Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Harusi nayo ilikuwa gharama kubwa, we acha tu !!! Nafuu ungekaa nae kama mchumba kwa mda mrefu ili ugundue tabia zake.
 
Sawa Nkamu....kama unatingwa Nkamu atafutwe tu mdada[emoji3]

Maana mimi ni yule mama wa Kinyakyusa nimekuja namkuta mwanangu anaosha vyombo halafu mke umekaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]patachimbika
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nitaandamwa ukoo mzima[emoji16][emoji23].


Japo kusaidiwa kazi na housegirl hainogi...inanoga na mume[emoji2960]
 
Hivi kwanza mnaoa ili iweje..??
Kuna sababu kadhaa za kwanini watu wanaoa au kuolewa..

1. Kuzaliana (Procreation). Japo saivi watu wengi wanazaliana bila ndoa, lakini bado kuna watu walioshika dini na tamaduni zao za kimaadili zinazowanyima kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi bila Ndoa. Kwaiyo ili azaliane lazima awe kwenye ndoa kwanza.

2. Kuepuka Upweke (Emotional Security). Sio watu wote wanaweza kupambana na solitude. Kwaiyo kuna watu hawawezi kuishi peke yao kabisa na ni lazima wawe kwenye mahusiano. Hapa ndio zinatokea zile ndoa za makosa. Ile mtu kaolewa/kaoa ili tu awe au aonekane na yeye yuko kwenye ndoa.

3. Kujiongezea Kipato. Wengine ndoa kwao ni kama fursa ya kiuchumi, akipiga mahesabu yeye anaingiza labda laki 5 kwa mwezi, akioana na mkulungwa anayeingiza kama Milioni kwa mwezi hivi kuna namna atasaidiwa gharama za maisha na yeye atabakiwa na mzigo mwingi wa kusave na kufanya mambo mengine. Hii pia ndio inapelekea wazazi wenye uwezo kifedha kukataa watoto wao kuoa au kuolewa na mtu ambaye anayumba kiuchumi.

4. Kupata mtu wa kukufariji kwa ukaribu hasa ukiwa unapitia kipindi kigumu kama kuugua. Maana hata watoto wako wanaweza wasiwepo karibu wakati unaumwa kwaiyo kama una mume au mke ni rahisi kusaidiwa kwa haraka.

Sababu nyingine ambayo naiona binafsi, ni kwamba unapoishi na mtu mwingine muda mrefu unapata nafasi ya kujijua undani wako vizuri. Yani unaanza kujiona wewe ni mtu wa aina gani, kama ni mtu wa makasiriko kwenye vitu vidogo, au sio mwaminifu au ni mtu wa kudharau vitu na kuchukulia poa mambo ya mwenzako au ni mbinafsi au ni mtu mwenye wivu sana. Nasema hivi kwa sababu ukiwa unaishi peke yako ina maana mara nyingi utakua una interact na watu wengine ndani ya comfort zone. Kwaiyo kuna namna unaji behave na kuficha makucha yako involuntary. Lakini ukiwa kwenye ndoa, kila tabia uliyokua unaficha hadharani, lazima ionekane tu. Kwaiyo ndoa inakusaidia pia kujua zaidi weakness zako na inakua rahisi kuzifanyia kazi ili uwe a better person.


Kama nikitakiwa kukushauri aidha uwe kwenye ndoa au usiwe kwenye ndoa. Binafsi, nitakushauri uwe kwenye ndoa, ila tu ukijiona mwenyewe uko tayari, na sio kwa kulazimishwa na mtu. Kuhusu suala la utajuaje kuwa uliyemuoa/aliyekuoa ni mtu sahihi kwako au lah, hapa nasikitika kukwambia kuwa utakuja kugundua baadae kadri unavyoishi naye (Wale wa Mke Mwema Anatoka kwa Bwana Naheshimu Pia Mawazo Yenu). Kwa sababu maisha mtakua mnaya-face pamoja, usjali kuna matatizo yakikukuta utajua tu kama uliotea embe dodo chini ya mnazi au uliuziwa mbuzi kwenye gunia. But all in all, we live for experience not for perfection!

Kila la Kheri [emoji1479]
 
Mlizungumza jinsi ya kulea familia na mgawanyiko wa majuku kabla ya ndoa. Sababu u-busy wake haukuanza ndani ya ndoa.

