Wakili Mwabukusi: Rais Samia atusikie, Mkataba wa Bandari haulindi uhai wa Nchi yetu

Wakili Mwabukusi: Rais Samia atusikie, Mkataba wa Bandari haulindi uhai wa Nchi yetu

PROFESA TIBAIJUKA ASTUKA NA KUFADHAISHWA NA UWEZO WA KUFIKIRI WA 'WANAWE' WAANDISHI VIJANA

Prof. Tibaijuka ashangaa maswali na hoja za waandishi wa habari katika sakata hili la mkataba wa DP World



Ni pale mwandishi alipouliza kuna tabu gani Kuwapa taarifa Dubai kila wakati wakati (Kifungu 4.2 cha mkataba) tunataka kufanya masuala ya sovereignty... profesa anashangaa waTanzania kutojipenda na kukubali kudharauliwa kutokana na maneno yalivyosukwa katika mambo makubwa na waandishi wanayachukulia kimasihara ... kuwa kuitwa kujieleza mbele ya Dubai ni suala la kishikaji / partnership wakati mkataba huu haupo hivyo Tanzania haina usemi katika mkataba huu mbovu ...

Huyu Tibaijuka si 'mali' ya Karamagi?
Anatetea biashara ya "mtu" wake?
 
Mama naona kama ana kiburi,mbona kanyamaza kimya kama hayamuhusu vile, kwanini Mkuu wa nchi unanyamaza kimya kwenye suala nyeti kama hili na wakati kwenye nyaraka saini yake ipo?hii inamaanisha nini jamani!
Mzee Mkapa aliposhutumiwa na sera yake ya ubinafsishaji mashirika ya Umma na migodi,alitokeza kufafanua na Mzee Kikwete vilevile kwenye sakata la Richmond na IPTL Escrow Account alitoa ufafanuzi.
Kulikoni Rais Samia?
Kimbukeni ata sakata la mgomo Kariakoo,napo alikaa kimya kama hayupo na alimuhusu!
Ukimya wake ndio unaonesha vile hatoshi kukalia kile kiti, amepwaya sana, sasa ndio atajua kuitwa Rais maana yake nini, sio kuuza sura tu na misafara ya vin'gora.
 
PALESTINA NA TABGANYIKA ZIKO on the same situation

Zimepoteza identity zake na wavamizi wanaziendesha kama wanavyotaka.
 
Ndio maana JPM aliwekwa pembeni, alikuwa mzalendo namba moja.
JPM ndio chanzo cha mkataba huu wa DPW, majadiliano aliyofanya na Kagame 2016 ndio yameileta hii kampuni na ndio yamewezesha ujenzi wa SGR kwa trilioni 16 fedha za Tanzania.

Hii ni biashara kubwa sana yenye lengo la kuondoa umaskini huu unaotutesa. Lakini wanaompinga mwekezaji ni hawa wanaojiita wazalendo, ambao nyuma ya hoja zao kuna pesa imepenyezwa kutoka kwa hao waliokuwa wakifaidika na bandari kuendeshwa kwa magumashi na upigaji mwingi, kina TICTS na GSM.
 
Ukimya wake ndio unaonesha vile hatoshi kukalia kile kiti, amepwaya sana, sasa ndio atajua kuitwa Rais maana yake nini, sio kuuza sura tu na misafara ya vin'gora.
SSH ni mtulivu mwenye kupima kabla hajaongea au hajafanya maamuzi. Anajua ukubwa wa adui anayepigana nae pale bandarini.

Anajua namna pesa chafu inavyotembezwa muda huu katika kupinga uwekezaji wa DPW, hivyo hawezi kufanya kazi kwa matakwa yangu na ya kwako.
 
Profesa Lipumba anakwenda mbali na kuonya kuwa mkataba huu wa nchi ya Tanzania na sehemu ya shirikisho la Emirati UAE unatutengenezea mgogoro na Abu Dhabi bila kusahau mgogoro na nchi ya UAE.

Wasiwasi wa profesa Haruna Lipumba kuhusu mgongano Tanzania walioupika kiaina baina ya Abu Dhabi na Dubai hivyo Tanzania kwenda kuambulia patupu, kaka mkubwa Abu Dhabi alikuwa anafukuzia mradi huu kwa ushirikiano na kampuni ya kubwa ya India Adani.

