kibobori mahoro
JF-Expert Member
- Dec 12, 2022
- 7,452
- 10,785
Ndio maana JPM aliwekwa pembeni, alikuwa mzalendo namba moja.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
PROFESA TIBAIJUKA ASTUKA NA KUFADHAISHWA NA UWEZO WA KUFIKIRI WA 'WANAWE' WAANDISHI VIJANA
Prof. Tibaijuka ashangaa maswali na hoja za waandishi wa habari katika sakata hili la mkataba wa DP World
Ni pale mwandishi alipouliza kuna tabu gani Kuwapa taarifa Dubai kila wakati wakati (Kifungu 4.2 cha mkataba) tunataka kufanya masuala ya sovereignty... profesa anashangaa waTanzania kutojipenda na kukubali kudharauliwa kutokana na maneno yalivyosukwa katika mambo makubwa na waandishi wanayachukulia kimasihara ... kuwa kuitwa kujieleza mbele ya Dubai ni suala la kishikaji / partnership wakati mkataba huu haupo hivyo Tanzania haina usemi katika mkataba huu mbovu ...
Ukimya wake ndio unaonesha vile hatoshi kukalia kile kiti, amepwaya sana, sasa ndio atajua kuitwa Rais maana yake nini, sio kuuza sura tu na misafara ya vin'gora.Mama naona kama ana kiburi,mbona kanyamaza kimya kama hayamuhusu vile, kwanini Mkuu wa nchi unanyamaza kimya kwenye suala nyeti kama hili na wakati kwenye nyaraka saini yake ipo?hii inamaanisha nini jamani!
Mzee Mkapa aliposhutumiwa na sera yake ya ubinafsishaji mashirika ya Umma na migodi,alitokeza kufafanua na Mzee Kikwete vilevile kwenye sakata la Richmond na IPTL Escrow Account alitoa ufafanuzi.
Kulikoni Rais Samia?
Kimbukeni ata sakata la mgomo Kariakoo,napo alikaa kimya kama hayupo na alimuhusu!
JPM ndio chanzo cha mkataba huu wa DPW, majadiliano aliyofanya na Kagame 2016 ndio yameileta hii kampuni na ndio yamewezesha ujenzi wa SGR kwa trilioni 16 fedha za Tanzania.Ndio maana JPM aliwekwa pembeni, alikuwa mzalendo namba moja.
SSH ni mtulivu mwenye kupima kabla hajaongea au hajafanya maamuzi. Anajua ukubwa wa adui anayepigana nae pale bandarini.Ukimya wake ndio unaonesha vile hatoshi kukalia kile kiti, amepwaya sana, sasa ndio atajua kuitwa Rais maana yake nini, sio kuuza sura tu na misafara ya vin'gora.
Hahaha sawa sawa mzee dp worldWazalendo uchwara.
Profesa Lipumba anakwenda mbali na kuonya kuwa mkataba huu wa nchi ya Tanzania na sehemu ya shirikisho la Emirati UAE unatutengenezea mgogoro na Abu Dhabi bila kusahau mgogoro na nchi ya UAE.
Some of the distinct features of the UAE's heritage are hospitality, tolerance, family cohesion and solidarity among members of the society along with honour and pride associated with being part of this heritage. However, the emirs of Abu Dhabi and Dubai have effective veto power in elections for the role of President. The last presidential election was held in 2009.
Wasiwasi wa profesa Haruna Lipumba kuhusu mgongano Tanzania walioupika kiaina baina ya Abu Dhabi na Dubai hivyo Tanzania kwenda kuambulia patupu, kaka mkubwa Abu Dhabi alikuwa anafukuzia mradi huu kwa ushirikiano na kampuni ya kubwa ya India Adani.
Wazee wa taifa wajitokeze haraka kumshauri rais kwa heshima kuwa kuwa wajisahihishe kuurejesha mkataba huu tena bungeni ....[emoji419][emoji375]WAKILI MWABUKUSI: Rais Samia atusikie, Mkataba wa Bandari haulindi uhai wa Nchi yetu
Katika mahojiano leo na wakili Mwabukusi anaangazia mambo zaidi kamati ya bunge, uwakilishi wa muswada wa mkataba bungeni na jinsi muda finyu waliopewa wabunge kuujadili ...
.
Wabunge Halima Mdee, Aida Kenani pamoja na Luhaga Mpina ambaye hakupata nafasi bungeni kuwakilisha hoja hivyo kuwakilisha maoni nje ya bunge kwa maandishi watambuliwe kwa kupewa maua yao hayo bila kumsahau dada yetu mpendwa wa taifa Mange Kimambi amesema wakili msomi Boniface Mwabukusi
Aliyevujisha mkataba ni mzalendo halisi na hii inatia moyo kuwa bado kuna Wazalendo wachache ndani ya serikali... na huyu atambuliwe wajibu wake mkubwa kulinda maslahi ya taifa
Serikali inawajibika kwetu umma yaani wananchi hivyo viongozi wote serikalini watambue mamlaka zote tulizowapa ni zili zilizotamkwa katika katiba kama hawawezi waache nyadhifa zao waende nyumbani ...