Ndoa nyingi zina feli sababu watu wanashindwa kuwa na mazungumzo muhimu kabla ya ndoa.
Sahihi mkuu,ujue muundo wanamna yakuendesha hyo ndoa ,mlitakiwa kuujua mapema kabisa either kwamazungumzo rasimi au kuona Tu niaiana gani yamtu unaenda kuingia nae Katika ndoa,ukweli ningumu kwamwanamke mhangaikaji/au mwajiriwa anaeweza kuleta kipato home,atekeleze majukumu yaleyale kama wifemaid ningumu,mno,nikweli mwanamke aliyehome Tu masaa24,kufanya inshu zahapanapale nikawaida
 
Kumbadilisha mtu mzima Ni kazi na swez kupoteza mda kufanya hvo.
Kwa nn nilazimishe kukaa na mtu ambae naona chemistry zinakataa.
Naomba mwenye deep education kuhusu chemistry ktk mapenzi au mahusiano inamaana gani haswa,naje nikweli chemistry inamatter Sana ktk mahusiano yakimapenzi au ndoa??msaada wanajamvi wenzangu,nnateseka nahili
 
Ila alikuja kuzidi mahali ndio maana ndio ikawashinda kwa uzoefu wangu wanaume wanaoendelezewa kielimu au kibiashara ndoa zao hufa, a moment mke akipata kazi au hela humuona mume si chochote
Ms cariha hebu tuelezee kidogo kwann hii hutokea maranyingi,why ndoa Hufa as mwanamke anapoendelezwa either kibiashara/kielimu nammewe,kuna mifano halisia Sana kwawatu wetu,
 
Pole sana kwa yaliyoikukuta mkuu. Kiukweli ni changamoto sana kuishi na mwanamke mwenye kiburi na dharau.

Ila mkuu nawewe usingemshauri akasomee uanasheria kwa mustakabali wa ndoa yenu. Unaoaje mwanamke mwanasheria labda muwe kada moja ila kama ni tofauti hao watu ni much know sana.

Kwa ambae hujaoa nakushauri usioe kwani hakuna faida yoyote ya ndoa.
Duuu,mbona mnatutisha mkuu,watoto utaleaje pekeyako mkuu,mfano unawatoto wakike utawafundishaje,juu Yamaisha Yao
 
Ms cariha hebu tuelezee kidogo kwann hii hutokea maranyingi,why ndoa Hufa as mwanamke anapoendelezwa either kibiashara/kielimu nammewe,kuna mifano halisia Sana kwawatu wetu,
Mara nyingi sana honestly mtu akiwa na shida ana fake uhalisia na kujifanya mwema na upendo Ili atimiziwe haja yake ya kifeza na kimwili, na anakuwa pale kwa ajili ya shida na sio upendo wa kweli so akipata alichokitaka ndio huanza kuonyesha true color zake na wewe kukuona sio hadhi yake na mshamba, so ni vizuri kwa kweli mpendane kila mtu akiwa na kipato chake hapo ndio mtajua ana upendo wa kweli na sio kufata fedha au unafuu, ni heri ukutane na mtu yuko vizuri na hela zake na utamjua tabia yake kuliko maskini wa kipato na akili akipata fedha kwanza anakuwa limbukeni na hashikiki, kiukweli hii tabia ya kujifanya wapenda maskini eti umwendeleze lazima siku moja ulie
 
Hapo kwenye bond na chemistry nmepaelewa aisee...unaweza kuwa na demu mkali had washkaj wanakuonea wivu ila ukawa huna bond nae na chemistry hakuna..ila ukawa na demu wa kawaida tu ila mka connect vibaya mno...yameshanitokea haya mambo
Naendelea kusisitiza kuomba elimu juu ya chemistry nisifa zipi zinafanya muwe machemistry inafanana,nakwann nikitu muhimu mno ktk maisha yamahusiano
 
Naomba kutambua MTU mwenye inferiority complex anakua nadalili zipi mkuu,au sifazipi
Someone who is insecure in every thing, hana jema yeye ni malaika anakosewa yeye tu, pia anaji feel less a man Kwa vile mwanamke ana vitu flani flani kiasi hata wakitofautiana yeye anaona mkewe kamdharau kisa kamzidi vitu flani, kumbe kutofautiana kupo tu, au wengine wanaamini forinstance mkewe kumfulia kwa mikono instead ya machine anaona ni dharau flani.
 
Back
Top Bottom