Wakristo tushukuru sana ndoa zinaweza kuvunjwa mahakamani, Makanisa hayana msaada, Sheria zetu za ndoa zipo mdomini tu ila si kwa uhalisia


nani hafati sheria hii??

kama haifiatwi unadhani kwanini mletamada kaja kulia hapa??

hakuna mlango wa talaka,kuna mlango wa kutengana,ndoa iko pale pale.msijifanye kuujua sana ukristo kwenye mambo mnayotaka yafurahishe tamaa zenu za kimwili.
 

mimi nashangaa mkuu,mtu anataka koti la ukristo ila ya ukristo hayataki[emoji23][emoji23][emoji23].
ooooooh uislam una sheria tamu za ndoa,sasa si usilimu ukaoe hao wake 4 na kuwaacha hata ukivuta bangi[emoji23][emoji23]
ndio maana RC ina kanuni yake inaita”kujitenga na kanisa”yaani wewe mwenyewe kwa uamuzi wako unafungua buti na kushika njia zako,wala hawakukimbizi.

sasa huyu jamaa anakomaa na jambo ambalo liko mikononi mwake,vunja ndoa jichukulie kimada wako wa maisha muishi,simple as that.hakuna ndoa tena ya kanisani.
 
Usilete mambo ya sheria hizo za serikali na watu, tuwe strict kwenye sheria za ukristo tu.

Unaposhiba ni vema uwajue na wenye njaa, si vema kwasababu ndoa yako imeshiba basi usitilie maanani zenye matatizo.

Ndio maana nimeweka hapa tukio moja wapo kuonyesha udhaifu wa sheria za kikristo kwenye ndoa.

Imetokea mmeoana mkiwa vijana wadogo tu mna miaka 23 alafu mwenzako anafungwa jela kifungo cha maisha, Inabidi ukae bila mke mpaka uzeeni na hata kifo ?

Usidhani wanaokwenda jela wote wana hatia, wengine wanasingiziwa, wengine kubambikiwa, wengine hufanya kosa bila kukusudia, n.k
 
Ila itabidi watu wachunguzane kabla, suala la kuvunja ndoa ni hatari sana haswa kama mna watoto.
 
Huu ni uzembe wa wanaume wanao waoa. Fanya ichunguzi wako vyema acha mahaba kwanza kama kweli unataka mke.

Vijana wengi wanaangalia mwanamke mwenye shepu, sura, na muonekano watu wamsifie anamke mzuri.

Kumbe sura na vyote hivyo havina maana bali ulinganifu na dhamira maisha, ucha Mungu, maono yanayoemdana (sufuria na mfuniko). Vijana wengi badala ya kutafuta mifuniko itayoifumika sufuria wao wanaenda kutafuta sufuria zingine tena size tofauti. Aidha utazama humo ndani au hiyo hiyo sufuri itakua ndogo.

Mfano; vijana mnatafuta wanana wanaofanya kazi eti kuongeza kipato cha familia sawa.

Je upo tayari aende kufanya kazi zake za shift usiku

Je upo tayari afanye safari zake za kikazi na boss wake n.k

Vijana wengi hawawezi hili hata kidogo ndio maana kipato au kazi sio mojawapo ya kigezo cha mke bora.
 
Ila itabidi watu wachunguzane kabla, suala la kuvunja ndoa ni hatari sana haswa kama mna watoto.
Hata ukichunguza hakuna anaeijua kesho,

Inatokea paap, Mke wako labda kahamishwa kikazi kwenda Marekani, wewe unabaki hapa bongo na kazi yako.

Anarudi mara 1 kwa mwaka mnaonana kwa wiki 2 tu,

Wewe kama mwanaume hapo ambae ni rijali, huoni pana tatizo.
 
Hili suala ni mtihani sana kama mwanamke anafanya kazi ni balaa kabisa.😅😅
 
Hili suala ni mtihani sana kama mwanamke anafanya kazi ni balaa kabisa.😅😅
Na ulimschunguza ana tabia njema na bado anaendelea kuwa mwema lakini sasa yupo huko ughaibuni karibu mwaka mzima, hapo sasa /
 
Vipi kuhusu mke wako kuanza kukunyima tendo mwaka mzima na viungo vyako vya uzazi kila siku vinajaa

usijibu kama huna nguvu za kiume ama ni shoga
Ila hua kuna sababu mkuu..itibu hiyo sababu
 
Kuachana kwenye ndoa ni mpaka kifo kiwatenganishe ama moja wenu achepukue,

Nje ya hapo ni dhambi.

Kwanini wakristo hawataki kufuata sheria zao ?
Huwa naona kama ndoa inafungwa na mahakama. Kanisani ni igizo tu.
 
Watu wana ingia kwenye ndoa wakija kupendana ndio kitu pekee.
Wanasahau Staha, uvumilivu na maarifa ya kudeal na matukio tofauti. Wisdom wisdom wisdom kujua uchukue ma'amuzi gani kwa wakati fulani ni ushindi mkuu.
WENGI wanao achana ukiwauliza utakuta bado wanapendana.
 
hakuna kuachana labda ununue magunia matatu ya mkaa umchoe aishe
 
Kama hana hatia mpambanie mkeo atoke mje kula maisha.

Kabla ya kufunga ndoa uliyajua hayo kwamba ni wako katika shidana raha?

Kama ulijua haya yote kwa nini unalamika sasa.

Njia rahisi jitenge na kanisa kaoe huyo unayemtaka kwa utaratibu mwingine, wa kimila au kiserikali.

Angalizo: kwenye cheti imeandikwa ndoa ya mke mmoja au wake wengi. Basi hata huku serikalini hutafunga ndoa ingine mpaka uivunje ya kwanza.

Pia tambua hata huko serikalini mojawapo ya sharti la kuvunja ndoa lazima pande zote mbili ziridhie kuivunja.
 
Sababu yake umrudishe mama yako mgonjwa kwao kijijini, hataki awepo
Au mama anawafitinisha? Ila hata kama...HAKUNA KAMA MAMA... Nakuelewa...kiatu chako kinabana.....mpambanie Mama..mengine 🚮
 
Kanisa linafungisha ndoa halafu cheti kinatoka serikalini na kanisa halina uwezo wa kuvunja ndoa. Bali serikali halafu padri anasema alichokiunganisha Mungu wanadamu asiwatenganishe
 
Umeishiwa point huna kingine zaidi ya kuanza kutaja mambo ya vyeti,

Mtu afungwe jela maisha uishi single mpaka kufa, be serious!!!

halafu hio ni scenario moja tu, na mke wako akipata kazi huko ulaya huku wewe una kazi yako huko Ruvuma anakaa mwaka mzima kwa siku 10 tu hapo vipi ?

Acha kuchukulia mambo kirahisi rahisi
 
Au mama anawafitinisha? Ila hata kama...HAKUNA KAMA MAMA... Nakuelewa...kiatu chako kinabana.....mpambanie Mama..mengine 🚮
Na ndipo unapokuja kuelewa kwamba sheria za kikristo ni za mdomoni tu hazina ukamilifu katika uhalisia.

Hapo hamna namna itabidi muachne tu, mama abaki
 
Hekima ya mwanadamu ni upuuzi mbele za Mungu. Yeye aliyesema alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikivunje alikuwa na Helma sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…