Sio Waislam walioanzisha vita kuu mbili za dunia, hizo nchi zote za kiislam ulizozitaja ukizijumlisha idadi ya watu waliouawa katika hizo vita zao hazifikii idadi ya waliokufa kutokana na vita kuu za dunia ambazo hazikuanzishwa na Waislam.
Sio Waislam waliochinja mayahudi milioni 6 wala sio Waislam waliotumia mabomu ya nyuklia (zote hizo ni vita kuu ya pili ya dunia), mabomu ya nyuklia yametumika mara mbili tu na waliotumia sio Waislam.
Sio dola za Waislam zilizoua mamilioni huko Korea na Vietnam.
Sio Waislam wanaoongoza na kuanzisha magenge ya kuuza madawa ya kulevya huko Latin America (drug cartels na narco-terrorism) magenge ya uhalifu na ya madawa ya kulevya ya Latin America yanafanya ukatili na unyama ISIS/Daesh hawaoni ndani.
Sio nchi za Kiislam zinaongoza kwa gun violence. Wala rape.
Hata baadhi ya nchi ulizotaja kama Afghanistan na Iraq unaelewa zilichafuka kwa sababu gani.
Wanaoichochea Congo izidi kuwaka moto nadhani unawajua.
Sio Waislam walioanzisha genocide Cambodia wala Rwanda.
King Leopold wa pili ambaye utawala wake uliua mamilioni Congo, hakuwa Muislam.
Sio Waislam walioua nakufanya genocide dhidi ya native Americans.
Nadhani unajua kuwa mpaka karne ya 20, nchi za Ulaya zilikuwa zinapigana vita zisizo na kichwa wala miguu. Kama Hundred Years' War, The Thirty Years' War, The Seven Years' War na kadhalika
Stalin, Mao Ze Dong, Polpot, Lenin, Trotsky hawakuwa waislam (walikuwa atheists). Kusanya watu wote unaodhani waliuawa na Waislam hawafikii idadi ya waliouawa chini ya hao.
Nadhani unajua ni nani aliwafuata Waislam Palestina, sio Waislam ni mayahudi wazungu kutoka Ulaya ambao sio Waislam, ambao ironically walikimbilia Mashariki ya Kati kukimbia mateso ya "ndugu" zao ambao pia sio Waislam. Na sasa unaona wanachowafanyia ndugu zetu huko Palestine (Allah awanusuru ndugu zetu wanaoteseka Palestina na kwengine kote Duniani).
Ukristo unahubiri upendo wa Crusades? Genocide dhidi ya wenyeji Marekani? Kuwaua wenyeji Canada, Australia na New Zealand na kuwapokonya ardhi zao?
Sio Waislam walioanzisha Apartheid Regime Afrika Kusini.
Struggles dhidi ya Ukoloni zilizomwaga damu huko Zimbabwe, Angola, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini hazikuwa struggle za kupambana na Waislam. Zilikuwa za kupambana na dhulma za wasio Waislam.
Ooh! Nilitaka kuisahau Ukraine!
Na kadhalika na kadhalika.
.↙️NIMEONA ULIPITA KIMYA KIMYA NIKAONA NI COPY NA KU-PASTE ILI UTULIZE KICHWA USOME