reymage
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 12,203
- 28,789
Woiiiii!Haloooooo
Piga kelele kwa rey akeeee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Woiiiii!Haloooooo
Piga kelele kwa rey akeeee
😅😅😅😅😅😅 nilishawahi andika makala humu! Hizi ndoa za watu kukutaniaga KFC na lodge tu eti ni wachumba huwa zina matatizo sana😅Ila kukaa na mtu muda mrefu kabla hamjaamua kuishi inasaidia sana.
Kua na mtu kwenye uhusiano angalau miaka 4, miwili ya uchumba ndiyo uoe kama mtu miyeyusho pale pale kwenye uhusiano unamjua unakaa kushoto.
Bro wangu alilia mara ya kwanza na sasa hivi analia tena, muda wote huu mi nipo na mmoja huyo ndiyo namchunguza.
Haha... Ni kazi ya nani sasa?Wakuu tuelewane kufua,kupika,usafi wa nyumba sio kazi ya mkeo jamani ,kazi ya mkeo kukuzalia watoto nankufanya mapenzi na wewe kazi zingine apate msaidizi pia lakin isiwe kama sheria
Duh pole mkuu Mungu pekee ndio mwenye kutetea ndoa yako.NGOMEKONGWE2021 - Tupo wengi, kiongozi. Mie pia watoto 4 kama wewe. Miaka 12 ya ndoa. Mama wa nyumbani. Tatizo hawezi kujifunza kitu.
Kila siku ni shida tupu ndani ya nyumba. Mfano, hawezi kutoa magamba ya samaki yakaisha yote kabla ya kumpika samaki. Chakula anavyonunua kwenye supermarket, ndivyo navyokipika!
Anaweza kupika nyama ya kuku na kinyeo chake ama bado kuna kiasi fulani cha vinyoya!! Hata nikimweleza vipi, akili yake haishiki!! Hataki niwafundishe watoto. Nikiwakosoa watoto kwa namna ya kuwafundisha, anakuja juu.
Watoto wananiona mimi shetani na yeye malaika. Amejenga chuki kati yangu na watoto ambao bado ni wadogo tu. Sijawahi kumpiga ama kuchepuka lakini nilikwisha mwambia kuwa tungekuwa tunaoa mara ya 2, nisingemuoa tena. Sina hamu tena hata ya kulala naye.
Hata kumkunjia mumeo nguo zilizo andaliwa na beki tatu ni ngumu pia?Hapana mkuu huyo dada yupo sahihi kabisa,hili jambo haliwezekani kwa wanawake wengi.
Kwa wanaoweza acha wafanye,kwa ambao wanashindwa wasibezwe kwa sababu ni kweli na wao wanachoka.
Imagine mke mwalimu anarudi labda saa tisa kazini,akifika nyumbani kachoka hapo aanze kufua,kupika,kuosha vyombo huku wewe baba kama baba au mume umetulia kwenye sofa unachati jamii forum ukiwa na soksi miguuni zenye vitobo vimetafunwa na panya unasubiri kula.
Hii haikubaliki,nenda kamsaidie mkeo kazi kwa sababu wote mumetoka kazini.
Wanaume wengi wakitz bado tuna umwinyi sana na upuuzi flani ambao hauna maana yeyote,kwanza hizo kazi sio lazima kwa mwanamke kufanya kijamii tu ndio kwa kuwa wanawake wengi ni watu wa nyumbani ndio imeonekana ni kazi zao.
Walijichanganya sana, mwanamke akishakuwa mbishi mbishi tu ni red flag😅Haha... Unakuwa hautofautiani na wasiooa, zaidi unawazidi stress tu. Na hii ndiyo sababu wengi waliooa hawa feminists wanatamani kutoka kwenye ndoa.
kwani baba yake analala nae? yani ufananishe status ya baba na mume mbona jua na mweziHilo ndo huwa nashangaa kwamba baba yake akimtuma ni sawa ila mumewe akimtuma anamuwekea ligi?
Ni changamoto za malezi nafikiri hizi na matokeo yake ndio haya hapo!
