Wakili Mwakubusi: Vyama vya Upinzani kazi yao ni kufukuzia tu ubunge na ruzuku, haviwezi kulikomboa Taifa

Wakili Mwakubusi: Vyama vya Upinzani kazi yao ni kufukuzia tu ubunge na ruzuku, haviwezi kulikomboa Taifa

"Vyama vyetu vya siasa nadhani aidha vimechoka sana vyote vinahitaji kupumzika au viongozi wake wamechoka sana wanahitaji kupumzika, na ndio maana wanapoteza ile hamu ya kulikomboa na kulisimamia taifa, wanakuwa watu wa kufukuzana na tuvyeo, ubunge, ruzuku, kugawana, kukaa kaa mezani. Kila mmoja yuko bize, wanachotaka ni kugawana tu sio kupambana kwa ajili ya wananchi. Lakini kikubwa ninachojaribu kusema kwamba inawezekana katiba kupatikana bila wanasiasa.” – Wakili Boniphace Mwabukusi

Chanzo: Swahili Times
Siyo Mwakubusi bali ni Mwabukusi
 
Kazi ya Wakili imekwisha kamilika.

Tunashukuru Wakili Msomi kwa kupeleka Mjadala ule wa Bandari kwa namna ile hadi kufikia hitimisho lile

najivunia kuwa CCM ambayo tangu kuanza kwake imekuwa mbele ya muda kwny mijadala yote inayotishia umoja na mshikamano wa Taifa

Chadema pia inathamini sana amani kwa kuwa inajua bila ya amani hakuna ruzuku

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app

Umejaa dharau na kebehi. Shauri zako.
 
Haya aliyoyasema ni sahihi kabisa, hili tunaliona wananchi lakini je, tufanyaje? Mwambukusi hana chama lakini kiukweli namkubali sana. Hivyo sauti ya huyu mwamba itaeleweka pasipokuwa na chama!?
Mwabukusi, si Mwambukusi
 
Yupo sahihi 100%.Umesikia upinzani ukiongelea mgao wa umeme unaondelea?Umesikia upinzani ukipinga vikali mkataba wa bandari?Hii serikali ni ya ovyo kuwahi kutokea lakini upinzani upo kama haupo.

Wewe ndio huna maana. Kwa hivyo mama yako Samiah ametoa miezi SITA umeme usiwe mgao, upinzani ndio walalamike ili iweje?. Kwenye shida mnaoponda upinzani, ila mwenye mamlaka ya kuleta umeme mnalamba miguu na kumuogopa.
 
Haya aliyoyasema ni sahihi kabisa, hili tunaliona wananchi lakini je, tufanyaje? Mwambukusi hana chama lakini kiukweli namkubali sana. Hivyo sauti ya huyu mwamba itaeleweka pasipokuwa na chama!?
Upinzani nani kakuambia ni chama? Kule Sudani Maandamano ya kumung'oa Alibashiri hayakuanzishwa na Vyama vya upinzani.

Turudu kwenye Maada,Mwambukusi akiitisha Maandamano utatoka?au wewe ni keybord man?
 
Tapeli mwenyewe. Unahangaika na CHADEMA kuliko wezi wa ripoti ya CAG.
Mkuu Chadema ni Genge la matapeli. Na uelewe mimi sio CCM.Saizi Chadema ni tawi kificho la CCM ndio maana huwezi kuta wako na wananchi kupambana juu ya udharimu wa CCM.Mbowe na genge lake wamefeli, bora kije chama kingine cha upinzani. Haiwezekani Nchi yenye upinzani imara tukawa tunalala giza huku utawala unakuja na hoja za kipuuz.
 
"Vyama vyetu vya siasa nadhani aidha vimechoka sana vyote vinahitaji kupumzika au viongozi wake wamechoka sana wanahitaji kupumzika, na ndio maana wanapoteza ile hamu ya kulikomboa na kulisimamia taifa, wanakuwa watu wa kufukuzana na tuvyeo, ubunge, ruzuku, kugawana, kukaa kaa mezani. Kila mmoja yuko bize, wanachotaka ni kugawana tu sio kupambana kwa ajili ya wananchi. Lakini kikubwa ninachojaribu kusema kwamba inawezekana katiba kupatikana bila wanasiasa.” – Wakili Boniphace Mwabukusi

Chanzo: Swahili Times
Ukweli mchungu
 
Yupo sahihi CCM imechokwa na wananchi lakini wamekatishwa tamaana vyama mbadala. Kwa matukio ya Sasa kuanzia mfumko wa Bei, tatizo la umeme na mengineyo ni chama kipi kinayazungumzia?
Upinzani ni Ideology, sio Chama,Kama vyama vimechoka na Ideologt vipi?Unataka Mbowe na Familia yake Waandamane nyie mkiwa Majumbani?
 
Hata hicho Chama tawala Kiko madarakani kwa sababu za kihistoria tu, na katiba inayokibeba sio nje ya hapo. Na Wala hakipo hapo kwa ubora.
CCM iko madarakani kutokana na udhaifu wa upinzani uliopo. Na CCM itatawala milele kama aina hii ya upinzani inatendelea kuexist. Now CCM ina mtaji wa wananchi wajinga na upinzani uchwara.
 
Haya aliyoyasema ni sahihi kabisa, hili tunaliona wananchi lakini je, tufanyaje? Mwambukusi hana chama lakini kiukweli namkubali sana. Hivyo sauti ya huyu mwamba itaeleweka pasipokuwa na chama!?
Ni NCCR Mkuu - Hana chama kivipi?
 
Yupo sahihi 100%.Umesikia upinzani ukiongelea mgao wa umeme unaondelea?Umesikia upinzani ukipinga vikali mkataba wa bandari?Hii serikali ni ya ovyo kuwahi kutokea lakini upinzani upo kama haupo.
Upinzani ni nani?tuanzie hapo,Kama hawaongelei kwa nini wewe usiongelee Mkuu? Unataka Mbowe na familia yake watoke wabebe mabango waandamane kupinga mgao wa umeme? Nyie mkiwa kwenye keybord?
 
Back
Top Bottom