Wakuu maternal death ( kifo cha mama mjamzito) kinaweza kupoteza kazi au kufungiwa leseni?

Wakuu maternal death ( kifo cha mama mjamzito) kinaweza kupoteza kazi au kufungiwa leseni?

Ndo maana hospital nyingi hazipokei wajawazito waliomis session tatu na zaidi, wazee tuwapeleke wake zetu clinic asee

Tunatafutia wenzetu matatizo yasiyo na msingi
Hospital za serikali inabidi wapokee tu wanakuwa hawana jinsi, hapo vifo nje nje. Mtu anaenda kujifungua ana upungufu wa damu tayari maana hata zile dawa za kuongeza damu hakunywa. Majanga juu ya majanga.
 
Mjini kuna watu hawako serious hivi?
Mkuu, yaani hapa Bongo wajawazito ambao wako serious hawafiki 30% nakuhakikishia hilo. Na hao ni familia ambazo zimeelimika sana yaani wameenda shule hadi viwango vya juu na pia baba yuko makini. Wababa wengi pia hayo mambo ya kliniki hawayataki kwa sababu wanaogopa kupima HIV, kwahiyo wanakausha hawawakumbushi wake zao, ujauzito unalelewa hivyo hivyo kijima.
 
Dah! Sasa watoto wengine wanazaliwa na maambukizi kwa ujinga wa wazazi.
 
Ndiyo shida ya kuanzisha watoto shule wakiwa na miaka 4, anamaliza diploma akiwa na miaka 20.

Ona sasa mambo madogodogo kama haya hata bado haujui.

Na unapataje PTSD kwa changamoto ya kazi yako, kitu ambacho ni unajua kabisa in one way or another litatokea tu.

Sasa kama unapata PTSD kirahisi hivi, si confidence yote ya kuhudumia watanzania itaisha?
Majibu ya kiume ndo haya
 
Kwa hiyo ndio maana mnapeleka pesa za sadaka kwa mchungaji baada ya kujifungua salama na mkatoka salama wewe na mtoto badala ya kumpa daktari aliye hangaika na wewe OT aka angalia maendeleo yako kwa siku tatu kabla hajakuruhusu urudi nyumbani?
Pesa haziendi kwa Mchungaji,
Pesa zinaenda kwa Mungu.

Mimi binafsi huwa narudisha Shukurani kote,,Nikianzia na Daktari kwanza,,na Mungu aliyemtumia Daktari kuniponya lazima nitoe Shukurani,,na siyo lazima nitoe Kanisani.
Madaktari waliowahi kurescue maisha yangu sasahivi ni zaidi ya ndugu kwangu, na wanajua namna nawapenda, na namna nawapa Shukurani kila tunapoonana.
 
Kuna uzembe tena unakua wa wazi kabisa ambao mpaka unafanya sisi tusio watu wa fani hizo za tunajiuliza hivi hawa madaktari wamesomea na kupasishwa kabisa kuhudumia roho za watu au ni uhuni tu. Pamoja na hilo kuna uzembe pia kwa sisi wapokea huduma kwa kiasi fulani kunakukatisha tamaa hawa wanaotuhudumia kwa kutokuweka jitihada zozote ili tupate huduma ipasavyo. Kila mmoja anapaswa kuwajibika kwa nafasi yake. Na mwisho baada ya jitihada zote na kujitoa kuna bahati mbaya pia ko tusilaumu sana.
 
Yaani mkuu,hii ni changamoto kubwa. Vifo vya wamama havisababishwi na wahudumu wa afya pekee,vinaanza na uzembe wa mjamzito. Wajawazito wanaohudhuria kliniki ipasavyo hapa Bongo hawafiki hata nusu ya wajawazito wote. Bado kufuata ushauri wanaopewa na wahudumu wa afya, wengi hawaufuati bali wanasikiliza maneno ya mtaani. Bado siku ya kujifungua kuna ile tabia ya mjamzito kuchelewa kwenda hospital kwa madai kwamba anataka akifika tu ajifungue asikae na uchungu sana,mtu anakuja tayari ana hali mbaya,hapo wahudumu watalaumiwa tu bure. Jamii yetu bado haijaelimika kabisa kuhusu afya ya mama na mtoto,bado sanaa,na hivi vifo havitapungua hadi jamii ielimike. Yaani imagine hadi leo madaktari bado wanatumia nguvu kuwaelezea wamama umuhimu wa kunywa folic acid na dawa za kuongeza damu, kwa hali hiyo vifo vitaisha kama wajawazito bado wanakataa kunywa dawa ambazo zina umuhimu kwao na kwa mtoto?..Unakuta mtu anasema" kwani wahadzabe wanakunywa hayo madawa"?.
Ni kweli kabisa mkuu, lawama nyingi ni kwa wahudumu wa afya ila tunasahau kuwa wajawazito wengi hawafuati maelekezo ya wataalamu.
 
Yaani mkuu,hii ni changamoto kubwa. Vifo vya wamama havisababishwi na wahudumu wa afya pekee,vinaanza na uzembe wa mjamzito. Wajawazito wanaohudhuria kliniki ipasavyo hapa Bongo hawafiki hata nusu ya wajawazito wote. Bado kufuata ushauri wanaopewa na wahudumu wa afya, wengi hawaufuati bali wanasikiliza maneno ya mtaani. Bado siku ya kujifungua kuna ile tabia ya mjamzito kuchelewa kwenda hospital kwa madai kwamba anataka akifika tu ajifungue asikae na uchungu sana,mtu anakuja tayari ana hali mbaya,hapo wahudumu watalaumiwa tu bure. Jamii yetu bado haijaelimika kabisa kuhusu afya ya mama na mtoto,bado sanaa,na hivi vifo havitapungua hadi jamii ielimike. Yaani imagine hadi leo madaktari bado wanatumia nguvu kuwaelezea wamama umuhimu wa kunywa folic acid na dawa za kuongeza damu, kwa hali hiyo vifo vitaisha kama wajawazito bado wanakataa kunywa dawa ambazo zina umuhimu kwao na kwa mtoto?..Unakuta mtu anasema" kwani wahadzabe wanakunywa hayo madawa"?.
Kusikiliza watu wa mitandaoni ambao hawana hata elimu ya afya
 
Back
Top Bottom