Wakuu na wajuzi, Israel (Mossad) imeruhusu vipi Iran kumiliki drones na silaha za kisasa hivi?

Wakuu na wajuzi, Israel (Mossad) imeruhusu vipi Iran kumiliki drones na silaha za kisasa hivi?

Iran ni adui mkuu wa Israel kwa sasa. Na Israel inekuwa ikuhujumu mikakati ya kisiraha hatarishi ya Iran miaka yote.

Ikumbukwe Moja ya sababu kushindwa kutoa mifumo ya Ulinzi Kwa Ukraine, Israel walesema mifumo yao ni Kwa ajili ya magurunet tu ya kawaida haitaweza kupangua makombora ya kisasa ya yanayosumbua huko Ukraine.

JE, taifa la Israel Sasa liko hatarini Kwa uhodari wa Iran?

JE, ni Urusi ndio inatengenezea Drone Iran ili kutengeneza tension Kwa washirika wa US huku zile zake za kisasa imeziweka kibindoni?

JE, Israel bado ina mifumo imara sana, na hizo drone ni chamtoto kwa Ulinzi wa Israel?

Karibuni
Ndo ujue kuwa propaganda za west zimewadanganya sana. Wakati Iran anazindua ndege, drones zake mara kadhaa media za west hadi humu kuna threads walikuwa wanasema mara ni matoy, mara molds tu za plastic wanaanza kuchambua hadi rangi, leo sijui kimekuwaje.
Muajemi sio level zetu wale jamaa wako vizuri.
 
Sasa mbona vikombora vya Hamas na Hezbollah vinawasumbua vile ,watu wanakufa na majumba yanabomoka,
Mrusi pekee ndio mkweli ktk silaha Ila Hawa wanaokomolewa kinyesi Ni mbwembwe tu, wote including Israel wamepeleka interception Ukraine by Russia anafanya anavyotaka
Hii ni kauli ya shabiki lialia wa mpira anayeshinda njaa vibanda vya kubeti. Israel haijapeleka air defence system yeyote Ukraine, hizo taarifa labda umezitoa kuzimu. Maroketi zaidi ya 2,400 yamezuiwa na Iron Dome pekee na success rate yake ni zaidi ya 95% hadi 97% kila series of attack.

Na kama una hasira nao, ulizaliwa ukakuta wanaishi kwa fujo na Waarabu, utakufa uwaache wapo palepale. Waarabu wenzio kina UAE walishaanzisha hata flights na wana mjadala wa kununua silaha kwao, wewe uko hapa na hasira zako. Wenzio hata nafasi ya kujilipua wamenyimwa
 
Nitajibu swali lako la mwisho.

Israel ndio nchi pekee duniani ambayo ina air defence system 24/7 ziko active. Wale muda wowote unawashtukiza unafyatua kombora na wanalifanyia interception. Ni gharama kubwa za uendeshaji ila wanalazimika maana wana maadui na confrontation yao ni active.

Nchi nyingine kama Marekani na Urusi wao hawana adui kila dakika, mpaka ufikie hatua Urusi awaze Marekani atafyatua kombora hapo kuna mnyukano wa hali ya juu ushatokea na tension kwenye majeshi ishafikia level 3 kwenye readiness. Mfano sasa hivi, sio Russia wala Marekani anayewaza kwamba mwenzie atamrushia kombora usiku huu. Ila Israel muda wote wanaishi kwa mashaka, 'magaidi' wanalipiza kisasi wakipata nafasi.
Hamas au Hezbollah leo wanalala wanajisikia vizuri usiku wanaamua wafyatue maroketi kwa mkupuo kisha watokomee.

