Hivi kwanza mnaoa ili iweje..??
Kuna sababu kadhaa za kwanini watu wanaoa au kuolewa..
1. Kuzaliana (Procreation). Japo saivi watu wengi wanazaliana bila ndoa, lakini bado kuna watu walioshika dini na tamaduni zao za kimaadili zinazowanyima kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi bila Ndoa. Kwaiyo ili azaliane lazima awe kwenye ndoa kwanza.
2. Kuepuka Upweke (Emotional Security). Sio watu wote wanaweza kupambana na solitude. Kwaiyo kuna watu hawawezi kuishi peke yao kabisa na ni lazima wawe kwenye mahusiano. Hapa ndio zinatokea zile ndoa za makosa. Ile mtu kaolewa/kaoa ili tu awe au aonekane na yeye yuko kwenye ndoa.
3. Kujiongezea Kipato. Wengine ndoa kwao ni kama fursa ya kiuchumi, akipiga mahesabu yeye anaingiza labda laki 5 kwa mwezi, akioana na mkulungwa anayeingiza kama Milioni kwa mwezi hivi kuna namna atasaidiwa gharama za maisha na yeye atabakiwa na mzigo mwingi wa kusave na kufanya mambo mengine. Hii pia ndio inapelekea wazazi wenye uwezo kifedha kukataa watoto wao kuoa au kuolewa na mtu ambaye anayumba kiuchumi.
4. Kupata mtu wa kukufariji kwa ukaribu hasa ukiwa unapitia kipindi kigumu kama kuugua. Maana hata watoto wako wanaweza wasiwepo karibu wakati unaumwa kwaiyo kama una mume au mke ni rahisi kusaidiwa kwa haraka.
Sababu nyingine ambayo naiona binafsi, ni kwamba unapoishi na mtu mwingine muda mrefu unapata nafasi ya kujijua undani wako vizuri. Yani unaanza kujiona wewe ni mtu wa aina gani, kama ni mtu wa makasiriko kwenye vitu vidogo, au sio mwaminifu au ni mtu wa kudharau vitu na kuchukulia poa mambo ya mwenzako au ni mbinafsi au ni mtu mwenye wivu sana. Nasema hivi kwa sababu ukiwa unaishi peke yako ina maana mara nyingi utakua una interact na watu wengine ndani ya comfort zone. Kwaiyo kuna namna unaji behave na kuficha makucha yako involuntary. Lakini ukiwa kwenye ndoa, kila tabia uliyokua unaficha hadharani, lazima ionekane tu. Kwaiyo ndoa inakusaidia pia kujua zaidi weakness zako na inakua rahisi kuzifanyia kazi ili uwe a better person.
Kama nikitakiwa kukushauri aidha uwe kwenye ndoa au usiwe kwenye ndoa. Binafsi, nitakushauri uwe kwenye ndoa, ila tu ukijiona mwenyewe uko tayari, na sio kwa kulazimishwa na mtu. Kuhusu suala la utajuaje kuwa uliyemuoa/aliyekuoa ni mtu sahihi kwako au lah, hapa nasikitika kukwambia kuwa utakuja kugundua baadae kadri unavyoishi naye (
Wale wa Mke Mwema Anatoka kwa Bwana Naheshimu Pia Mawazo Yenu). Kwa sababu maisha mtakua mnaya-face pamoja, usjali kuna matatizo yakikukuta utajua tu kama uliotea embe dodo chini ya mnazi au uliuziwa mbuzi kwenye gunia. But all in all, we live for experience not for perfection!
Kila la Kheri [emoji1479]