Nimekuwa nikishuhudia jinsi vijana wengi wanavyojinasibu kuwa wanafanya biashara(crypto) , lakini maisha yao yanaendelea kuwa magumu kama yangu tu!
Unapotembelea mitandao yao ya kijamii, hasa kwenye status za WhatsApp, unakutana na jumbe kama vile "Financial freedom" na kadhalika. Lakini ukweli ni kwamba, haya maneno hayana mashiko kama huwezi kuonyeshs ushahidi wa mafanikio yao.
Mimi binafsi, nitakuja kuamini biashara zao pale nitakapoona mabadiliko chanya katika maisha yao. Pale nitakapoona ushahidi wa wazi wa mapato yao, na kuona hatua kubwa walizopiga kimaisha.
Jambo lingine linalonishangaza ni jinsi wa Afrika, hasa wabongo, walivyo wachoyo na wenye roho mbaya. Wanaweza kweli kukupatia mbinu/maarifa jinsi wanavyo tengeneza hiyo mipesa?
Vijana tafuteni mapori mkafyeke na mfanye kilimo, hakuna hela ya kupakua kama unapakua SINGELI