Hofu ya profesa ni kutokana na ukweli tamaduni za jamii ya Kiarabu za Mashariki ya Kati kuaminiana kwa mali - kauli halafu kugeukwa si ajabu Abu Dhabi katika vikao vya wana-ndugu wafahamianao kwa vilemba vya unduguakimkoromea na kumuonya bwana mdogo Dubai aachane na bandari ya Dar es Salaam na ukawa mwisho wa mradi huu ulio na utata wa kitamaduni, desturi na kisheria kuonekana uachwe
Some of the distinct features of the UAE's heritage are hospitality, tolerance, family cohesion and solidarity among members of the society along with honour and pride associated with being part of this heritage. However, the emirs of Abu Dhabi and Dubai have effective veto power in elections for the role of President. The last presidential election was held in 2009.

AD Ports Group And Adani Ports And SEZ Ltd Sign MoU For Joint Infrastructure Investments In Tanzania


Tanzania Port Authority saga continues

By Angelo Mathais

09/08/2022
Indian port conglomerate Adani Group (APSEZ) has concluded a memorandum of understanding (MoU) with AD Ports (Abu Dhabi Ports) to jointly pursue strategic investment opportunities in Tanzania.

The partners said they aimed to offer end-to-end logistics infrastructure and solutions covering rail, ports, maritime services, digital services and industrial zones in the East African country.

“A series of potential country-level investments to grow, improve, and promote an end-to-end maritime and logistics ecosystem will make Tanzania a hub for the African region,” they said.

The move follows an official approach from the Tanzanian Port Authority (TPA), which governs port-inland waterways systems, for investment support from the Indian side to develop maritime infrastructure projects, notably a $500m three-berth expansion at Dar es Salaam Port.


Other projects on the drawing board include: construction of a major port in Bagamoyo, with some $1bn funding; a $600m plan for the Mangapwani multipurpose port in Zanzibar; and a $300m investment in a new oil jetty in the Dar es Salaam harbour.

“With the East African Free Trade Zone and African Continental Free Trade Area coming into play, Tanzania is likely to emerge as a major transit point for general commodities as well as petroleum products,” said the Indian Ministry of Shipping. “In this backdrop, investment in the port sector or oil jetty in Tanzania would make good commercial sense.”

The potential in Tanzania mainly stems from its “gateway access” to cargo volumes moving in and out of the six land-locked countries of Malawi, Zambia, Democratic Republic of Congo, Burundi, Rwanda and Uganda.

“This MoU with Adani Ports is significant in its impact on both Tanzania’s ability to transform itself into an African trading hub, as well as our ability to further develop our global capabilities and connections that will bring goods to market faster and more efficiently,” said Capt Mohamed Juma Al Shamisi, MD and group CEO of AD Ports Group.

Karan Adani, CEO of APSEZ, added: “We are pleased to be partnering with AD Ports Group in the development of key quality infrastructure in Tanzania, especially in the ports and maritime sector, which will improve and bring about positive change in the communities, standing by our commitment to growth with goodness.”

APSEZ has been aggressively working to extend its port network reach beyond India in a bid to become the world’s largest port operator by 2030. And targeting the Tanzania market is expected to “yield significant contributions towards that goal”.

While preliminary plans indicate landside connectivity development interests to speed up hinterland cargo flowing through Dar es Salaam, those project specifics were not immediately available
 
Wasiwasi wa profesa Haruna Lipumba kuhusu mgongano Tanzania walioupika kiaina baina ya Abu Dhabi na Dubai hivyo Tanzania kwenda kuambulia patupu, kaka mkubwa Abu Dhabi alikuwa anafukuzia mradi huu kwa ushirikiano na kampuni ya kubwa ya India Adani.

1687472092911.png


Alhamisi 15/7/2021
Sheikh Shakhbout bin Nahyan bin Mubarak Al Nahyan, Waziri wa Nchi, amekutana na mheshimiwa Samia Suluhu, Rais wa Tanzania na kujadili njia za kuendeleza uhusiano wa jumla kati ya nchi hizo mbili marafiki.

Al Nahyan alitoa salamu za Rais Mtukufu Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Mtawala wa Dubai, Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Ufalme wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa UAE, kwa Rais Suluhu Hassan na matakwa yao ya maendeleo na ustawi zaidi kwa wananchi wa Tanzania.

Rais wa Tanzania alipokea salamu hizo na kuwatakia wananchi wa UAE kuendelea na maendeleo na ustawi.

