Wakuu wa shule za sekondari nchi nzima Tanzania wamchangia Rais pesa za form ya kugombea Urais mwaka 2025

Wakuu wa shule za sekondari nchi nzima Tanzania wamchangia Rais pesa za form ya kugombea Urais mwaka 2025

Ubarakaka, Unafiki, kujikomba, na kujipendekeza ni Kansa ya hatari sana inayodumaza Maendeleo barani Afrika.
Samia anayejenga hotel ya nyota tano ndiyo wa kupitisha bakuli kwa watu wasio na uhakika wa kesho yao?
Ukitaka kum control mtu tengeneza mazingira ya njaa
 
Ignorance is eating Tz.. Hivi huu ukuu wa shule huwa zoazoa tu? Hivi kati ya hao elf 3+ hakuna mwenye akili ya kushtuka na kuwaza nje ya box? Hivi hawa wanajua majukumu yao na miiko yake kweli.

"Mfanyakazi wa SERIKALI haruhusiwi kushaaabikia siasa na kuonesha upande wake waziwazi. Pia haruhusiwi kujihusisha na siasa ktk mahali pa kazi wala kugombea nafasi yoyote ya uongozi hadi atakapostaaf au kuacha kazi". Sasa hawa wavaa kaunda hawakulijua hili? Hawakujua kuwa kwenye kile kikao walikuwa kazini, tena kazi maalum?

Hawa ndo wanafanya baadhi ya walimu wanakuwa chawa wao kwa sababu za kujipendekeza. Sidhani km wanajua impact ya walichofanya. Hivi ikitokea chama pinzani kikashinda uchaguzi sura zao wataziweka wapi na nafasi zao zitakuwaje.

Wamedhalilisha sn taaluma na profession yao. Watu wenye dhamana ya kuelimisha jamii lakini ndiyo wa kwanza kuonesha kuwa kichwani hakuna kitu. Ndo maana wanadharauliwa na jamii kwa mambo ya hovyohovyo km haya. Ila tusiwalaamu sn hawa wamezoea kujipendekeza, hata ukuu wao huupata kwa kujipendekeza na rushwa na wengine hadi hutafunwa na maboss wao ili wateuliwe. Hawa ni watu wa kuhurumia sn,
 
Muhusika angekubali hii bado no awamu ya tano na anafanyia kazi ilani ya chama ya 2020 na angeacha watendaji wale wale na kubadili mambo kidogo nakuhakikishia angeomba awamu ijayo wangemuonea huruma wakampa walau Kwa mhula mmoja,lakini kwakua kaifanya hii kama awamu ya kwanza ya kwake halafu Ile nyingine iwe kama ya pili ya kwake kaharibu,umepewa koti la kuazima lifue lirudishe uombe Tena sio unalifanya lako utagombana na mwenye nalo!!
Sina uhakika kama umesoma katiba walau mstari mmoja.

Samia hajajipa awamu hii kama awamu yake ya kwanza bali katiba inatamka wazi kwamba ikiwa Rais aliyepo madarakani chini ya miaka miwili tangu achaguliwe atafariki dunia, kuugua ugonjwa utakaofanya ashindwe kuendelea na majukumu yake ama sababu nyingine yoyote ya kumuondoa madarakani basi Makamu wa Rais ataapishwa kuwa Rais na atahesabika anatumikia awamu yake ya kwanza ya Urais.

Lakini endapo Rais angefariki madarakani akiwa amevuka zaidi ya miaka mitatu tangu achaguliwe basi Makamu wa Rais ataapishwa kumalizia kipindi kilichosalia na hatahesabika kama ni awamu mpya bali anamalizia awamu ya aliyefariki.

Magufuli alifariki ndani ya mwaka mmoja tu tangu alipochaguliwa kama Rais wa nchi kwa awamu ya pili.
 
Hivi hawa wavaa kaunda na magauni ya vitenge wakati wanachangishana hizo pesa waziri wao hakuwepo? Yeye ni profesa na ndo mlezi wao kwa nini hakuwakataza. Km na yeye kabariki ujinga na udhalilishaji huu wa taaluma ya ualimu naye tutakuwa na mashaka naye.
 
Bora hata walimu wa kike hawa wakiume utawakuta na naviatu yao mbele yamechongoka kama alibaba wanavitambi kama mapipa alafu kila saa yanasmile kama yamezhinda lottery hayo ndio mabumunda aisee yan daaah hayo ndio yakimwona tu hata RAS hayaishiwi tabasamu sa huwa sielew wanacheka cheka wanakuwa wanafurahia nini wakati wananyonywa kweli kweli
 
Ndio maana walimu wa Tz wanaonekana vituko kama watu wasiojielewa kwa ujinga wao.
 
Kujipendekeza hakujawahi kumuacha mtu salama.
 
Kazi kweli kweli Aisee..

Maslahi ya walimu bado yako duni sana na hii ndo wanachofanya
 
Back
Top Bottom