Nilipoamua kufanya biashara niliamua kufanya yenye risk ndogo kwasababu mtaji niliokuwa nao ni mdogo na wakuungaunga alafu sikuwa na muda wakusimamia mtaji around 700,000/= sikutaka kupoteza pesa nikafungua Video Library imekaa miezi 4 sijaambulia hata Tsh 100/= kipande ya faida nilimpa mshkaji wangu asimamie kilakitu yeye mzoefu na biashara hiyo kwenye biashara alikaa dogo basi miezi 4 sijapata hata 100/= ya kununua pipi kifua, Biashara ilikuwa ndio ipo kwenye scratch na dogo anazingua eti hakuna biashara anarudisha ufunguo ukweli biashara ilikuwa ngumu kwasababu ya competition hapo nilipo kulia kuna nyengine nyuma ndanindani kuna nyengine nyuma tena mbali kidogo kuna balabala zipo nyingi mbaya zaidi nilivyofungua tu biashara jamaa wengine wakafungua pembeni yangu hatua 15 tu za miguu alafu jamaa wana mtaji na frem mzuri kuona hali tete nikaamua niuze biashara au vitu vyote nikawa nauza kwa pressure maana nipo chuo sina pesa yaani Boom limekata nilikuwa tayari kuuza mpaka kwa 150,000/= njaa isikie tu, kuna wateja wa 350,000/= wakawa wanapiga karenda nikaona huu ujinga nawapa Golden chance mimi nimetumia 800,000/= nawapa hadi kwa 300,000/= wanajivuta nikafikiria changamoto niliyonayo pesa ya kula sina nilipo nikamwambia jamaangu ninahitaji kama 40,000/= itaweza ni push mpaka narudi Home tufungue tena sehemu nyengine akaweka bondi Computer akanitumia 40,000/= nikaishi mpaka nikarudi.
Nilivyorudi nikasaka location nzuri tukasema tuiweke hapa nilivyopata pesa nikaiweka, wakati naiweka kuna majaamaa nao hatua 10 nyingi wameweka yao yaani kwenye nyumba Hiyohiyo mimi nimechukua frem wao wamejenga kibanda nikasema hawa watakimbia wenyewe[emoji23] [emoji23] tumeanza biashara mwezi ujaisha Computer imeungua jamaa zangu wakakopa sijui wapi wakapush mpaka wakalipa, [emoji23] [emoji23] muda nao ujapita wahuni wakapita usiku wameiba fremu za mtaa mzima kwangu waliiba sabufa mwenzangu mbele mtaa uwouwo wakamkombea Computer, Sabufa, Kobe nk jamaa akafunga biashara [emoji23] wahuni sio watu basi ukizingatia biashara ndio tunaisimamisha then assert zake kubwa zinaungua na kuibiwa sikupata faida miezi kama 4 tena ila nilikuwa napata elfu kumikumi kidogo tofauti namwanzo Yule wa karibu yangu nae alikimbia mapema tu maana sisi tulikuwa tunapiga kazi sio ya kusikilizia aliishiwa upepo mapema tu akaja kubeba kibanda chake basi changamoto nyingi zimeenda zimerudi wee ila PATIENT ndio msingi mkuu sasahivi sijawa millionaire ila atleast napata pocket money hazikauki mfukoni, simuombi mtu pesa ya bando, ya chai sasahivi nimesafiri uku pesa inangia tu biashara inanirisha mpaka huku mbali market tumeikamata wateja hadi raha jumatatu ndio usiseme wanajaa ndani kama pantoni siku zinavyozidi kwenda Circle ya faida na payroll inazidi kukuwa.
Najivunia ni Biashara niliisimamisha mwenyewe kimtaji mpaka leo bila kusaidiwa na mtu hata Sh 10 licha ya changamoto zote ila kinachofanikisha mpaka leo GOOD TEAM watu ninaofanya nao kazi wamejitoa imagine Computer imeungua wamingia Risk wenyewe kukopa na kulipa wamehaso mpaka kukopeshwa sio msoto wa hapa na pale, Sabufa wameiba wameazima wanapush.
Toka nimefungua hii Biashara mpaka leo ipo ni wenzangu wanne (4) wamefunga ila mie bado ipo.
Nimejifunza
1)Patient, ndio msingi kwenye biashara bila patient hii ingekuwa ishafeli muda mrefu sana.
2)Good Team, biashara huwezifanya mwenyewe hata sikumoja ila ukifanya nawatu wawe watu wenye kujitoa na maono iyo fortune itafika mbali.
3)Mtaji, hii kitu inatesa sana sie kajamba nani.
Kingine, kwenye biashara inabidi uwe na mahesabu mimi naamini kwenye biashara ya ofisi yaani iliyokuwa na ofisi endapo una mtaji mdogo na huna muda Risk inapungua mfano umeajiriwa una mtaji mdogo 1000,000/= ukifanya biashara zisizo na ofisi kama kilimo, kuuza mazao kuna asilimia kubwa ya kuchoma pesa kuliko ukiweka kwenye ofisi kama ukifungua Juice Point ya miwa, Uwakala, Carwash....nilivyokuwa na 700,000/= mwenzangu nae alikuwa na 800,000/= akafanya kilimo kaichoma hata mwezi ujaisha ila mie mpaka leo bado inanizalishia 700,000/= yangu.