Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Kuna wanaume mnajitambua asee
 
Jamaa anamaindi hajawekewa maji ya kuoga na mke mwenye dili zake za biashara. 😃
Upuuzi tu na kuiga wazee wa zamani.

Kuwekewa maji ya kuoga sio vibaya ila vibaya ni kulalamika endapo mtu hujawekewa maji ya kuoga.

Mimi upuuzi huu kwwngu siutaki.
Upuuzi wa kuwekewa maji ya kuoga.
Upuuzi wa kuagiza maji ya kunywa wakati mwenyewe naweza kwenda kuchukua hizi ni puuzi za kuachwa tu hazifai katika jamii ya kitanzania.

Maji ya kuoga unatakiwa uweke mwenyewe chooni.
 
Pole mzee ila mi ndo si semi kilichonikuta ni balaa mke ni janga, mkosi nuksi na kila taka taka
 
Tatizo watu wanataka mteremko wa kusaidiwa majukumu, mteremko wa kupikiwa, mteremko wa kupasiwa, mteremko wa kuandaliwa maji ya kuoga. Mteremko wa papuchi. HAIWEZEKANI.

Chagua ufanye majukumu yako 100% kama mwanaume, yaani utoe huduma zote za familia au mshirikiane majukumu upoteze kuhudumiwa kama mfalme.
 
Ahaaahaahaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23]

Sasa si uliteseka na maugwadu yako till morning [emoji1787]
 
Kwahiyo sisi ndiyo tuliumbiwa kuteseka eeh, kamume kenyewe kamekaa sebuleni tu kameshika remote, mama anapalangana na masufuria jikoni, bado na kuoga upelekwe,akii wewe utatulisha kwa jasho humo ndani yaani utalipa kila bills sitoi mimi chochote na siku nikitoa pesa nakuandika kwenye kitabu cha madeni cha familia utanirefund tu.😂 si wataka kuwa kichwa cha familia eeh sawa sisi mikia tutakudekeza baba.ila utalipia hadi chumvi.🏃‍♀️
 
Inawezekana ukawa sahihi kulingana na maoni yako.....
Hapa tunajadili hoja hatujadili maoni.

Maoni kila mtu anayo ila hoja ndani ya maoni hayo ndicho kitu cha msingi.

Pinga kwa hoja usiishie kusema maoni yangu na kufanya hiyo ni hoja ya kujitetea kwako.

Huu ujinga wa kumrundikia mwwnamke mikazi haukubaliki katu.
 
Haina shida endapo ww unafanya sehemu yako kwa asilimia zote. Leta chakula, somesha watoto, mpe mke pesa ya matumizi, hakikisha malazi, Afya na mavazi ni ya uhakika kisha muulize mkeo kwann hakuna maji ya kuoga bafuni.
 
Inawezekana ukawa sahihi kulingana na maoni yako.....
Hapa tunajadili hoja hatujadili maoni.

Maoni kila mtu anayo ila hoja ndani ya maoni hayo ndicho kitu cha msingi.

Pinga kwa hoja usiishie kusema maoni yangu na kufanya hiyo ni hoja ya kujitetea kwako.

Huu ujinga wa kumrundikia mwwnamke mikazi haukubaliki katu.
 
Mlizungumza jinsi ya kulea familia na mgawanyiko wa majuku kabla ya ndoa. Sababu u-busy wake haukuanza ndani ya ndoa.

Ndoa nyingi zina feli sababu watu wanashindwa kuwa na mazungumzo muhimu kabla ya ndoa.
 
Huyo mke ana akili Kama za mahouse girl ninaokutanaga nao mie, Sasa hivi tumeamua sisi wenyewe na watoto wetu tukamate majukumu ya housegirl na tukibanwa sana tutafute mtu anakuja kufanya usafi hiyo siku Mara moja moja Basi kesi inaisha.
Sijajua connection kubwa Kati ya housegirl na ujinga aisee, au sie tunagundu nao? Wengi wao hawajielewi na ukiwaelekeza wanaona wanaonewa na kuteswa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo uzezeta wake hukuona mwanzoni? Au ndip ulisema atabadilika ndani ya ndoa.

Huwa tuna ignore red flags kwenye mahusiano ya awali
 
Huyo mwanamke anafanana sifa na mahousegirl wengi tunaokutana nao...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa ndugu nimekubaliana na wewe....
 
Wapi na nani kasema kwamba ni lazima mke akuwekee maji ya kuoga mkuu ?

Ni sahihi mkeo anayepata kila kitu kutoka kwako kukuhudumia hata kukuogesha ikimpendeza. As long as anapata kila kitu kutoka kwako na yeye akili yake ipo kwa ajili yako akikusubiri urudi akufurahishe.

Tatizo linakuja mwanamume kuacha majukumu akitegemea mwanamke azibe pengo huku akitimiza majukumu yake kwa mume kwa 100%
 
Kuna wanaume mnajitambua asee
Tujaribu kuvaa uhusika wa wanawake tutaona ugumu wanaopata.

Au wanaume tujifunze kuwasaidia kazi wake zetu tunaweza angalau kuona ugumu wa kazi hizo.

Mimi nakumbuka wakati wife analea mtoto wetu mchanga hatukuwa na binti wa kazi nilikuwa naamka saa kumi kasoro nakosha vyombo,nafua nguo,nadeki,nasafisha jiko,napika chai,natia maji chooni ya kutumia then saa mbili nakoga naenda kwenye ishu zangu,yeye wife anabaki anapambana na mtoto.

Tulikiiishi kipindi hiko bila binti wa kazi,lakini hizo kazi zote ningemuachia mzigo ungezidi kuwa mzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…