Wakristo, Hivi andiko gani limesema maiti azikwe akiwa kwenye Jeneza?

Wakristo, Hivi andiko gani limesema maiti azikwe akiwa kwenye Jeneza?

Una uhakika simu haipo kwenye maandiko? Dunia itakuwa kigajani ina maana gani? Kwamba kila kitu utakiona bila kificho.

Kitu nilichouliza. Tuliza akili ndo ujibu
Kuwa muelewa usiulize kitu km una majibu,imeandikwa wapi ktk Quran kuwa upande daladala,ukalie makochi,ukiswali utandike zulia,ukijenga nyumba uweke tiles au vioo ,ukioa basi ni vzr mkalala uchi,saa 2 ndio saa 8 au saa 9 ndio saa 3, siku km Ijumaa,Jms ,J2 zimeandikwa wapi mbn unazifuata,mwezi wa 1 una siku 31,wa pili siku 28/29 hizi tarehe na idadi ya siku zimeandikwa wapi,km Kila kitu kingeandikwa kwny biblia , bible ingekuwa kubwa sana na isingebebeka
 
24 Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo.
Mwanzo 50:24

25 Yusufu akawaapisha wana wa Israeli, akasema, Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu.
Mwanzo 50:25

26 Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.
Mwanzo 50:26
Umeprove andiko kuwa Misri ndiyo waanzilishi wa hii kitu.

Yusufu alizikwa kwenye sanduku kwa sababu aliiishi utamaduni wa Wamisri. Wamisri matajiri na wenye vyeo walizikwa ktk masanduku pamoja na sehemu ya utajiri wa vito vya thamani

Wayahudi hawakuwaga na utamaduni huu. Yesu alizikwa kwa kuviringwa kwenye sanda.
Lazaro aliyefufuliwa na Yesu alizikwa kwa kuviringwa kwenye sanda. Utamaduni wa wayahudi ni sanda kisha mwili unawekwa kaburini. Na kaburi zao hazikuwa za kuchimba chini. Wanachoronga mwamba.

Haya majeneza ni uharibifu wa mazingira tu
 
24 Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo.
Mwanzo 50:24

25 Yusufu akawaapisha wana wa Israeli, akasema, Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu.
Mwanzo 50:25

26 Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.
Mwanzo 50:26
Kama anataka kuelewa basi Mwanzo 50:26 imemaliza Kila kitu.
 
24 Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo.
Mwanzo 50:24

25 Yusufu akawaapisha wana wa Israeli, akasema, Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu.
Mwanzo 50:25

26 Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.
Mwanzo 50:26
 
Usitumie kitabu chochote cha dini, tumia tu akili uliyopewa na Mungu. Ulitoka tumboni kwa mama mtupu na utarudi kwenye udongo mtupu.
 
ukipata jibu namimi nijibu imeandikwa wapi tusafiri kwa kutumia magari na wakati punda wapo.

waarabu walizikwa pasipo ya jeneza kutokana na uhaba wa mbao uko jangwani kwao, ikawa ni kama sehem ya utamaduni wa mwarabu, mara imeingizwa ktk dini yetu pendwa ya kukopi na kupesti utamaduni wa mwarabu.

ukute ata kuvaa kobazi nayo ni sunnah
Kwa hiyo mpaka sasa waarabu hawa uwezo wa kuzika kwenye sanduku?wewe unawazi uwezo sio[emoji14][emoji14]
 
Back
Top Bottom