Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu hiyo ndio kauli ya wakulima. Ndio kauli ya pamoja, Ndio msimamo wa wakulima, Ndio uamuzi wa wakulima, Ndio Hitimisho la wakulima. Wakulima wanasema na kuapa kuwa watamuunga mkono Rais Samia katika uongozi wake wa kuendesha serikali yake ya CCM, wameapa kumpa ushirikiano wa kutosha yeye na serikali yake.
Wakulima wanasema Tangia kupata Uhuru kwa nchi hii kwa Mara ya kwanza mkulima amekuwa na sauti katika soko la mazao, Sasa kilimo Ni Biashara yenye Faida, kilimo Ni ajira ya uhakika, kilimo Sasa Ni Tumaini la wanyonge, kilimo Sasa kinatoa Nuru katikati ya Giza, kilimo Sasa kinawatoa kimasomaso wakulima, kilimo Sasa kinapunguza umaskini wa Kaya mojamoja. Ardhi Sasa imekuwa na thamani, inatoa matumaini kwa yeyote atakaye weka jembe ardhini, inatoa Neema kwa kila atakaye weka mbegu ardhini, inatoa matumaini kwa yeyote mwenye kulishika jembe
Wakulima wanamshukuru Rais Samia kwa namna alivyokikuza na kukipa thamani kilimo, kwa namna alivyomjari mkulima, kwa namna alivyomfungulia milango ya biashara mkulima, kwa namna alivyokipa heshima na kukiheshimisha kilimo na kukipa Thamani. Sasa vijana wanakimbilia katika kilimo,Sasa vijana wanatafuta ardhi ili walime. Sasa vijana wanajitupa katika kilimo ili watoke na kuinuka kiuchumi.
Hapa ndipo wakulima kwa kauli moja wanaposema kuwa Rais Mama Samia Atoshaa, Amekonga nyoyo za wakulima na wao wameamua kumlipa kwa kumuunga mkono na kushirikiana naye. Huwaambii kitu wakulima kwa Sasa juu ya Rais Samia kutokana na namna wanavyompenda na kumkubali, hasa baada ya kutoa mabillioni ya Ruzuku katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei sokoni.
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627