Kama Israel ingekuwa na air defence systems mbovu tungeziona kwenye kurushiwa maroketi na Hamas inafeli. Ilifanya interception ya 97% ya maroketi, hapo ni baada ya radar kupima trajectory na kugundua yatadondoka sehemu ya makazi. Kama hayadondoki sehemu hatarishi yaanachwa ila hata hivyo hakuna anayerusha kombora porini labda lipotee njia. Picha ni Iron Dome ikiharibu maroketi anga la Tel AvivView attachment 2389617

Kuhusu kupambana na cruise missiles, drones, anti ship missiles na ndege wanayo mifumo kama Barak na Arrow 3 (kuna 2 pia)View attachment 2389616

Ballistic missiles wanao mfumo wa David's SlingView attachment 2389615Mifumo yao ni multi layelled na kila mmoja una kazi tofauti na mwingine.
Hakuna mfumo kamilifu unaofanya kazi zote, ndio maana walioicheka MIM Patriot ya Marekani kushindwa kuzuia suicide drones za Houthi zilizolipua matenki ya mafuta ya Saudi Arabia ndio hao hao walishangazwa na S-300, Pantsir na Tungushka za Urusi kushindwa na drones za Ukraine.

Morocco imeagiza AD system, nimeona na UAE inataka iagize, Finland nayo inachagua mmojawapo ya mifumo miwili ya Israel. India walikuwa na joint project
Nahisi uzi uishie hapa!! Umetema madini Sana mkuu
 
Hata mimi mwenyewe Sijakuelewa
Nimesema wengi mnayangalia mataifa haya kwa muonekano wa nje nasio muonekano wa ndani hivyo ndio wakubwa wa dunia wanataka nyie mjue hivyo kwamba ni maadui, lakin ukishajua yaliyo nyuma ya pazia ambao ndio ukweli halisi ulio katika muonekano wa ndani huwezi kudanganyika kwakua ukweli unaujua.
 
umeandika maneno mengi yasiyo na tija kama unajua si uongee
Unapoyangalia mataifa haya mawili ya irani na israeli inabidi uyatambue kimuonekano wa ndani bila kusahau muonekano wa nje, kwakuwa wew unayangalia kimuonekano wa nje, kutokana na kila taifa kupiga kwake hatua kubwa za maendeleo kijeshi na kwenye masuala ya sayansi na teknolojia.

Jambo unalotakiwa ujue urusi haitengenezei irani drone bali iran inatumia wanasayansi wake wa ndani, kwakua wew na watu wengi mmebase kwenye msimamo wa kuwa haya mataifa ni maadui na nikweli israeli na irani ndio mataifa yenye uwezo mkubwa wa kijeshi hapo mashariki ya kati.

Lakin hivyo ndio wakubwa wanataka nyie muamini hivyo kimuonekano wa nje kupitia migogoro yao kama israeli kuuwa wanasayansi wa nuclear wa irani na irani kusapoti makundi yenye uadui mkubwa na israeli kama hezbollah na hamasi bila kusahau wanavyotishiana kufutana kwenye ramani ya dunia.

Unachopaswa kujua matunduizi ni kuyatambua mataifa haya kimuonekano wa ndani na hapa ndio siri kubwa ilipo kati ya mataifa haya hivyo nimalizie kusema jitahidi kufanya research ya kutosha wew binafsi maana dunia ni zaidi ya tuijuavyo sie wanadamu.
 
Mzee maandiko yanasema ipo siku Israel watakuja kupoteana.

Yaani watapigwa wachakae sema bado sana.
Usemalo ni kweli ila kipigo hicho ni kwa sabab walimkataa Yesu na kwa sababu ya kumuasi Mungu, ila kumbuka pia after hicho Kichapo Yesu atatokea na mwishowe atawasaidia vita Israel atashinda na hao waliokuwa upande wa shetani yaani russia, iran, china, umoja wa ulaya na wengine ndiyo itakuwa mwisho wao! then utakuja utawala wa miaka 1000 wa Yesu hapa duniani akitawala tokea Israel kwa sasa naishia hapa.
 
