Naongezea.
Wakati suala la mkataba wa uwekezaji wa Bandari umezuka, na nipo tayari kusahihishwa, Mbowe et al walikaa kimya kwa mda mrefu kweli, nadhani, walitegemea vuguvugu lile liishe na mambo yaendelee kama kawa. Haikuwa hivyo!
Sasa baada ya kuona yale majaribio yao kujitambulisha tena kwa Wananchi(operation 255) yamekufa, manake yale maigizo-Kurukaruka na helikopta, mara kupigiwa saluti na Askari, mara mtoto wa miaka 9 kumlilia Mbowe, mara kutembelea kaburi la mwanasiasa mkongwe, mara yupo Ikulu kupiga picha n.k n.k kubuma Ikabidi waanze upya.
...na kuanza huko walibidi wateke headlines, ndio akatokea mbowe na kauli yake ile ya "Uzanzibari" after the fact
Kilichfanyika ni kufunika kabisa mijadala ambayo kwa wiki chache kulionekana uwepo wa Umoja, yaani ulikuwa hauwezi kuotofautisha uzalendo au itikadi za kichama, uwe CCM au chama kingine chochote au usiwe na chama, watu wengi walionekana wakitetea Rasilimali yao, Bandari.
...255, imebuma, Lissu kakimbilia kutomaswa(massage therapy) ubeligiji huku kukiwa na tetesi za mgawanyiko ndani ya CHADEMA, CHADEMA walikuwa wamekosa headlines chanya!
Opportunity ikatokea, wakabidi waingie kwenye reli pamoja na wanaharakati, lakini hawakuingia kuendeleza mjadala, hapana, waliingia kuufunika. Wakaanza kukimbizana na Kaburi la Hayat, mara Katiba, mara Uchaguzi na vimbwanga vingi tu kuwachanganya Wananchi kama walivyopaswa na masharti ya Maridhiano yao ya awali- Toka jela, Kula Ruzuku, Sifia SSH, kandamiza legacy and so forth badala ya kukalia papo tu, yaani, KUSITISHA mkataba, Urudishwe Bungeni uwe kalas.
Wameniudhi, wametuudhi, na ndio katika mlolongo huo wa kutuchanganya ndipo wananchi sasa wanaanza kuona Mbadala haueleweki, hususani ukija upande wa Upinzani, pamoja na kwamba nimeishikia bango CCM ijivue tu madaraka, Wanachama warudishe kadi, lakini sidhani kama CHADEMA wapo na Dhamira ya kutuvusha tulipo. Na kama ilivyosemwa huko juu, wapo kutaka kugawana madaraka 2025.
.... wapo lakini hawapo.