Advocacy tunayofanya ni kazi ya kuelimisha wananchi na ndiyo wajibu wetu kwani waziri Mbawara katika hadhira tofauti tofauti anasema mkataba huu ni makubaliano na akifika mbele ya viongozi wa dini n.k wanasema mkataba ...
Viongozi waache propaganda kwa kwenda sehemu mbalimbali Tanzania kupotosha wananchi kuwa marekebisho yatafanywa... hata wakienda mpaka kilele cha mlima Kilimanjaro haitasaidia kuzimisha kelele za wananchi ...
Linalotakiwa ni bunge hili hili lirudi haraka ili kwa kikao cha kingine liupitie tena maana ni hitajito la kikatiba wakati kunapotokea hali kama hii tunayoiona badala ya kujaribu kuutetea mkataba huu mbovu ...
Bunge halina uwezo wa kuita watu kuwahoji hata pale walipowatisha kwa kuwaita kina Paschal Mayalla, Dr. Reginald Mengi na wengine ni batili. Kwa bunge haliwezi kuwa prosecutor na mahakama
Kumtishia balozi Dr. Wilbrod Peter Slaa ambaye ni Whistle blower bona-fide kuwa aitwe bungeni ahojiwe kuhusu press conference zake za kuhusu sakata la DP World, hili ni kinyume cha katiba na batili maana bunge halina mamlaka hayo....
Hata mimi Boniface Mwabukusi nikiitwa Dodoma siwezi kutishwa na sitakwenda maana ni wito batili na haramu wala kukidhi sheria na katiba yetu kwa kuwa bunge halina mamlaka hayo
Mikataba ya kunyonya Mali ya asili yetu haikubaliki ni mikataba pekee ambayo ina manufaa kwa taifa na muwekezaji ndiyo tunayoiafiki siyo mkataba mbovu kama huu ...
Tunawashukuru wananchi kwa kupaza sauti katika suala hili ..... maana sasa Bunge halitaweza tena kututia vitanzi kama hivi vya DP World, Loliondo, Madini n.k bila wananchi kuhusishwa kimamilifu na siyo kuburuzwa ....
Kuna masharti yasiyo general policy ndani ya mkataba .... reciprocacy hakuna, huu mkataba una mlinda mwekezaji badala ya kumpa haki ya kudai fidia pale anapodhulumiwa...
High level consultation kwa kutumia katiba yetu Ibara ya 27.1 ya raia kuwa na haki ya kulinda Mali inafanyika na si muda mrefu waTanzania watapewa mrejesho na watafahamishwa
Ibara ya 28 ya katiba hairuhusu mtu yeyote kumilikishwa eneo lolote bali inaruhusiwa kutumika kwa shughuli hivyo mwekezaji hatakiwi kumilikishwa bali kuendesha shughuli za kibiashara ...
Bungeni kulikuwa na tukio na siyo mjadala maana hakuna mwanasheria mkuu hakuoneshwa siku hiyo na mwanasheria mkuu ana kiti chake maalum bungeni lakini hakuwepo na badala yake spika wa bunge kuliteka bunge kinyume na uendeshaji wa bunge huku akiwadhalilisha, kuwa harass wabunge Halima Mdee, Aida Kenani na kulibadilisha bunge kuwa kama darasa la chekechea / kindergarten la a,e,i,o,u huku dhihaka za kutunzana noti, miluzi, kugonga meza kiasi cha bunge kuwa eneo mithili ya ngoma ya mchiriku wakati jambo muhimu la eneo la nchi linamilikishwa kwa taifa lingine geni milele
Ya fuatayo yarekebishwe katika mkataba huu wa DP World katika yafuatayo : Sheria za nchi zizingatiwe masuala ya umilikaji ardhi, umilikaji wa bandari, uvunjwaji wa mikataba, tusikatazwe kutwaa eneo pale usalama wa taifa unapotishiwa tofauti na mkataba huu unavyotukataza kitu ambacho ni kinyume na katiba, spika aache kuligeuza bunge kuwa kikaragosi cha serikali, maandamano yaratibiwe maana katiba inaruhusu
Ushauri kwa Mh. Samia Hassan, ni kuwa mimi nina mashaka rais amepotoshwa maana hata wataalamu kama mwanasheria mkuu hakuonekana ndani ya televisheni siku ya tarehe 10 June 2023 jumamosi mjini Dodoma. Pia namshauri mchakato wa haraka ufanyike Serikali iurudishe mkataba huu tena bungeni na utaratibu wote utumike kikamilifu na uwazi mkubwa kusuka upya mkataba huu tata.
Freeman A. Mbowe ameeleweka na watu wenye uwezo wa kufikiri ila kuna watu wanataka kupotosha ujumbe mzuri aliowakilisha
Ni nchi mbili tu yaani Palestina kule mashariki ya kati na Tanganyika hapa Afrika Mashariki nchi zao zimepotezwa .....