Rais Macron akimkaribisha Rais wa UAE Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan jijini Paris
1687501796774.png


20 June 2023
Abu Dhabi

Rais wa UAE Sheikh Mohamed Zayed amkaribisha Rais Sassou-Nguesso wa Congo Brazzaville


Rais Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan alikutana na Denis Sassou-Nguesso, Rais wa Jamhuri ya Kongo, ambaye yuko katika ziara ya kikazi katika UAE.

Wakati wa mkutano wa Qasr Al Bahr huko Abu Dhabi, Sheikh Zayed alimkaribisha Rais Sassou-Nguesso, na viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya UAE na Jamhuri ya Kongo. Pia walijadili fursa za kuendeleza uhusiano baina ya nchi hizo mbili, hasa katika nyanja zote za kiuchumi, biashara na maendeleo muhimu, ili kuimarisha fursa za maendeleo endelevu kwa nchi zote mbili.
 
May 14, 2022
Abu Dhabi
KIAPO CHA UTII KWA RAIS WA UAE AMBAYE PIA NI MTAWALA WA ABU DHABI
1687473142086.png

Picha : Rais wa UAE mtukufu mheshimiwa maulana Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan mtawala wa Abu Dhabi

Viongozi wa vyombo vya serikali ya Abu Dhabi wamempongeza Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan kwa kuchaguliwa kwa kauli moja na wajumbe wa Baraza Kuu la Shirikisho kuwa Rais wa UAE, akimrithi hayati Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan.

Viongozi walitangaza utii na uaminifu wao kwa Sheikh Mohamed bin Zayed kwa kuahidi kuendelea kulitumikia taifa kwa kujitolea na ikhlasi chini ya uongozi wake, wakimtangaza kuwa mrithi anayestahiki wa mtangulizi wake mkuu, ambaye hekima yake itachagiza enzi ijayo ya hatua ya mambo makubwa kwa UAE....

Mohamed Ali Al Shorafa Al Hammadi, Mwenyekiti, Idara ya Maendeleo ya Uchumi ya Abu Dhabi alisema: “UAE imebarikiwa kuwa na Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan kuchaguliwa kuwa rais wake. Mwanamume ambaye amejitolea kuongoza maono ya baadaye ya maendeleo ya UAE, na kuimarisha zaidi nafasi yake ya kimataifa kupitia juhudi za kutetea maadili ya usalama na amani."

Watawala wa UAE Falme za Kiarabu, masheikh na mawaziri mbalimbali wametoa pongezi na uaminifu wao kwa rais mpya wa UAE , Sheikh Mohamed bin Zayed.

Baraza Kuu la Shirikisho la UAE lilimchagua kwa kauli moja Sheikh Mohamed bin Zayed kuchukua jukumu hilo siku ya Jumamosi.

Barua ya kuhuzunisha, iliyowekwa mtandaoni na Sheikh Mohammed bin Rashid , Makamu wa Rais na Mtawala wa Dubai, iliangalia nyuma utumishi wa umma wa Sheikh Mohamed bin Zayed na mbele ya matamanio mapya.

"Kwa miaka mingi, watu wa UAE wamempenda," Sheikh Mohammed aliandika kuhusu rais mpya wa UAE .

Kwa uongozi wako tunaanza safari ya kihistoria, iliyojaa mafanikio na matumaini



1687474725348.png

Watawala toka Emirati 7 zote zinazounda UAE wajitokeza mjini Abu Dhabi mji mkuu wa UAE kwenda kuonesha utiifu kwa Rais wa UAE


Kila goti la heshima laelekezwa kwa emir mpya wa Abu Dhabi Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan ambaye pia ndiyo rais wa UAE Umoja wa Falme za Kiarabu. Ni utamaduni, desturi na mila kula yamini kwa ma emir wa majimbo ya shirikisho la Falme za Kiarabu kwenda kutangaza kumheshimu rais wa UAE kwa akili na nguvu zao zote.



The National
May 14, 2022
The rulers of the emirates, various sheikhs and ministers have offered their congratulations and loyalty to the new president, Sheikh Mohamed bin Zayed.

“Today, his people pledge allegiance to him, promise to listen and obey, and follow him while he leads them in a new historical journey in UAE. The future generations rejoice in the third president of the UAE, and the world is pleased with a country that represents a future international model characterised by goodness and brotherhood to all of humanity,” Sheikh Mohammed said.

“We congratulate His Highness again and the people of the UAE.

“We pray God to protect him.

