Wakuu maternal death ( kifo cha mama mjamzito) kinaweza kupoteza kazi au kufungiwa leseni?

Wakuu maternal death ( kifo cha mama mjamzito) kinaweza kupoteza kazi au kufungiwa leseni?

Hospital za serikali inabidi wapokee tu wanakuwa hawana jinsi, hapo vifo nje nje. Mtu anaenda kujifungua ana upungufu wa damu tayari maana hata zile dawa za kuongeza damu hakunywa. Majanga juu ya majanga.
Kuna mmoja ananiambia anakula mboga za majani damu ipo nimeshangaa labda uzoefu maana ni mtoto wa 3,mm nilimeza hizo dawa na nilikuwa na akiba zikiisha kabla ya siku ya kwenda naendelea kumeza
 
Ulivyo onesha hofu kupitia bandiko lako inaonekana hauko experienced kabisa.

Kwa nini hukufanya kila liwezekanalo mpka akavuja damu mpaka kifo?

Yaani mjamzito anafika hospotalini kwa ukosefu wa damu na wewe upo?

Au haukuwa kazini na ukaachia mtu baki, au wale wa field wafanye hilo?
 
Sasa mbona unanitisha😔
Ndio hivyo .

Mama kabla hajawa discharged lazima afundishwe umuhimu wa family planning, umuhimu wa hygiene , umuhimu wa breastfeeding sana sana exclusive breastfeeding, dalili hatarishi ambazo huenda akakumbana nazo nk.

Lazima aambiwe umuhimu wa hormonal , muscle and nutrients recovery kupitia spacing ya kutosha. Mama anayebeba beba mimba hovyo bila kuzingatia spacing anapelekea muscles kuchoka (exhausted) nk.
 
Unatisha watu em tulia kwanza mkuu
Ni miongoni mwa vitu ambavyo mama anabidi afundishwe kabla hajaruhusiwa kwenda nyumbani.

Lazima afundishwe family planning hata kama alishafundishwa kipindi cha antenatal , lazima ajue proper spacing ya kubeba ujauzito either kama alijifungua kwa njia ya kawaida (Spontaneous Vaginal Delivery (SVD)) au alijifungua kwa Cesarean Section (CS) na hata kama bahati mbaya ilitokea abortion , lazima afundishwe family planning na post abortal care.
 
Kuna mmoja ananiambia anakula mboga za majani damu ipo nimeshangaa labda uzoefu maana ni mtoto wa 3,mm nilimeza hizo dawa na nilikuwa na akiba zikiisha kabla ya siku ya kwenda naendelea kumeza
Hii taarifa haijakamilika,

Kwamba anakula mboga za majani damu ipo chini au vipi?

Kama ishu ipo hivyo tatizo bila shaka litakuwa lipo kwenye mapishi, huenda anazipika kwa muda mrefu hivyo anavunja zile bonds hivyo anakula makapi.

Ajitahidi mboga zisiive sana (fresh green vegetables) pia apendelee kula matunda yenye vitamin.C kwa ajili ya kuongeza absorption ya hizo iron.
 
Acha aongee ukweli tuelimike

Asante sana mkuu!
Na kingine chukua hii ikusaidie.

Mbali na kujua umuhimu wa spacing kati ya mimba moja mpaka nyingine.

Unapotaka kubeba ujauzito , mfano mwezi unaofuata unaweza ukaanza hata utaratibu wa kutumia zile dawa za damu kwenye low dosage ili kuhakikisha unakuwa na damu ya kutosha mwilini mwako.
 
Wakuu mama mjamzito amefariki wakati namzalisha baada ya kumwaga damu nyingi hali iliyopelekea kufariki hii tukio linastress sana na kunipa posttraumatic syndrome nalijitahidi kadri ya uwezo wangu kiukweli nilipaniki sana je maternal death ( kifo cha mjamzito) inaweza kufungiwa leseni yangu na kufukuzwa kaZi?

Halmashauri( CHMT) wasimamizi wa afya ngazi ya halmashauri wameniambia nisimuhumudumie mgonjwa, mjamzito au mteja yoyote yule)
Kwani unalipwa bei gani mpaka unapata stress na kazi za kijinga? Wenzio wanateka na kuua na wanaishi vizuri tu. Kupanga ni kuchagua. Kazi za afya hasa hospitalini zina stress za kijinga sana not worth it.
 
Sikupona, nikaenda kwa daktari mwingine akafanya assessment + full lab, akacheck na past diagnosis,alichogundua hata lab results zao ni fake na inawezekana hawakufanya (was just a made up BS),nilipona within a week
Kwenye lab.results niliwahi kuwekewa jina tofauti na la kwangu. Huwa nina katabia ka kupitia majibu kabla ya kurudi kwa Dr.

Ile napitia nakuta jina sio la kwangu, nikarudisha kwa mtaalamu, akadai ni mistake tu imefanyika kwa upande wa jina lakini majibu ya vipimo ni ya kwangu.

Just imagine umepewa majibu ya watu halafu kitu imesoma “Imooo” Si wataua watu kwa mshtuko.

Kuweni makini tusije kupiga ukunga mahospitalini jamani 😁😁😁.


Changamoto nyingine ipo kwa mama wajawazito kutoa taarifa za uongo kuwahusu.
Huwa wanadanganya kusema ni mimba ya kwanza kuepusha kuambiwa kwenda hosp. za wilaya kutokana na umbali na gharama.
 
Back
Top Bottom