Katika matatizo ya Islamophobes ni kama haya. Nje ya Uislam jamii zote za binadamu utakuta tabia ya ukabila na kujifakharisha kwa nasabu.
Unatia aibu. Inaonesha huijui kabisa kabisa historia ya Uislam.
Halafu ni Uislam ndio umekuja kuondoa ukabila na ni Uislam ndio dawa ya ukabila. Malcolm X anakwenda Hijja miaka ya 60 kashangazwa na aliyoyaona kule mpaka akaandika barua kutokea Makkah ndani yake akielezea aliyoyaona. Anashangaa watu ambao wameunganishwa na Imani wako bega kwa bega katika Ibada na wako rangi tofauti na jamii tofauti, kitu ambacho kwao hakukiona wakati ambao watu weusi baadhi ya sehemu Marekani wakikatazwa hata kuchanganyika na weupe makanisani.
Allah said:
إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ
Verily, the most noble of you to Allah is the most righteous of you.
Surat al-Hujurat 49:13
Abu Nadrah reported: The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَلَا إِنَّ رَبَّكُمْ وَاحِدٌ وَإِنَّ أَبَاكُمْ وَاحِدٌ أَلَا لَا فَضْلَ لِعَرَبِيٍّ عَلَى أَعْجَمِيٍّ وَلَا لِعَجَمِيٍّ عَلَى عَرَبِيٍّ وَلَا لِأَحْمَرَ عَلَى أَسْوَدَ وَلَا أَسْوَدَ عَلَى أَحْمَرَ إِلَّا بِالتَّقْوَى أَبَلَّغْتُ
O people, your Lord is one and your father Adam is one. There is no favor of an Arab over a foreigner, nor a foreigner over an Arab, and neither white skin over black skin, nor black skin over white skin, except by righteousness. Have I not delivered the message?
Source: Musnad Aḥmad 22978, Grade: Sahih
Uislam gani unaouzungumzia?
Amr ibn al-‘As reported: The Prophet, peace and blessings be upon him, said, “Verily, the relatives of my father are not my allies. Verily, only Allah and the righteous believers are my allies. Yet, they have the bonds of kinship and I will uphold their family ties.”
Source: Ṣaḥīḥ al-Bukhārī 5990, Ṣaḥīḥ Muslim 215
Ndio hoja yako hii kuonesha kuwa Ukabila ni "core values" ndani ya Uislam? Hizi ndio "Logic" mnazosoma sio? Kwanza, kuoana wenyewe kwa wenyewe sio ushahidi wa kuonesha ukabila.
Pili, kuuhusisha desturi hii na Uislam au waarabu peke yao ilhali jamii zote za binadamu zina kawaida ya kuoana wao kwa wao, huo ni ujinga au chuki tu au vyote kwa pamoja.
Tatu, Uislam haujakataza kuoa nje ya race, tribe au ethnic group yako. Ili mradi tu ufuate Shari'ah ya Dini katika Ndoa, unaweza kuoa kabila lolote au rangi yoyote. Na katika Uislam kuna interracial, inter-tribal, inter ethnic marriages nyingi mno. Hili halipaswi hata kuwa mjadala.
Mtu kuoa au kuolewa na rangi fulani au kabila fulani ima ni la kwake au la kwengine ni chaguo lake kwa sababu tofauti tofauti zinazokubalika. Afuate tu Shari'ah ya Dini inasemaje.
Umoja na kuungana ni katika Tawheed (kumpwekesha Allah). Hii sio dini ya ukabila. Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) alipigana mpaka na kabila lake la Quraysh kwa ajili ya Dini hii na katika waliokuwa pamoja naye wapo mpaka watu weusi akina Bilal (Allah Amridhie yeye na Maswahaba wote wa Mtume).
Ni katika Uislam ndio watu kama Swahaba mtukufu Bilal (Allah Amidhie) ambaye alikuwa mtumwa mweusi kabla ya Uislam, baada ya Uislam akawa ni Muadhini wa kwanza. Mtu aliyeitoa Adhana juu ya Ka'abah Tukufu.
Uislam sio Dini ya ukabila ndio maana Abu Lahab ataingia motoni wakati ni baba yake mdogo Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na Bilal (Allah Amridhie), mwafrika ataingia peponi. Abu Talib ataingia motoni ilhali ni baba yake mkubwa Mtume na alimtetea Mtume kwa sababu ya ukabila na ujamaa. Ndio maana akina Abu Jahal na 'Utba Bin Rabi'ah wataingia motoni japo walikuwa kabila moja na Mtume na waliishi Makkah karibu na Ka'abah.
Uislam sio Dini ya ukabila, ndio maana ukakuta Maswahaba wa Mtume waliokuwa weusi (Bilal, Ummu Ayman, Wahshi, na kadhalika), waliokuwa wafursi kama Salman al-Farisy, waliokuwa wana asili ya uyahudi (wakaja kusilimu) kama 'Abdullahi Ibn Salam, Mama yetu Safiyya Bint Huyayy (Mke wa Mtume) na wengineo wengi Allah Awaridhie wote. Kuna wanafunzi wa Maswahaba ambao walikuwa sio waarabu, kuna wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahaba ambao hawakuwa waarabu, kuna Maimam wakubwa katika Dini hii ambao hawakuwa waarabu kama Imam Bukhari, Imam Abu Dawud, Imam Tirmidhi, Imam Nasa'i, Imam Ibn Majah, Imam Abu Hanifa na wengineo wengi kutoka zamani mpaka sasa.
View: https://youtu.be/yAzlsFDmsJI?si=fIA7bI8SnTe7qLcE
Dini hii imetumikiwa na kila jamii. Bado Dola za jamii tofauti tofauti kama Waturuki (Seljuqs, Ottomans na kadhalika), Wakurdi (akina Salahuddin al - Ayyubi), Songhai Empire, Mali Empire akina Mansa Mussa waafrika, Almohads (Al Muwahhiduun) na AlMoravids (Al Murabituun) Wa Berber wa Afrika Kaskazini, kuna Waajemi, na wengineo. Wote wameitumikia Dini hii tukufu ya Uislam.