Read More : UAE leaders pledge allegiance to new President Sheikh Mohamed bin Zayed
 

WAKILI MWABUKUSI: Rais Samia atusikie, Mkataba wa Bandari haulindi uhai wa Nchi yetu




Katika mahojiano leo na wakili Mwabukusi anaangazia mambo zaidi kamati ya bunge, uwakilishi wa muswada wa mkataba bungeni na jinsi muda finyu waliopewa wabunge kuujadili ...
.

Wabunge Halima Mdee, Aida Kenani pamoja na Luhaga Mpina ambaye hakupata nafasi bungeni kuwakilisha hoja hivyo kuwakilisha maoni nje ya bunge kwa maandishi watambuliwe kwa kupewa maua yao hayo bila kumsahau dada yetu mpendwa wa taifa Mange Kimambi amesema wakili msomi Boniface Mwabukusi

Aliyevujisha mkataba ni mzalendo halisi na hii inatia moyo kuwa bado kuna Wazalendo wachache ndani ya serikali... na huyu atambuliwe wajibu wake mkubwa kulinda maslahi ya taifa

Serikali inawajibika kwetu umma yaani wananchi hivyo viongozi wote serikalini watambue mamlaka zote tulizowapa ni zili zilizotamkwa katika katiba kama hawawezi waache nyadhifa zao waende nyumbani ...

Advocacy tunayofanya ni kazi ya kuelimisha wananchi na ndiyo wajibu wetu kwani waziri Mbawara katika hadhira tofauti tofauti anasema mkataba huu ni makubaliano na akifika mbele ya viongozi wa dini n.k wanasema mkataba ...


Viongozi waache propaganda kwa kwenda sehemu mbalimbali Tanzania kupotosha wananchi kuwa marekebisho yatafanywa... hata wakienda mpaka kilele cha mlima Kilimanjaro haitasaidia kuzimisha kelele za wananchi ...

Linalotakiwa ni bunge hili hili lirudi haraka ili kwa kikao cha kingine liupitie tena maana ni hitajito la kikatiba wakati kunapotokea hali kama hii tunayoiona badala ya kujaribu kuutetea mkataba huu mbovu ...

Bunge halina uwezo wa kuita watu kuwahoji hata pale walipowatisha kwa kuwaita kina Paschal Mayalla, Dr. Reginald Mengi na wengine ni batili. Kwa bunge haliwezi kuwa prosecutor na mahakama

Kumtishia balozi Dr. Wilbrod Peter Slaa ambaye ni Whistle blower bona-fide kuwa aitwe bungeni ahojiwe kuhusu press conference zake za kuhusu sakata la DP World, hili ni kinyume cha katiba na batili maana bunge halina mamlaka hayo....

Hata mimi Boniface Mwabukusi nikiitwa Dodoma siwezi kutishwa na sitakwenda maana ni wito batili na haramu wala kukidhi sheria na katiba yetu kwa kuwa bunge halina mamlaka hayo

Mikataba ya kunyonya Mali ya asili yetu haikubaliki ni mikataba pekee ambayo ina manufaa kwa taifa na muwekezaji ndiyo tunayoiafiki siyo mkataba mbovu kama huu ...

Tunawashukuru wananchi kwa kupaza sauti katika suala hili ..... maana sasa Bunge halitaweza tena kututia vitanzi kama hivi vya DP World, Loliondo, Madini n.k bila wananchi kuhusishwa kimamilifu na siyo kuburuzwa ....

Kuna masharti yasiyo general policy ndani ya mkataba .... reciprocacy hakuna, huu mkataba una mlinda mwekezaji badala ya kumpa haki ya kudai fidia pale anapodhulumiwa...

High level consultation kwa kutumia katiba yetu Ibara ya 27.1 ya raia kuwa na haki ya kulinda Mali inafanyika na si muda mrefu waTanzania watapewa mrejesho na watafahamishwa

Ibara ya 28 ya katiba hairuhusu mtu yeyote kumilikishwa eneo lolote bali inaruhusiwa kutumika kwa shughuli hivyo mwekezaji hatakiwi kumilikishwa bali kuendesha shughuli za kibiashara ...