Amemuacha apambane na mambo yatokanayo na kutokuvaa mashungi vizuri
 
Usemalo ni kweli ila kipigo hicho ni kwa sabab walimkataa Yesu na kwa sababu ya kumuasi Mungu, ila kumbuka pia after hicho Kichapo Yesu atatokea na mwishowe atawasaidia vita Israel atashinda na hao waliokuwa upande wa shetani yaani russia, iran, china, umoja wa ulaya na wengine ndiyo itakuwa mwisho wao! then utakuja utawala wa miaka 1000 wa Yesu hapa duniani akitawala tokea Israel kwa sasa naishia hapa.
Yesu atakuja kwa ajili ya walimwengu wote na KUHUKUMU KWA HAKI .sio kwa ajili ya wana Israel tu.maaana hao sidhani Kama watakuja kumkubali masihi
 
Nimesema wengi mnayangalia mataifa haya kwa muonekano wa nje nasio muonekano wa ndani hivyo ndio wakubwa wa dunia wanataka nyie mjue hivyo kwamba ni maadui, lakin ukishajua yaliyo nyuma ya pazia ambao ndio ukweli halisi ulio katika muonekano wa ndani huwezi kudanganyika kwakua ukweli unaujua.
umeandika upumbavu, na hivi unavyotaka kurekebisha ndio unaonekana mpumbavu kabisa
 
Kuhusu kurudi kwa yesu sijui...ila mwisho wa dunia watu wamekuwa wakisema umekaribia kabla hata yesu mwenyewe hajazaliwa.
Huyo bwana atarudi ataishi ataoa mke na kuzaa watoto ataishi miaka 40 na yeye atakufa.ila haya mambo ya mwisho wa dunia NI kweli yalisemwa tangu tangu na hata Adam aliambiwa ila kufika mwisho wa dunia NI kimbembe ila UPO.maana kila lenye mwanzo Lina mwisho
 
Hata hao unaowaona sio waisrael halisi @“khazarians” maandiko yaliandika waisrael watakua watumwa kwenye mataifani.
Shida ya hao jamaa ni ujeuri..ila wao ndo wanaongoza kwa kupewa mitume na manabii wengi.ila waliwakataa na wengine kuwauwa.siku nikipata hela natamani niende misri nikasome historia yao.uwa napenda sana
 
L
Iran ni adui mkuu wa Israel kwa sasa. Na Israel inekuwa ikuhujumu mikakati ya kisiraha hatarishi ya Iran miaka yote.

Ikumbukwe Moja ya sababu kushindwa kutoa mifumo ya Ulinzi Kwa Ukraine, Israel walesema mifumo yao ni Kwa ajili ya magurunet tu ya kawaida haitaweza kupangua makombora ya kisasa ya yanayosumbua huko Ukraine.

JE, taifa la Israel Sasa liko hatarini Kwa uhodari wa Iran?

JE, ni Urusi ndio inatengenezea Drone Iran ili kutengeneza tension Kwa washirika wa US huku zile zake za kisasa imeziweka kibindoni?

JE, Israel bado ina mifumo imara sana, na hizo drone ni chamtoto kwa Ulinzi wa Israel?

Karibuni
Labda kwanza tuanze kujiuliza uo uadui wao unatokaa na nn?
 
Huyo bwana atarudi ataishi ataoa mke na kuzaa watoto ataishi miaka 40 na yeye atakufa.ila haya mambo ya mwisho wa dunia NI kweli yalisemwa tangu tangu na hata Adam aliambiwa ila kufika mwisho wa dunia NI kimbembe ila UPO.maana kila lenye mwanzo Lina mwisho
Hivi mwisho wa dunia ni nini? Mwisho wa binadamu duniani, mwisho wa viumbe vyote, au mwisho wa hii sayari kabisa?
Kumbuka hii sayari imekuwepo kabla hata ya viumbe wote na tutaiacha.
 
hizo drones ni matokeo ya tech ya Usa drone ambayo ili tunguliwa 2011 na iran na kuanza kuzistudy na kuzifanyia modifications zao hivo hakuna jipyaaaa
 
Back
Top Bottom