Mume akitoa order ni lazma itekelezwe bila kelele matatizo ya kuwa na mwanamke argumentative kwenye kila kitu ndio inakuja kuharibu watoto
Hongera sana kulelewa hvyo ...na omba Mungu umpate wa kufanana nae!hawa wa kwetu wako tofauti na wenyewe tunaona kawaida tu..Mbona kwetu wanaume hufanya mambo mengi including cooking na hata kujifanyia mambo mengi na haijawahi kuwapunguzia uanaume wao ndani, I grow to see my aunties, ba mdogo wanafanya vitu common kabisa ambacho huku JF naona mwanaume analalamika Hadi kuvunja ndoa yake kabisa, Mimi babangu kupika sio issue hata kaka zangu na haijawahi kuwapunguzia uanaume wao so it's just a matter of perspective kwa dunia ya Sasa watu watavunja sana ndoa zao ka wanaamini kuto kumsaidia mke kazi hata akiwa kachoka kazini ndio uanauke Bora au uanaume Bora, basi before marriage tafta mwanamke anayeendana na wewe, huwezi acha kazi zako na kutimiza ndoto ukiwa wampikia mume, sijui unapinda mgongo woooi, that's why nasema watu tumetoka different backgrounds unayemuoa make sure atafanya utakavyo, na ndio naona huyu mleta mada angetakiwa aoe mke wa kijijini wa darasa la saba Ili awe mama wa nyumbani afanye hayo yote
Nani hapo ni inferior: mwanamke ambaye hataki kutimiza majukumu yake akihisi ataonekana inferior - ananyanyaswa au utumwa - ama mwanaume anayemtaka mwanamke atimize majukumu yake ipasavyo?Kwa sababu wanaume mumeaminishwa kuwa kuzidiwa vitu na mwanamke ni kosa na Hilo ndio tatizo lilipoanza
Hakuna mwanamke asiyependa kumdekeza mumewe apatapo nafasi, ila inategemea kwa mama mfanyakazi kama atapata muda jioni ni vizuri kupika na kumtengea mume ila ikitokea amechelewa kurudi labda , mume amuelewe na asicomplicate maisha kama dada yupo basi atasaidia kupika, ila mimi sitopenda dada amsevia mume wangu chakula ntajitahidi nimsevie mwenyewe ama ajisevie mwenyewe.
Ila on weekends kupika ni lazima mama mjengo nioneshe maujuzi jikoni harufu nzuri nyumba nzima hadi baba mjengo aseme leo kaingia mama mwenyewe jikoni rahaa.[emoji3]
Ila wanaume nyie mnadeka sana eti tuwatengee chakula, maji ya kuoga wakati mlivokua single mlikua mnasugua hadi sufuria na michanga na kubeba madumu ya maji, ila ghafla umeoa basi umegeuka mtotoo huwezi hata kusogeza maji ya kuoga bafuni[emoji2957]. Ila fresh tu tunawapenda hivo hivo watoto wetu.
Mimi nisaidiwe tu tena nitafurahi sana huwa nafanya kitu nikijiskia if I don't feel doing it naacha, Yani nafanya jambo kwa kuamua na sio kuwaza Ili nisisaidiwe what I know you can't please people hata ufanyeje binadamu haturiziki, so nafanya kujifuraisha I would rather allow my partner kufanya anachojiskia kuliko Kuni force kufanya nisichotaka kabisa.
[emoji23][emoji23][emoji16][emoji16]the job is present[emoji23]
Ok kama mmekubali kusaidiwa sasa muache kupiga kelele za wivuHafu hayo mambo I grow to see my parents hata watu wengine wanaume kujifanyia vitu vingi wenyewe tofauti na wanaume wa humu wanaopenda umwinyi, kwao upendo ni kumutumikisha mke ka punda wa dobi badala ya kumsaidia, ulezi wa watoto tu huwa ni kazi ngumu bado kuachiwa mambo mengine.
Dah wanaume kuweni na huruma na sisi huwa tunachoka tunahitaji kusaidiwa
Sasa why mna force watu wafanane, oeni wake watakao kuwa wanawabeba Hadi migongoni mwao ka watoto[emoji23][emoji23]Wapo wenye shule wanaji sacrifice kuhudumia waume na watoto zao as they get everything they want! Pesa ipo yani
Na we binadamu ambao naturally ni wakorofi, hao unawazungumziaje?Michepuko ishawaroga huko hata akili haifanyi kazi tena.
Hakuna mwanamke asomheshimu mwanaume wake, ukiona hauheshimiwi ujue wewe ni jipu haustahili heshima.
Kwahiyo ukishalala naye hatakiwi kukutuma?kwani baba yake analala nae? yani ufananishe status ya baba na mume mbona jua na mwezi
Ndio kaoe hao Sasa muache kusakama wanawake wanaotafta hela na maendeleo Yao.Hata mjini wapo na hata wewe hapo mtaani kwako unawaona yaani na wewe ungekuwa umeolewa wangekuwa wanakushangaa na kukusuta.
apart from that sisi ndio tuko🤣Sasa why mna force watu wafanane, oeni wake watakao kuwa wanawabeba Hadi migongoni mwao ka watoto[emoji23][emoji23]
ALIYEKUAMBIA HELA YA MWANAMKE NI YA FAMILIA NI NANI?,MIMI NINA LAKI 3,MKE WANGU ANA LAKI 5,NIKIULIZWA MNA SH NGAPI HAPO NYUMBANI JIBU SAHIHI NI SH 300,000 NA SIO 800,000Yaani unampiga mkeo kisa hajapika au hajafua! Hivi sijui kwanini mnafananisha mwanamke anayetafuta pesa na anayeshinda nyumbani, mkae mkijua hawa ni wanawake wa aina mbili tofauti yaani hawatakaa wawe sawa, kama ambavyo mwanaume tajiri na mwanaume masikini hawako sawa kwenye hii dunia!
Mwanamke anayekusaidia wewe kutafuta pesa usitegemee ataweza kutimiza majukumu yake kikamilifu kama anavyofanya mama wa nyumbani, ninyi wenyewe si ndiyo mmetaka haya mambo ya kusaidiana maisha, kwa kukimbia majukumu yenu! Basi kama vipi oeni wanawake wasiosoma muwahudumie tu!