Wale Graduate mlioweza kujiajiri mlitumia mbinu (njia) kuweza kujiajiri?

Tanzania kuna kasumba. Nilivyomaliza form 6 kwenye 1990s, nilitaka kufanya kazi ya kupiga debe Dar. Basi nikawaona watu wote waliokuwa kwenye business ya aina hiyo niliokuwa nawafahamu. Unajua nini? Wote walinikatisha tamaa na kusema siiwezi kwa vile eti ni msomi. Kila niliyemomba kazi ya aina hiyo, alisema siyo kzi yangu. Mwishoe sikupata japo nilikuwa tayari kuifanya.
 
goood .nimefurahi sana kuona namna gani ulivyo na point
 
Alafu ukute wewe mwenyewe hujui hata mashamba yanafananaje...wewe jamaa umenichefua sana,kwa akili zako kilimo hakiitaji mtaji eti??
Unavyooongea kirahisi eti kuna mashamba ya bure....kwa hiyo wewe hata ukipita pale mikumi ukiyaona yale mapori,unadhani ni mashamba so akili yako inakutuma kuwa mtu yoyote akichukua tu jembe anaweza anza lima pale...akishalima akili yako inakutuma mbegu na mbolea huwa vinaokotwa tu or kugawiwa bure...alafu watu kama wewe ndo huwa mmekalia tu viti vya ofisi mlizoajiriwa kwa kujuana na kupeana na kina mjomba so unavyopigwa na kiyoyozi hapo unajiona mjanja ku comment ujinga kwenye post za watu wanaoumiza vichwa kutafuta namna gani wanatoka kimaisha
 
Umemjibu vizuri.
 
Nakumbuka ilikuwa 2017 mwezi wa 8...!!nilipostpone masomo baada ya kuona kuna kila dalili ya kurudi mtaani nikiwa sina kitu
Kumbuka hapo nilibakiwa na boom 1 tuuu

Nilichokifanya ni kununua diary...nkaandika business za kufanya nkiacha chuo

Kila biashara ilinicost kwenye kodi...coz nakumbuka boom ilibaki 520k

So nikakumbuka kuna frem pale hom waliitelekeza baada ya kushindwa biashara

Nikawapanga ndugu...nkampanga mzazi...nae akakubali(hapo hajui kama nmeacha chuo)

Nikaandika barua ya kuahirisha masomo
Nikauza vitu vyangu
Nkapanda ndinga kurudi town dsm

Kwenye gari nilitumia mda mwingi kuandika tactics za kuikuza biashara

Nikaingia kazini
Japo mtaji ulikuwa mdogo lakini nilijitahidi kuukuza kwa kuacha faida pia ijizungushe
Nilijinyima vingi mpk girlfriend aliniacha

Nikajitahidi kujifunza kwa wauza maduka wengine hapa jf na pia google

Taratibu mambo yameanza kunyooka
Nimepanga chumba
Vitu ndan vipo japo co vingi
Nakula nnchotaka
Na juzi BIKO wameniongezea mil.10

Kikubwa ni kuweka malengo..ukiweka anasa pemben na ukpambana...Mungu atakulipa
 
hongera mzee, naamini tunaishi kwenye simulation kama the matrix, yani kila mtu ana ramani yake ambayo the great architect "God" ameshamchorea, ndio maana unakuta mtu kasoma wee hadi doctrate af anaishia kuimba mziki, big up mzee for responding that call since it was already decided as its said "you're not here to make a choice, but to understand why you made it"
 
Ndo maana naamini yawezekana ilipangwa nifanikiwe kupitia biashara na co ajira...!!Mungu atujalie sote tufike tunapotaka...!!
 
Duuh kumbe biko ni kweli aisee hongera sanaaa
 
kwa akili zako kilimo hakiitaji mtaji eti??
Mtaji unao tayari....nguvu na elimu yako.
akishalima akili yako inakutuma mbegu na mbolea huwa vinaokotwa tu or kugawiwa bure...
Acha kutafuta visingizio visivyo na mashiko. Mbegu shilingi ngapi? Acha kujificha kwenye changamoto, tumia elimu yako kuzitafutia ufumbuzi.
.
Unauliza kuhusu mbolea???
Zunguka kwa wafugaji omba samadi mwaga shambani kwako.
 
Pesa ya mbegu
Pesa ya nauri na mizungoko yote
Pesa ya jembe
Pesa ya kusafirisha mazao
Pesa ya kula
Pesa ya madawa
Pesa ya malazi
Pesa ya
Pesa ya

Hacheni story zenu nyinyi mlivyopewa pesa na wazazi wenu munaongea tu.
 
Acha kuandika ujinga angalau itakusaidia kuficha upuuzi wako...kumbe unajua mbegu hazigawiwi bure...na hayo mashamba unafikiri yanagawiwa bure??or kwa akili zako ukisafiri na gari ukiviona vichaka huwa akili zako zinakutuma yale ni mashamba mtu yoyote anaweza chukua jembe na kuanza kulima...alafu mbolea unadai eti nizunguke kwa wafugaji nichukue samadi,kwa hiyo unadhani wakulima wanavyolalamikaga na kuiomba serikali iwapelekee mbolea wote ni wajinga na wavivu...we jamaa ni mjinga sana na hujui hata shamba linafananaje...icho kikazi ulichonacho najua kinakupa kiburi na kutuona sisi tunaohangaika hatuna akili...sawa mjanja wewe mimi nakuombea upoteze iyo kazi inayokupa kiburi uje huku mtaani tuangaike wote tukuone wewe mjanja mwenye akili unayeweza kuvamia milima na vichaka ukavigeuza mashamba na ukatumia samadi tu kulima...KARMA is watching you...vitu vingine acha kuleta ujuaji...we endelea kupigwa na kiyoyozi hapo ofisini kwenu
 
This z my dream. Ofisi yangu ya pili itakuwa hii au duka la simu na vifaa vyake
 
vp stationary ina faida nzuri? yaan return yake ikoje per day?
 
Well,

Vipi kwa sasa hauendelei na hiyo biashara mkuu?
Lengo nipate information,
Nina lengo la kufungua hiyo biashara maeneo ya chuoni (preferably UDSM_Mabibo Hostel).
Well, kwa sasa nimesitisha biashara hiyo kutokana na kutokuwa karibu na eneo la tukio na kiukweli napata wakati mgumu sana kumuamini mtu anifanyie biashara kama nilivokuwa nimewazoesha wateja wangu. but nina plan ya kuiendeleza kama nitapata mtu amabye atakuwa tayari kujifunza kazi kutoka kwangu na aifanye kama nilivyokuwa nikifanya mimi.
Kama lengo lako ni kufanya biashara ya Stationery tena maeneo ya chuo, unapaswa kutambua kuwa wateja wako wengi (karibia wote) ni wanafunzi, na wanafunzi wengi huwa rational, so utapaswa kujua ni bei gani utoe copy na bei gani ufanye printing.
Pia utapaswa kujua u-base kwenye hudama zipi na zipi i.e. unaweza ku-base kwenye kutoa huduma pekee au ukaweka na bidhaa pia.
 
Well,

Vipi kwa sasa hauendelei na hiyo biashara mkuu?
Lengo nipate information,
Nina lengo la kufungua hiyo biashara maeneo ya chuoni (preferably UDSM_Mabibo Hostel).
Stationary wai kufungua udom ujasi hutojuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…