Pia alikuwa mjumbe kwenye bunge maalum la katiba. Je alipambania maoni ya Wananchi? Mfano tulitaka mbunge awajibishwe kwa kutotimiza wajibu wake, lakini msimamo wa chama chake ulilazimisha akae mpaka amalize kipindi cha miaka mitano. Isitoshe wananchi tulitaka ukomo wa mbunge uwe ni kipindi Cha miaka 10, chama chake Bado kililazimisha akae zaidi ya miaka 10 ili mradi achaguliwe na wananchi! Yeye alikuwa upande wa maoni ya wananchi? Hii huruma ya Sasa inatoka wapi kama sio hadaa?
Hakuna mfumo hata mmoja unaompa nafasi mwananchi kuwajibisha mamlaka, lengo ni ili waitwe wanyonge na kupatiwa haki zao kama hisani ya viongozi wanaosaka madaraka.