Bungeni kulikuwa na tukio na siyo mjadala maana hakuna mwanasheria mkuu hakuoneshwa siku hiyo na mwanasheria mkuu ana kiti chake maalum bungeni lakini hakuwepo na badala yake spika wa bunge kuliteka bunge kinyume na uendeshaji wa bunge huku akiwadhalilisha, kuwa harass wabunge Halima Mdee, Aida Kenani na kulibadilisha bunge kuwa kama darasa la chekechea / kindergarten la a,e,i,o,u huku dhihaka za kutunzana noti, miluzi, kugonga meza kiasi cha bunge kuwa eneo mithili ya ngoma ya mchiriku wakati jambo muhimu la eneo la nchi linamilikishwa kwa taifa lingine geni milele

Ya fuatayo yarekebishwe katika mkataba huu wa DP World katika yafuatayo : Sheria za nchi zizingatiwe masuala ya umilikaji ardhi, umilikaji wa bandari, uvunjwaji wa mikataba, tusikatazwe kutwaa eneo pale usalama wa taifa unapotishiwa tofauti na mkataba huu unavyotukataza kitu ambacho ni kinyume na katiba, spika aache kuligeuza bunge kuwa kikaragosi cha serikali, maandamano yaratibiwe maana katiba inaruhusu

Ushauri kwa Mh. Samia Hassan, ni kuwa mimi nina mashaka rais amepotoshwa maana hata wataalamu kama mwanasheria mkuu hakuonekana ndani ya televisheni siku ya tarehe 10 June 2023 jumamosi mjini Dodoma. Pia namshauri mchakato wa haraka ufanyike Serikali iurudishe mkataba huu tena bungeni na utaratibu wote utumike kikamilifu na uwazi mkubwa kusuka upya mkataba huu tata.

Freeman A. Mbowe ameeleweka na watu wenye uwezo wa kufikiri ila kuna watu wanataka kupotosha ujumbe mzuri aliowakilisha


Ni nchi mbili tu yaani Palestina kule mashariki ya kati na Tanganyika hapa Afrika Mashariki nchi zao zimepotezwa .....

Rais amwelekeze waziri aliyemkasimisha madaraka (Delegata potestas non potest delegari) kujiuzulu maana alimuamini waziri hakutumia imani hiyo vizuri lakini sasa amemuingiza katika matatizi makubwa na pia mkataba huu urejeshwe bungeni tena maana paka akifungiwa chumbani katika kona paka huyu huweza kujigeuza Simba... pia Spika Tulia Ackson ajiuzuli nafasi yake mara moja ya uspika kwa kushindwa kulipa bunge na wabunge nafasi ya kuishauri serikali kwa uwazi hilo linawezekana maana Job Ndugai alijiuzulu kufuatia utata ... na kadhia hii ya bandari ni moto kuliko ya Job Ndugai spika aliyepita ..

Wazee wa taifa wajitokeze haraka kumshauri rais kwa heshima kuwa kuwa wajisahihishe kuurejesha mkataba huu tena bungeni ....
Wazee wa taifa wajitokeze haraka kumshauri rais kwa heshima kuwa kuwa wajisahihishe kuurejesha mkataba huu tena bungeni ....[emoji419][emoji375]
Lakini ujue kuna mingine zaidi ya 30 imeshasainiwa kwa kasi ya 5G

Sent using Jamii Forums mobile app
 
22 June 2023
Abu Dhabi

Rais wa UAE Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan akipokea ujumbe toka Iran



President Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan receives Iranian Foreign Minister Mr Hossein Amirabdollahian, who is on a working visit to the Emirates, conveyed the greetings of Iranian President Ebrahim Raisi to Sheikh Mohamed and called for the continued progress and prosperity of the UAE. Sheikh Mohamed relayed similar sentiments
 
Kazi ya wabunge ni ipi ikiwa kila mtu anatakiwa afike Dodoma kutoa maoni yake?.

Nini faida ya kampeni za uchaguzi kutumia mabilioni ya pesa mara moja kila baada ya miaka mitano ikiwa kwenye suala moja tu tuanzishe urasimu usio na mantiki yoyote?.

Reforms zina gharama yake tena kubwa na zinaumiza baadhi ya taasisi, sisi sio wa kwanza kufanya mabadiliko ya kiuchumi, hivyo tuwe wapole tu wakati sindano zikiwa zinaingia, baada ya muda tutakuwa tumepona.
Wewe unadhani huu mkataba ni sawa na vidonge vya majira??
 
Huyu Tibaijuka si 'mali' ya Karamagi?
Anatetea biashara ya "mtu" wake?
TICS ilishaondoka na wala haiwezi kurudi, tunataka mkataba kama huo ukivurunda tunakuondoa tunaweka mwingine, mkataba kijini jini hapana, ukishapewa jini umepewa likufanye vizuri au vibaya hauwezi kulifukuza.
 
