Kutengeneza familia yenye maadili,mwanaume kama baba kuwatengeneza watoto wake jinsi anavyotaka,hakuna malezi ya simu sijui video call muone mtoto wa MR II yule alizaa na Faiza unadhani akiwa aged 20 atakuwaje yule?kuishi kistaarabu ktk jamii ya wastaarabu (haiyumkiniki kila siku mwanaume aonekane ana mwanamke mpya huo siyo ustaarabu wa binadamu).
Kujilinda na maradhi mbalimbali hatari HIV,UTI na siku hizi nasikia ipo UTI sugu,kutunza kipato maana kila mwanamke ana gharama zake,kupata utulivu wa maisha na akili ya mwanaume kupanuka zaidi pindi akiwa na majukumu,sababu ni nyingi usichukulie ndoa kama vita mimi hapa mke wangu na familia wamesafiri nyumba naiona kubwa yote ni kwa sababu bila wao maisha yangu siyafurahii.