Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
Jamani kwani hapa anayeongelea haki sawa ni nani?? Kwahiyo kwa sababu wanaume hampati madhara kama wanawake basi ndiyo tusiwaambie ukweli?? Lazima tuseme ukweli kwamba wanaume nanyi mnachangia katika uwepo wa single mothers
Na ni lazima ukweli usemwe kwa jinsia zote mbili na siyo kuangalia eti jinsia moja ndiyo inapata madhara kuliko nyingine yaani ni sawa na mtu badala ya kukemea wezi eti anawaambia wanaoibiwa ndiyo wawe makini utafikiri wezi hawana makosa kabisa ila wanaoibiwa tu ndiyo wana makosa!!
Tendo la ndoa limekatazwa kwa wote. Wote jehanam inawahusu, lakini wakijirudi mwanamke anabaki na madhara permanent.
Kwa mfano wako wa wezi, unapoonywa kwamba funga milango na madirisha unaposafiri, ama unapolala usiku, au usiwazoeshe wahuni kuingia ndani mwako wasije wakachora ramani ya kukuibia utanung'unika?? Utalalamika kwamba kwa nini msiwakemee wezi sisi tuishi kwa uhuru, tukiacha milango wazi, tukitembea na mamilioni mtaani? Ukifanya hayo ukaibiwa watu watakucheka wewe, sio wezi. Wataona kuwa uliyataka mwenyewe.