Hilo swali tafadhali lisijibiwe ki jazba.
Ukosefu wa maadili unatupeleka pabaya sana. U singo mama na u singo baba unakuja kwa njia tofauti lakini kuu zaidi ni hili la singo mama.
Nyumba zinazoitwa " vituo vya yatima", binafsi naziita vituo vya watoto waliokosa bahati. Kwa sababu vituo hivyo vimejaa watoto wenye wazazi wao, lakini kwa kuwa watu wameona ni biashara inayolipa, wanachukuwa vibali vya vituo hivyo na kuwajaza humo kujitengenezea kipato haramu.
Wengine wa hao watoto wa singo maza na singo faza, ni watoto tunaowaona wakilelewa na walezi wengine kabisa, ambao siyo wazazi wao. Kama vile bibi, shangazi, dada mama mkuu. Je kuna siri zipi nyuma ya pazia?
Nini kinachosababisha u singo maza? Majibu yangu binafsi kwa uchache.
1) Wengi, pengine asilimia kubwa zaidi, za watoto wasio na bahati, hupatikana mimba kwa kujamiiana watu walio wa karibu kabisa, baba, mjomba, kaka, baba mdogo, baba mkubwa mpaka mababu.
Mashangazi, dada, mama mdogo, mama mkubwa nao wamo.
Watoto wanaopatikana ni kipi kitawazuwia wasiwe wa singo maza?
Wanasema "nyumba uloizowea kuihama ina kazi". Mtindo huo hujirudia sana tu.
Kuna kesi mbili tatu nazifahamu binafsi za namna hiyo, dunia haina siri.
Nyote, mnaoambiwa ni watoto wa singo maza msiowajuwa baba zenu, au kila mwanamme anaeingia kwenu unaambiwa "mwamkie babako" mjuwe baba zenu mnao na ni watu wenu wa karibu kabisa.
Tukiona Watanzania wengi ni mapoyoyo, hiyo nayo ni sababu ya kuwa na taifa lenye watoto wenye mapungufu.
Tatizo siyo wanaoitwa au jiita ma "singo mama" tu, kuna watoto wengi sana wanaoambiwa "mamako alikufa" au "babako alikufa", kumbe ni uwongo mtupu. Huyo baba au mama aliyekufa isibaki hata picha? Au ndugu zake?
Ma singo baba, sababu zao ni nini?
Tusilee uozo wa maadili.