Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Hayo umetaja ni mambo madogo dogo sana mtu kushindwa kufanya, ingawaje kama unasikia kiu ya maji ukiyafuata kunywa mwenyewe unapungukiwa nini? au kupakua chakula kitu gani kinakushinda kufanya hivyo? Mimi nasema kazi zile kubwa kubwa za kusema usifuliwe au kupikiwa chakula na house maid wakati mke nae anachangia pato la familia.
 
Mama ya misimamo yake...
Ila mwanaume wako lazima awe muelewa sana ukiwapata hawa waliopo sokoni mda wote Hahaha lazima talaka iandikwe
 
Jukumu lako la msingi ni kufanya kazi za nyumbani na malezi kwa ujumla... Whatever you do, hakikisha jukumu hili unalitimiza at the expense of other issues.
Mume kama wewe na mke wa kipindi hiki hiyo nyumba ligi zisingeisha. ndio maana ndoa za sasa hivi talaka mwaka hauishi sababu wanawake wameamka na wao wanajua haki zao.
 
Duuuh Mungu aniepushe na mwanamke wa aina hii, kwa hiyo mmeo hana shukrani, ila sidhani kama umeolewa
 
Hahahahahah kweli kila mtu na mtuwe bila shaka ulipokuwa mdogo wakati mama yako anakutuma kila wakati ulikuwa unalalamika kwanini anakutuma tuma pamoja na kukunja sura!

Tuna changamoto sana ya malezi kama vijana tunaoingia umri wa kuwa washua. Ifikie wakati mujue kwamba kazi mnazofanya haziwaondolei hali ya kuwa wake!

Trust me hata uwe katibu mkuu UN uko still utagonwa na utazaa na utanyonyesha vile vile! Nafikiri kwa akili zenu za sikuhizi wale wazee waliokuwa wanahimiza msipelekwe shule walikuwa na mantiki sana sahizi ndo tunawaelewa vyema sasa. Mwanamke ukimuwezesha anazidi kuwa mjinga kuliko akiwa na utashi tu wa kawaida!

Feminist wengi walikuwa wanazikwa na huu mfumo tofauti na leo wana mapembe na wanaendelea kuharibu wenzao.
 
Wanaume tunapotea kwa kasi sana. Na twanamke tulivyotujanja hawa wanaume mabwege tunawasifia kuwa majentlomen... Basi ubwege ndiyo unajaa. Haha...
Eeh jamaa anaitwa jentomen anachekelea halafu upande wa pili mwanaume jeuri na mbabe anamchapia uwa lake kila akisafiri😅
 
Mume kama wewe na mke wa kipindi hiki hiyo nyumba ligi zisingeisha. ndio maana ndoa za sasa hivi talaka mwaka hauishi sababu wanawake wameamka na wao wanajua haki zao.
Kuna wanawake wengi tu wanaojitambua na kutimiza majukumu yao kama mke na mama. Isipokuwa feminists wachache ndiyo hawa wanaongezea kundi la single mothers kwenye jamii.
 
Yani mwanaume asiwe anaenda kutafta hela atakuwa na mApepo huyo, wengine watafta hela yeye yuko nyumbani kufanya kazi za house girl si mwendawazimu huyo
Sindio hawa mnaitaga majentromenz 😅 wanawa care sana yani!
 
Labda hiyo type unayo izungumzia ww ndiyo unayo kutana nayo, ila wanaume wanaotimiza majukumu yao kuanzia kwenye kulipa mahali mpaka kutumiza majukumu yao ndani ya familia wapo wengi tu.

Tatizo wengi wao hawa wataki wabeijing na wanawake wanaotaka mashindano kama nyinyi. Mnawapata hao wanaopenda kulelewa na kwapa hela ya mahali wakawalipie, ili muwaendeshe.
 
Mume kama wewe na mke wa kipindi hiki hiyo nyumba ligi zisingeisha. ndio maana ndoa za sasa hivi talaka mwaka hauishi sababu wanawake wameamka na wao wanajua haki zao.
Sasa haki ipi ambayo inaruhusu wewe kukwepa majukumu yako kama mama wa familia 😅 mbona mnajiaibisha nyie!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…