Wakristo wasio Wasabato wanaruhusiwa kula paka, panya, kobe, kinyonga, kenge, kunguru, nyani, n.k?

Ubarikiwe Mtumishi hakika umemueleza ukweli, shida hawajui maana ujio wa Yesu Kristo! Na bila Yesu kumtafuta Mungu ni bure
 
Tafuta pesa dogo, tafuta pesa, narudia Tena tafuta pesa achana na mambo ya kutafsiri maandiko! Muamini MUNGU, hio inatosha saaaana
 
Uzoefu wangu kwenye hizi nyama, binafsi nguruwe sili kabisa japo sizuiwi na yeyote yule lakini Nyani nilikula kwa wamatengo mbinga, Ngedere nilikula butembo congo wao wanaita makako, mamba supu yake nilikula Masakaa Uganda, maduduwasha yale nilikula zambia na shima au ugali, Nyoka nilikula kwa jamaa mmoja bangedaido kama unaenda kisangani, wale panya wakubwa nilikula mtwara, na kuna vindege fulani nilikula kondoa, katika vitu vyote sikuwahi kuona tatizo lolote hivo toka nimekula hivo vitu hua siwezi kumhukumu mtu kwa sababu ya kitu anachokula maana hata hivyo nilivyokula wala sikuwahi kudhurika, hivo tuheshimiane kama wewe hauli acha wanaokula waendelee kula sio kesi
 
Si wakristo wala waislam wote wameshindwa mpaka sasa kumjibu hamis77 kimaandiko.

Wengi wanajibu tu kufuata hisia zao ila wanaojibu kwa kufata maandiko ni wachache.

Mnaokula teteeni hoja zenu basi, nasi wengi tujifunzege hapahapa.
 
Allah kasema Ukibanwa njaa kula ,wewe unasema kakataza
 
....Wakristo wengine wakadhani ni Yesu kawapa kibali wakaona ni ruksa ya kula chochote. Sasa najiuliza kwamba mbwa, konokono, vinyonga, kunguru, paka, chunusi, kobe, n.k wanaweza kuliwa?
Tena umejichelewesha sana kuuliza swali kwa kuzunguka na maneno mengi. Hakuna dhambi yoyote kula kitu chochote. Kiroho hakuna kosa lolote, iliyobaki ni uvumilivu na utamaduni, ambavyo kiroho havina nafasi yoyote
 
nguruwe ni haramu, hilo halina ubishi, wanaokula wale tu ila biblia imekataza
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Huyo wa uko kwenu.
Allaha kasema ,au unambishia


Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi kula Mizoga na Damu na nyama ya Nguruwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
 
Hiyo dharu
Allaha kasema ,au unambishia


Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi kula Mizoga na Damu na nyama ya Nguruwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Dharula haipo!! Kwa maana iyo haiwezi kutokea 😂😂😂sema dharura ipi..angalia conditions endelea kusoma mpaka chini utajua nn alikuwa ana maanisha
 
1 WAKORITHO 6:12 Kila kitu ni halali kwangu,”lakini si kila kitu kina faida. “Kila kitu ni halali kwangu,”lakini sitatawaliwa na cho chote.
 
shika adabu yako wewe unayeabudu siku badala ya mungu aliziumba siku ......
 
nguruwe ni haramu, hilo halina ubishi, wanaokula wale tu ila biblia imekataza
Achana na sheria za Wayahudi, fuata maelekezo ya Mungu. Kumbuka, sheria zile ziliwataka hata wazinzi wauawe. Sasa kwa nini mmeendelea na ya nguruwe mkiacha ya wazinzi?


2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha. 3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. 4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. 5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? 6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. 10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…