Nitajibu swali lako la mwisho.
Israel ndio nchi pekee duniani ambayo ina air defence system 24/7 ziko active. Wale muda wowote unawashtukiza unafyatua kombora na wanalifanyia interception. Ni gharama kubwa za uendeshaji ila wanalazimika maana wana maadui na confrontation yao ni active.
Nchi nyingine kama Marekani na Urusi wao hawana adui kila dakika, mpaka ufikie hatua Urusi awaze Marekani atafyatua kombora hapo kuna mnyukano wa hali ya juu ushatokea na tension kwenye majeshi ishafikia level 3 kwenye readiness. Mfano sasa hivi, sio Russia wala Marekani anayewaza kwamba mwenzie atamrushia kombora usiku huu. Ila Israel muda wote wanaishi kwa mashaka, 'magaidi' wanalipiza kisasi wakipata nafasi.
Hamas au Hezbollah leo wanalala wanajisikia vizuri usiku wanaamua wafyatue maroketi kwa mkupuo kisha watokomee.
Kama Israel ingekuwa na air defence systems mbovu tungeziona kwenye kurushiwa maroketi na Hamas inafeli. Ilifanya interception ya 97% ya maroketi, hapo ni baada ya radar kupima trajectory na kugundua yatadondoka sehemu ya makazi. Kama hayadondoki sehemu hatarishi yaanachwa ila hata hivyo hakuna anayerusha kombora porini labda lipotee njia. Picha ni Iron Dome ikiharibu maroketi anga la Tel Aviv
View attachment 2389617
Kuhusu kupambana na cruise missiles, drones, anti ship missiles na ndege wanayo mifumo kama Barak na Arrow 3 (kuna 2 pia)
View attachment 2389616
Ballistic missiles wanao mfumo wa David's Sling
View attachment 2389615Mifumo yao ni multi layelled na kila mmoja una kazi tofauti na mwingine.
Hakuna mfumo kamilifu unaofanya kazi zote, ndio maana walioicheka MIM Patriot ya Marekani kushindwa kuzuia suicide drones za Houthi zilizolipua matenki ya mafuta ya Saudi Arabia ndio hao hao walishangazwa na S-300, Pantsir na Tungushka za Urusi kushindwa na drones za Ukraine.
Morocco imeagiza AD system, nimeona na UAE inataka iagize, Finland nayo inachagua mmojawapo ya mifumo miwili ya Israel. India walikuwa na joint project