Wakristo wasio Wasabato wanaruhusiwa kula paka, panya, kobe, kinyonga, kenge, kunguru, nyani, n.k?

Context katika hilo fungu haikuwa aina ya chakula bali issue ilikuwa ni kunawa mikono
Kwenye mjadala Yesu na wanafunzi haikuwa aina gani ya chakula iliwe au isiliwe
waroho wanadakia kula kila kitu
 
uzoefu wako hauwezi kuwa ndo marking scheme ya ulaji
mtoa mada ameonyesha kile biblia inasema
 
Sili nguruwe ni mchafu sana kama mwenzake bata. Ila nikiwa na njaa na hakuna alternative nitaomba na ndimu. Haya mengine mbwembwe za dini tu tukiwa tumeshiba, hakuna binadamu wa kushindana na njaa.
 
Aliyekudanganya ya kupiga wazinzi imeondolewa Nan?


Soma BIBLIA VIZURI , HIYO SHERIA IPO ILA WAPIGAJI HAWAPO

SHARTI LA WAPIGAJI MAWE LAZIMA WASIWE NA DHAMBI


YESU ALIRUHUSU APIGWE MAWE ,

7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.





Tatizo mnasoma Biblia Kama mnafukuzwa,ndio maana kina Gwajima wanawaburuza, kina mwamposa wanawauzia maji na chumvi.
 
Ukiacha ukristo, lila kiumbe kinaliwa inategemea uko upande gani wa Ulimwengu huu.
 
1 WAKORITHO 6:12 Kila kitu ni halali kwangu,”lakini si kila kitu kina faida. “Kila kitu ni halali kwangu,”lakini sitatawaliwa na cho chote.
BIBLIA HAISOMWI HIVO, NDIO MAANA MNAFUNGUA MAKANISA KAMA UYOGA


Ikiwa kuna aya zinazowachanganya Wakristo wengi, pamoja na Waislamu, ni zinazotoka katika Nyaraka za mtume Paul, na ndio maana hata mtume Petro alitoa angalizo juu ya usomaji wa nyaraka za Paulo na akatoa onyo lifuatalo:
#2 Petro 3:15-17
Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.

Sio Petro tu ndio anadai kwamba nyaraka za Paul ni ngumu, bali hata watu wengine pia wanasema nyaraka za Paul ni ngumu, Na Paul yeye mwenyewe anashuhudia kwamba watu wanasema nyaraka zake ni nzito/ ngumu:

2 Wakorintho 10:9-10

nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu.
Maana wasema, Nyaraka zake ni nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini ni dhaifu, na maneno yake si kitu.
 
Acha kuweka assumptions zako, original manuscripts zitaonesha.

Hata hivyo kama ungekuwa umejifunza hebrew, aramaic na greek language utagundua maneno mengi sana kwenye kingereza na hatimaye kiswahili yaliongezwa ili kuleta tafsiri inayoshabihiana na kilichoandikwa kwenye original manuscripts. Hii inatokana na fact kwamba kiingereza na kiswahili ni lugha zenye maneno machache kuliko hebrew na greek language.
 
Biblia ya kwanza kutafsiriwa kuja kiingereza mwaka 1600 king james haikuongeza kitu wala kupunguza kitu, walitafsiri kama maandiko yalivyo, biblia hiyo haina mabano kama biblia hizi mpya, huku biblia za kiswahili ndio kabisa wameunganisha maneno ya kwenye mabano
 
Hakuna alipomuhukumu Mtumishi wa Mungu yeyote isipokuwa amewachukulia mfano kwa kupotosha maandiko matakatifu (BIBLIA) kwa watu wa Mungu.

2 TIMOTHEO 3:16-17.

[16]Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

[17]ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

Basi yakupasa kuwa mpole watu wanapoelekezwa maana pia YESU ananena ole wake atayemuonea aibu mbele za watu naye atamuonea aibu mbele za Mungu Baba (YEHOVA).
 
Mwamposa na wanaofanana nae hawajawahi kuwa watumishi wa Mungu

Mtumishi gan nitajie anauza maji,mafuta,chumvi , n.k

Nitajie kwenye maandiko, ndipo utajua hao ni MATAPELI
 
Mwamposa na wanaofanana nae hawajawahi kuwa watumishi wa Mungu

Mtumishi gan nitajie anauza maji,mafuta,chumvi , n.k

Nitajie kwenye maandiko, ndipo utajua hao ni MATAPELI
ISAYA 8:19-20.

[19]Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?

[20]Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.

Mungu ananena Manabii wanapaswa kuenenda kwa "SHERIA na USHUHUDA"

* SHERIA = AMRI 10 ZA MUNGU/KANUNI NA TARATIBU ALIZOWEKA MUNGU KWETU BINADAMU ILI TUZIFUATE.

* USHUHUDA = MATENDO WALIYOFANYA MANABII NA YESU.

Je Nabii yupi alikuwa anauza maji, mafuta, chumvi ili kueneza injili ya Mungu?

Yesu alielekeza wapi huduma za Mungu ziwe zinauzwa?

MATHAYO 10:8.

[8]Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

Roho Mtakatifu hutoa karama za UNABII, KUOMBA, KUFUNDISHA, KUNENA KWA LUGHA, KUTAFSIRI NDOTO, kwa kadri anavyopendezwa tena wala si kwa thamani yoyote ile ya gharama.

Hao akina Mwamposa, Gwajima n.k. wajitafakari sana njia zao maana Mungu anaonya;

MATHAYO 18:7

[7]Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!
 
Maelezo yote haya bila kuweka kifungu/Vifungu vya biblia ni ubatili mtupu
 
Kwanza wasabato sio wakristo.

Wasabato bila kujua ni wafuasi wa freemasonry.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…