Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Tusifieni na wanaume...kuna nchi nyingne wanawake wanataman hiz nafas za kupigwa mbupu mpk kupata mtoto sababu wanaume hakuna...
Hii ni neema
 
Hilo swali tafadhali lisijibiwe ki jazba.

Ukosefu wa maadili unatupeleka pabaya sana. U singo mama na u singo baba unakuja kwa njia tofauti lakini kuu zaidi ni hili la singo mama.

Nyumba zinazoitwa " vituo vya yatima", binafsi naziita vituo vya watoto waliokosa bahati. Kwa sababu vituo hivyo vimejaa watoto wenye wazazi wao, lakini kwa kuwa watu wameona ni biashara inayolipa, wanachukuwa vibali vya vituo hivyo na kuwajaza humo kujitengenezea kipato haramu.

Wengine wa hao watoto wa singo maza na singo faza, ni watoto tunaowaona wakilelewa na walezi wengine kabisa, ambao siyo wazazi wao. Kama vile bibi, shangazi, dada mama mkuu. Je kuna siri zipi nyuma ya pazia?

Nini kinachosababisha u singo maza? Majibu yangu binafsi kwa uchache.

1) Wengi, pengine asilimia kubwa zaidi, za watoto wasio na bahati, hupatikana mimba kwa kujamiiana watu walio wa karibu kabisa, baba, mjomba, kaka, baba mdogo, baba mkubwa mpaka mababu.

Mashangazi, dada, mama mdogo, mama mkubwa nao wamo.

Watoto wanaopatikana ni kipi kitawazuwia wasiwe wa singo maza?

Wanasema "nyumba uloizowea kuihama ina kazi". Mtindo huo hujirudia sana tu.

Kuna kesi mbili tatu nazifahamu binafsi za namna hiyo, dunia haina siri.

Nyote, mnaoambiwa ni watoto wa singo maza msiowajuwa baba zenu, au kila mwanamme anaeingia kwenu unaambiwa "mwamkie babako" mjuwe baba zenu mnao na ni watu wenu wa karibu kabisa.

Tukiona Watanzania wengi ni mapoyoyo, hiyo nayo ni sababu ya kuwa na taifa lenye watoto wenye mapungufu.
Tatizo siyo wanaoitwa au jiita ma "singo mama" tu, kuna watoto wengi sana wanaoambiwa "mamako alikufa" au "babako alikufa", kumbe ni uwongo mtupu. Huyo baba au mama aliyekufa isibaki hata picha? Au ndugu zake?

Ma singo baba, sababu zao ni nini?

Tusilee uozo wa maadili.
Watu wamekosa uvumilivu ktk ndoa!
 
Umewalaumu wanawake tu, ila jinsia zote zina tatizo.
Mkuu advantages za mwanaume na mwanamke zipo katika angle tofauti. Advantage ya mwanaume ni nguvu na advantage ya mwanamke ni ushawishi wa kingono.

Hii advantage ya mwanaume imedhibitiwa kwa kuwekewa sheria kali sana, ukilazimisha game unakutana na kifungo jela.

Lakini hii advantage ya mwanamke haijadhibitiwa, hakuna namna yoyote mwanamke anawajibishwa akitumia advantage yake ya ushawishi kingono.

Ndipo hapa linapokuja suala la ngono as long as mwanamke hajabakwa basi yeye ndie wa kulaumiwa.
 
Hili jambo ni serious.

Nakumbuka kuna jamaa alishawahi liandikia paper.

Ukiachana na ongezeko la single mothers kuna wanawake wengi mno ambao hawaolewi kabisa.

Kwakweli ipo haja ya hizi dini za mke mmoja kuangalia namna maana ndoa za mke mmoja zinazalisha masingle mothers wengi.

Mwanamke anaona umri unakwenda haolewi, bora azae tu.
Mwanamke akishaona hapati kijana atamuwezesha kuishi maisha anayotaka basi ndio hivyo ataamua kuzaa muda kukimbizana na muda na muda ni mchawi kwa mwanamke
 
Lawama zinavyotupwa kwa wanawake utadhani tunajizalisha wenyewe
Miaka ya 2000 mwanzoni binti kuzaa bila ndoa au kulipiwa mahari ulikuwa unawekewa kikao kipindi hicho wazee wetu tulikuwa tunawaita madingi lazima uwekewe kikao cha ukoo ueleze ilikuwaje
 
Nashukuru sana
Tusiingiliane mambo ya personal, jibu hoja zangu nijibu zako yamekwisha, sikuingia JF kutafuta mahusiano na mtu, iwe ye mtandao au vinginevyo.

Tuijuwe mipaka yetu.
 
Umaskini chanzo kikubwa cha single mothers
Hoja nyepesi sana hii, hebu fanya tathimin mwenyewe miaka ya nyuma na miaka ya sasa, miaka ya nyuma umasikini ulikuwa mkubwa, shule chache, ukipata nafasi ya kwenda shule utatembea umbali mrefu, huduma za afya zilikuwa hafifu au hamna kabisa katika maeneo mengi hasa vijini, sekta iliyokuwa inategemewa ni kilimo tu, katika hali hiyo ya umasikini single mother ulikuwa unawafuta kwa tochi, wanawake wa kizazi hicho walikuwa wanajiheshimu, walijua kuzivumilia hali zao, hawakuwa na tamaa ya vitu wasivyo na uwezo navyo, walijithamini zaidi kuliko kitu chochote.


Mabinti wa kizazi hiki tamaa iko mbele sana, wanatamani vitu wasivyo na uwezo navyo, hawajithamini kabisa kwa habari ya miili yao, zamani mwanamke kama hajakupenda mwili mwake hautaugusa, siku hizi ukiwa na pesa tu hata mke wa mtu unakula vizuri bila shida.

Shida sio umasikini ni tamaa, kuna familia ziko vizuri hizo shida ndogo ndogo hamna bado binti zao wanazaa kabla ya ndoa hapo bado utasema umasikini?
 
Back
Top Bottom