cha ujaji wa mahakama ya rufaa ila ucj hakuna kifungu kinachoruhusu kuongezewa muda. na kwa minajiri hiyo, ule waraka wa mama mugasha utaprevail kwamba anachokisema ndio cha kweli.
 
Hivyo ni vyeo viwili tofauti hata mishahara na marupurupu na instrumental zao za kazi ni tofauti.
Mbona Waziri Mkuu au Mawaziri wote ni wabunge ila vyeo vyao ni tofauti
umeongea vizuri. waziri ni mbunge ila sio mbunge ni waziri. waziri ambaye ni mbunge uwaziri wake ukitenguliwa anarudi kwenye cheo chake cha kawaida kama mbunge. mbona rahisi sana kuelewa ila watu wanataka kujustify.
 
Kwa hiyo alichokiandika Mh Jaji ni sahihi au sio sahihi?
Naomba unisaidie kama hutajali.....natanguliza shukrani.
Mayala mkuu kashakwambia ni ka utamaduni tu hakuna kifungu chochote cha sheria alichofafanua kinachompa mamlaka raisi kumwongezea mda jaji mkuu kwa hiyo na yeye yupo njia panda kumbuka mayala amekwambia ni wakili mtangazaji [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ndio ni taasisi kubwa ,nakubali ila sasa kikowapi, inakubali limkataba la ajabu namna hii, that's pia watu wanashangaa
 
Pasco uwe unafanya research kabla ya kuandika unajua kuna watu wengine wanarely sana kwako.Usije ukawalisha matango pori
Mkuu ras jeff kapita , kwa mujibu wa katiba ya JMT, rais wa JMT ni an executive president, anaruhusiwa kushauriwa lakini kwenye kufikia maamuzi, anafikia maamuzi yeye kama yeye, bila kuwajibika kufuata ushauri wa yeyote!.

Maamuzi pekee ambayo rais wa JMT ni lazima ayafuate ni Azimio la Bunge, na kuwasilisha ripoti ya CAG Bungeni.

Na kwenye uteuzi, rais atapokea majina pendekezwa kutoka mamlaka ya ushauri ili kuteua, akiwaona wote walioletwa hawatoshi, anamuongezea muda aliyepo na kutafuta mwingine!. Nyerere alifanya, Mwinyi alifanya, Mkapa alifanya, JK alifanya, JPM alifanya, na sasa Mama Samia anafanya!.
P
 
Wakili Mtangazaji,kweli?
Yes mimi ni Wakili Mtangazaji, na sio Wakili Msomi!. Fani yangu rasmi ni mtangazaji, nikasoma LL.B nikiwa mtangazaji, nikahitimu LL.B with honors from UDSM nikiwa mtangazaji, na baada ya kuhitimu, nimeendelea na utangazaji, nimepata uwakili nikiwa mtangazaji, sasa ni wakili na bado ni mtangazaji.
P
 
Wewe ni Mwanasheria mbobezi hutakiwi kujibu mambo kijumla jumla, namna hii, chambua vifungu na facts kupingana na hoja za mh.jaji Mugasha.kwanza kabisa suala la muda wa Jaji Mkuu kustaafu halikwepo kwenye katiba kipindi cha nyuma enzi za Mh.Jaji Francis Nyalali aliyehudumu kwa miongo, na pindi alipofikisha miaka 65 kulitokea mjadala na hata yeye alikiri hakuna mahali pameandikwa masharti ya Jaji Mkuu kustaafu.baada ya lacuna hiyo kwenye katiba na kuthibitika ni kweli, ndio haraka muswada ukapelekwa ili kutambua umri wa kustaafu kuwa ni umri wa jaji wa rufaa.katika ibara ya 118 yote zaidi ya hilo sharti hakuna kipengele mahususi kuhusu kuongezewa muda kama Jaji mkuu.vipengele vyote vingine vinataja kuhusu jaji wa rufaa na jaji wa mahakama kuu kuongezewa muda.hivyo basi kama andiko la jaji mugasha lilivyoeleza ,kwakuwa specifically ibara husika haijataja mahususi kuhusu jaji Mkuu, inamaanisha watunga sheria walikuwa na maana husika,otherwise ujaji mkuu ungekoma halafu aendelee kama jaji rufaa.so kuna lacuna kwenye hili.lakini kwakuwa ni maamuzi ya mh.rais yabidi yaheshimiwe na hayawezi tenguliwa,ila tu ni challenge wamepewa wanasheria kuchangamsha akili kuja na rival submissions ili kujiongezea uwelewa, na ndio raha ya sheria, kila mtu anapambana upande wake anaoona upo sahihi ukubalike👍😂
 
Mgongolwa ni wakili wa cheti FEKI. Nawatahadharisha wateja wake, mkipoteza kesi zenu mahakamani msije kutulalamikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…