Rais amwelekeze waziri aliyemkasimisha madaraka (Delegata potestas non potest delegari) kujiuzulu maana alimuamini waziri hakutumia imani hiyo vizuri lakini sasa amemuingiza katika matatizi makubwa na pia mkataba huu urejeshwe bungeni tena maana paka akifungiwa chumbani katika kona paka huyu huweza kujigeuza Simba... pia Spika Tulia Ackson ajiuzuli nafasi yake mara moja ya uspika kwa kushindwa kulipa bunge na wabunge nafasi ya kuishauri serikali kwa uwazi hilo linawezekana maana Job Ndugai alijiuzulu kufuatia utata ... na kadhia hii ya bandari ni moto kuliko ya Job Ndugai spika aliyepita ..
Wazee wa taifa wajitokeze haraka kumshauri rais kwa heshima kuwa kuwa wajisahihishe kuurejesha mkataba huu tena bungeni ....
Wewe unadhani huu mkataba ni sawa na vidonge vya majira??Kazi ya wabunge ni ipi ikiwa kila mtu anatakiwa afike Dodoma kutoa maoni yake?.
Nini faida ya kampeni za uchaguzi kutumia mabilioni ya pesa mara moja kila baada ya miaka mitano ikiwa kwenye suala moja tu tuanzishe urasimu usio na mantiki yoyote?.
Reforms zina gharama yake tena kubwa na zinaumiza baadhi ya taasisi, sisi sio wa kwanza kufanya mabadiliko ya kiuchumi, hivyo tuwe wapole tu wakati sindano zikiwa zinaingia, baada ya muda tutakuwa tumepona.
TICS ilishaondoka na wala haiwezi kurudi, tunataka mkataba kama huo ukivurunda tunakuondoa tunaweka mwingine, mkataba kijini jini hapana, ukishapewa jini umepewa likufanye vizuri au vibaya hauwezi kulifukuza.Huyu Tibaijuka si 'mali' ya Karamagi?
Anatetea biashara ya "mtu" wake?
Nioneshe mkataba mmoja duniani udioweza kukosolewa, ambao hauwezi kuwa challenged mahakamani.Jambo la kumshukuru sana Mungu, kila mtanganyika mwenye kuitakia mema Tanganyika yake tunaongea lugha moja.
Ajabu sana, watanganyika waliotakiwa kutoa maoni yao kuhusu hili suala walitakiwa kufika Dodoma tarehe 5, ili kufikia tarehe 6 saa 7 mchana wawe tayari kwa kutoa maoni.
Wakili anashangaa, inawezekana vipi kwa mtanganyika anayeishi Kigoma, Sumbawanga, Kagera, Ukerewe, Arusha na kwingineko wote wafike Dsm kutoa maoni yao siku inayofuata?
Watu wameitwa kuja kutoa maoni, ajabu mkataba wenyewe haujawekwa wazi, mtu anatakiwa kutoa maoni akiwa anajua nini anachozungumza, baada ya kupata muda wa kutosha kuuchambua mkataba, sasa unapowaficha mkataba, unataka wakazungumze kitu gani?!
Wakili anazidi kushangaa, kumbe bunge lilishaandaa Azimio la kupitisha mkataba, kabla hata bunge halijapitisha ule mkataba! huu ni ushetani kabisa.
Wakili anaendelea kusema, bunge badala ya kumshukuru Dr. Slaa kwa kuwa whistleblower, wao wanataka kumuita ili wamhoji, anadai bunge ni kinyago chetu tulichokichonga wenyewe, hakiwezi kututisha, zaidi anadai, yeye wakili akiitwa na bunge kutokana na haya maoni yake, hatakwenda. Cc Pascal Mayalla
Anadai bunge haliwezi kuwa mkamataji, muendesha mashtaka, na hakimu at the same time!.
Ana madini mengi sana.
Niuoneshe mkataba mwingine upi wa hovyo zaidi ya huo wa kipuuzi wa bandari uliouweka jukwaani mwenyewe!Nioneshe mkataba mmoja duniani udioweza kukosolewa, ambao hauwezi kuwa challenged mahakamani.
Hivi mnaelewa maana ya mikataba na nini kazi ya. Wanasheria?
Tuwache ujinga. Mkataba hata uandikwe vipi, unaweza kukosolewa na kupingwa, ndiyo maana mikataba yote inapofikia kuhukumiana kitu cha kwanza kinachotazamwa ni nia ya Mkataba,halafu yanafata mengine.
Tujisahihishe. Ni suala la kawaida tuJamaa amechambua vizuri sana aisee.
Ni mkataba unaodumu miaka na miaka kama ule wa TICTS uliosainiwa mwaka 2000 ukadumu mpaka 2017.Wewe unadhani huu mkataba ni sawa na vidonge vya majira??