Wakili Mwakubusi: Vyama vya Upinzani kazi yao ni kufukuzia tu ubunge na ruzuku, haviwezi kulikomboa Taifa

Nilishangaa sana kwanini ule moto wa bandari Chadema walikua nyuma nyuma sana?Watu wanapewa kesi ya UHAINI wao wapo wapo tu,mtu aseme Chadema ni chama cha SIASA?No,hili ni genge la wahuni.
 
Yupo sahihi 100%.Umesikia upinzani ukiongelea mgao wa umeme unaondelea?Umesikia upinzani ukipinga vikali mkataba wa bandari?Hii serikali ni ya ovyo kuwahi kutokea lakini upinzani upo kama haupo.
Wewe unataka waongee kwa namna gani ili uelewe?.Hakuna jambo ambalo halijaongelewa.labda kama masikio yenu yanachagua maneno yakusikia.au mnataka chadema wafanye siasa za namna nyingine ili mje tena na kauli kua wanaharibu amani.
 
Mbona mnasema Magufuli alikua anaua upinzani wakati tuliona akiwaalika akina Cheyo,Lipumba na wengine ikulu?Kwenye Positive mnaiweka Chadema kama ndio symbol ya upinzani ila kwenye negative mnaitoa mnataka wengine wawe included
Ungewauliza hao uliowaona wakisema sio mimi,

Je na wewe unakubali kwamba hakuna vyama vingine vya upinzani tofauti na Chadema au au unasema vyama vya upinzani vipo vingi ambavyo unaweza ukaviunga mkono kuitoa CCM?
 
Raia wana imani na serikali ya Samia ndio maana hawawezi kupelekwa barabarani kama manyumbu, kama unataka kuthibitisha hilo kamuite Polepole au Musiba waje waitishe maandamano uone watapata watu wangapi
 
Swala la kuikomboa nchi ni jukumu la kila mwananchi.sio swala la kuviachia vyama vya siasa na wanasiasa peke yake.Kwa upande huo chadema wamejitahidi sana kwasababu agenda ya kwanza kubwa ni kuelimisha jamii na chadema wametoa sana hiyo elimu kuanzia elimu ya katiba bora na haki msingi zakiraia.Chadema wamechagua siasa za kistarabu ambazo mwakubusi anaona hazisaidii kwasababu yeye anataka siasa za kufoka foka na kugomba kwa maneno makali yamsisitizo akifikiri hiyo ndio siasa sahihi,bila kujua kwamba unaweza ukafoka na ukatoa hadi wito wa maandamano bado ikawa kazi bure kama wananchi watakua hawajaelimika vya kutosha.Akumbushwe kua hili jukumu linatakiwa kufanywa kwa akili nyingi kulingana na aina ya siasa zinazoendeshwa na chama kilichoko madarakani.Ukifanya kwa mihemko na hisia atajikuta kaaribu badala ya kujenga.Aliye karibu naye amwambie mapambazuko yako karibu na kamba ukatikia pabovu.
 
Ndio mtajua kuwa hamjui,CDM ni lini watajifunza?wamepelekwa resi na Wakili Mwambukisi bila hata ya kushtuka ,haya sasa kashawapondo vibaya
Hajaitaja chadema lakini.😅😅
 
Huu ndio ukweli anaepinga ni mchawi.
Wananchi wanataka mabadiliko ila vyama vyote vimejaa matapeli ikiwamo CHADEMA.
Wananchi tumetelekezwa!
Ogopa wanasiasa na siasa zao
Hao Wananchi hawawezi kuunda chama cha maana?
 
Wewe umezuiwa kuanzisha huo upinzani madhubuti? Umekaa unakula keki na kuvimbewa halafu unataka wenzako wakupiganie? Hapana aisee.
 
Nilishangaa sana kwanini ule moto wa bandari Chadema walikua nyuma nyuma sana?Watu wanapewa kesi ya UHAINI wao wapo wapo tu,mtu aseme Chadema ni chama cha SIASA?No,hili ni genge la wahuni.
Wewe kama mwananchi ulifanya nini?.Au umekalisha makalio kwako unatupa tu visingizio kwa wengine wakufanyie.
 
Unaangalia mambo kwa namna mbaya unayoitaka wewe.kama ukuona agenda za maana zilizozungumzwa kwenye ile mikutano wewe ndiye utakayekua na shida sio chadema.ndo maana Umeangaika na porojo za watu badala ya agenda ndo maana ukaondoka na porojo ukaacha mambo ya msingi.
 
Kwenye statement yake amedai vyama vya siasa na si vyama vya upinzani.
Umeweka kichwa cha habari ku fit narrative yako

On the otherside ni kweli vyama vya siasa including chama tawala na upinzani.
Kuikomboa nchi si anaamanisha kuitoa CCM madarakani!! ? Sasa hapo CCM haiwezi kuingia tena sababu CCM tunaamini nchi hii iliisha kombolewa na ni nchi huru, anaananisha vyama vya upinzani
 
Aliyeongea haya hajui chochote. Anasahau kuwa katika taasisi huwa kuna malengo makuu mawili ambayo lazima yaende sambamba. Moja, lengo la kuendeleza taasisi husika na pili, lengo la kutimiza mahitaji ya wafanyakazi wa taasisi husika. Anataka hao wanasiasa waendelee kusukuma taasisi mbele huku wao wakiishije(chakula, mavazi, malazi, matibabu na mahitaji mengine ya familia)? Mimi nadhani kwa kupata nyenzo ya ubunge ndiko kunawawezesha kutimiza malengo yote mawili vizuri.
 
Watanzania sio manyumbu wa kurndeshwa kwa mihemko ya siasa za kikabila kama Kenya , Watanzania wana imani na serikali ya CCM ndio maana hata aje mtu gani hawezi kuwashawishi watanzania waandamane wavuruge amani, hata akifufuka mwendazake awaambie waandamane hatapata watu labda huko kwao Chato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…