Upuuzi huu. Msikae mnadanyana humu.

Aje mfanya biashara wa kimataifa, kutoka popote duniani apinge huu mkataba wa msendeleo, siyo Wanasheria uchwara na watu wenye njaa. Hakuna mkataba wa kibinaadam duniani usioweza kuwa challenged.
Nimemuukuza mpaka AI 👇🏾
Swali:
Is there an inter government agreement which cannot be challenged?
Jibu:
I'm not aware of any inter-governmental agreement that cannot be challenged. In general, inter-governmental agreements can be challenged if one of the parties involved believes that the agreement has been violated or if there is a dispute over the interpretation of the agreement ¹³.

In some cases, inter-governmental agreements may include dispute resolution mechanisms that allow the parties involved to resolve disputes without resorting to legal action ³. These mechanisms may include good offices, conciliation, mediation, and arbitration ³.

I hope this helps answer your question. If you have any further questions or need more information, please let me know.

Source: Conversation with AI Bing 23/06/2023
(1) Understanding Intergovernmental Relations: Key Features and Trends .... https://onlinelibrary.wiley.com/doi/10.1111/1467-8500.12025.
(2) WTO | Understanding the Sanitary and Phytosanitary Measures Agreement. WTO | Understanding the Sanitary and Phytosanitary Measures Agreement.
(3) Full article: A “party” at the border: An anthropological take on the .... https://www.tandfonline.com/doi/full/10.1080/23311983.2020.1727159.
Asiyejuwa Kingereza na adiyrjuwa namna yankutafsiri kutumia mtandqo aseme tumsaidie.
 
Jambo la kumshukuru sana Mungu, kila mtanganyika mwenye kuitakia mema Tanganyika yake tunaongea lugha moja.

Ajabu sana, watanganyika waliotakiwa kutoa maoni yao kuhusu hili suala walitakiwa kufika Dodoma tarehe 5, ili kufikia tarehe 6 saa 7 mchana wawe tayari kwa kutoa maoni.

Wakili anashangaa, inawezekana vipi kwa mtanganyika anayeishi Kigoma, Sumbawanga, Kagera, Ukerewe, Arusha na kwingineko wote wafike Dsm kutoa maoni yao siku inayofuata?

Watu wameitwa kuja kutoa maoni, ajabu mkataba wenyewe haujawekwa wazi, mtu anatakiwa kutoa maoni akiwa anajua nini anachozungumza, baada ya kupata muda wa kutosha kuuchambua mkataba, sasa unapowaficha mkataba, unataka wakazungumze kitu gani?!

Wakili anazidi kushangaa, kumbe bunge lilishaandaa Azimio la kupitisha mkataba, kabla hata bunge halijapitisha ule mkataba! huu ni ushetani kabisa.

Wakili anaendelea kusema, bunge badala ya kumshukuru Dr. Slaa kwa kuwa whistleblower, wao wanataka kumuita ili wamhoji, anadai bunge ni kinyago chetu tulichokichonga wenyewe, hakiwezi kututisha, zaidi anadai, yeye wakili akiitwa na bunge kutokana na haya maoni yake, hatakwenda. Cc Pascal Mayalla

Anadai bunge haliwezi kuwa mkamataji, muendesha mashtaka, na hakimu at the same time!.

Ana madini mengi sana.
Nioneshe mkataba mmoja duniani udioweza kukosolewa, ambao hauwezi kuwa challenged mahakamani.

Hivi mnaelewa maana ya mikataba na nini kazi ya. Wanasheria?

Tuwache ujinga. Mkataba hata uandikwe vipi, unaweza kukosolewa na kupingwa, ndiyo maana mikataba yote inapofikia kuhukumiana kitu cha kwanza kinachotazamwa ni nia ya Mkataba,halafu yanafata mengine.
 
Nioneshe mkataba mmoja duniani udioweza kukosolewa, ambao hauwezi kuwa challenged mahakamani.

Hivi mnaelewa maana ya mikataba na nini kazi ya. Wanasheria?

Tuwache ujinga. Mkataba hata uandikwe vipi, unaweza kukosolewa na kupingwa, ndiyo maana mikataba yote inapofikia kuhukumiana kitu cha kwanza kinachotazamwa ni nia ya Mkataba,halafu yanafata mengine.
Niuoneshe mkataba mwingine upi wa hovyo zaidi ya huo wa kipuuzi wa bandari uliouweka jukwaani mwenyewe!
 
Back
Top Bottom