Wakili Mwabukusi: Rais Samia atusikie, Mkataba wa Bandari haulindi uhai wa Nchi yetu

21 June 2023
Profesa Lipumba - Suala la Bandari , Abu Dhabi ndiyo baba wa UAE siyo Dubai....


Mtawala wa Abu Dhabi ndiyo rais wa UAE huku mtawala wa Dubai ni Makamu wa Rais wa UAE ....

Kimataifa Dubai siyo nchi nyenye sovereign na makao makuu ya UAE ni Abu Dhabi. UAE pekee ndiyo ina shughulika na ulinzi na mashirikiano ya nje ya kimataifa baina ya nchi na nchi ...

Profesa Lipumba anakwenda mbali na kuonya kuwa mkataba huu wa nchi ya Tanzania na sehemu ya shirikisho la Emirati UAE unatutengenezea mgogoro na Abu Dhabi bila kusahau mgogoro na nchi ya UAE.

Profesa Lipumba anaongeza ni bora mkataba mzuri wa kuhusu bandari ungeingiwa na Abu Dhabi sehemu ya UAE iliyo tajiri zaidi ya Dubai na pia Dubai inaitegemea zaidi Abu Dhabi kiuchumi inapotetereka ...

 
Kama sio 'sehemu ya mkataba' huu atatusikia, ila kama 'ndio hivyo tena' sidhani kama atatusikia!
 
Amekamisha mamlaka ya ufafanuzi kwa akina kitenge
 
Kwanza wabunge wenyewe wanajitambua?

Huyu Mwambukusi nitakwenda kumchukulia form ya ubunge 2025 kwa gharama zangu
 
Muda mwingi ametumia kusifu matarajio ya mapato badala ya ukakasi wa mkataba wenyewe. Nilijaribu kupiga simu kumwuliza swali ambalo hadi sasa sijapata jibu.
Hawajitambui
 
Lawyer Mwabukusi ni wale wale tu wanaoumia awamu ya sita. Karamagi na team yake nzima ya TICTS wamekula kwao mazima.
 
Huyo jamaa anajiita Lord Denning ni bonge la kiazi. Ila halijijui kuwa ni likiazi.
SSH anaendeleza reforms za marehemu JPM na anazifanya vizuri sana.

Hizi kelele ni za wale wanaokwenda kuumizwa na hayo mabadiliko ya kiuchumi. Kila kizuri kina gharama zake hivyo wanaolalamika ni lazima wawepo.
 
Tatizo hela waliyopewa na muarabu wameishaitumia
 
Yaan huyu wakili anajidai anaufaham mkubwa kuhusu mikataba kuliko uvccm? Tena wakiongozwa na Lord denning na covax? NB; Uvccm ni akili kubwa san!!!
 
Kazi ya wabunge ni ipi ikiwa kila mtu anatakiwa afike Dodoma kutoa maoni yake?.

Nini faida ya kampeni za uchaguzi kutumia mabilioni ya pesa mara moja kila baada ya miaka mitano ikiwa kwenye suala moja tu tuanzishe urasimu usio na mantiki yoyote?.

Reforms zina gharama yake tena kubwa na zinaumiza baadhi ya taasisi, sisi sio wa kwanza kufanya mabadiliko ya kiuchumi, hivyo tuwe wapole tu wakati sindano zikiwa zinaingia, baada ya muda tutakuwa tumepona.
 
NI msaliti na mbinafsi, hata kwenye swala la Ngorongoro alitumika hivi hivi.
 

Lakini umesikia pia kodi ya mafuta atakatwa mtanzania shilingi 100, na cement itaongezwa shilingi mia200? Kama kuna hela huko bandari kwann kodi zinaongezeka mkuu?

Changamsha ubongo mkuu” wewe unaamini watz hawana uwezo wakuendesha bandari mpaka waje hao jamaa?

Na shida sio kuwekeza waseme hawa watu mkataba wa miaka mi ngapi
 
Tunaunga mkono hoja kamwe Tanganyika haitaenda kizembe namna hii tutaitetea nchi yetu kwa gharama yeyote ile
 
Wapi imeandikwa DP world akija ndio mafuta atakatwa mtanzania sh 100? na hata ikiongezwa shida ikopo wakati kitakachoingia ni kingi zaidi, Tibaijuka ameshindwa kujenga hoja kwanini DP world asije kuwekeza Tz., hoja yake kubwa ni US walikataa 2006 lakini kashindwa kufafanua kwanini Uingereza DP World kapewa bandari 2 anaziendesha hadi sasa na nchi nyengine pia,

Sasa kama Muna uwezo wa kuendesha bandari kampuni ya Tiks imepewa hiyo bandari miaka mingapi kashindwa kuifanya bandari ya Dar es salaam kuwa ndio lango kuu la biashara, nchi kama Zambia, Uganda, kenya na nyengine zikakimbilia maeneo mengine? Mama anataka kuifungua Tanganyika mnaleta kauzibe

Hata akipewa bandari kwa miaka 100 shida iko wapi? lengo ni impact kuwaondoa watanzania na umasikini wao uliokubuhu na uchumi kukua., toka CCM ishike madaraka hakuna chochote mnapiga mdomo tu,

Watu wako mbali sana kiuchumi nyinyi eti bandari yetu hatutaki watu wananchi wanakufa na njaa, unataka ufe na utamu wako badala kutafuta namna kuleta maendeleo, siasa zenu za kishamba sana Mama hatakubali upuuzi wenu DP world yupo njiani bunge lishapitisha, Watanganyika ni watu waliolala usingizi wa pono, wavivu, waoga kupindukia.
 
Kwanini walikwenda Dubai, Je walielewa safari ya Dubai, maswali ni mengi kuhusu wabunge waliosafiri kwenda Dubai.

AIDA KHENANI WA CHADEMA AIBUA JAMBO SAFARI YAO YA TAREHE 28 JANUARY 2023 KWENDA DUBAI

Barua ya katibu wa bunge kuwataarifu wabunge haikusema kwa uwazi .... safari hii ya Dubai ... watu ni wachache bandarini Dubai tofauti na bandari ya Tanzania zilizojaa wafanyakazi .... mfumo wa kifalme Dubai haufanani na mfumo wetu wa jamhuri wa kidemokrasia ... maswali ni mengi alijiuliza mbunge huyu wa CHADEMA. Haya tusikilize wenyewe mbunge huyu makini akiweka wazi kila kitu alichojiuliza katika kutafakari sana ...
Source : SK Media Online TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…