Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wadau,

Nimekuja kugundua nilikosea kuoa baada ya kukaa kwenye ndoa miaka 15 na kupata watoto wanne. Dah nilijichanganya nikaoa a Corporate lady ambaye alikuwa mwanasheria kule Arusha, alikuwa ana vihela flani na connections za watu wazito ndani ya bongo....duh acha kabisa!!!

Nilikuja kujuta sana manake kazi zoote na mambo yooote ya nyumbani yalikuwa yanafanywa na mabeki tatu kuanzia Kufua nguo zangu, maji ya kuoga, kupika nk alikuwa hana time kabisa na nyumba yake. Hajui chochote kinachoendelea nyumbani kwake kila kitu anabishana na kushindana.

Mtu wa vikao vya dinner karibu kila siku. Miaka ya mwanzoni nilikuwa namdunda sana sana baadaye nikapataga kesi, wakati mwingine ilibidi niingie hasara ya kumpeleka hospitali na kumhudumia manake alikuwa na watoto wadogo.

Nikaamua kuingia kwenye pombe na michepuko ili nimpuuzie. Nikawa nampuuzia kama vile hayupo na yeye akanikazia, akazidisha kiburi na jeuri nikaanza tena kumdunda nikapata tena kesi kubwa manake ilikuwa nimuulie mbali.

Sasa baadaye nikafikiria sana watoto wangu tukafikia hatua ya kuachana na kukubaliana jinsi ya kuwalea watoto. Sasa tumeweka nguvu zoote katika kuwalea watoto na hali imekuwa shwari kabisa kila mtu anaishi kivyake baada ya talaka.

Najua kuna wale watakaosema tuishi nao kwa akili. Nilijitahidi kufanya hivyo kwa miaka 15 lakini ikashindikana manake ningeishia jela baada ya kumtoa uhai na watoto wangeteseka.

Bora iwe hivi hivi wote tupo wazima wa afya.

ALAMSIKI, DUH USIOMBE KUKOSEA KUOA BORA UKOSEE KUZALIWA

KARIBU NI WADAU WENZANGU MLIOKOSEA KUOA.

KWA NAMNA ULIVYO ELEZA, TAYARI NIMEJUA HUYU MWANAMKE NI WA KABILA GANI.
YEYOTE ALIYE OA HAWA WATU NDOA ZAO NGUMU, NI VILE WANAUME HATUNA UTAMADUNI WA KUSEMASEMA YA NDANI.
NI KWELI WAZURI WA SURA, UMBILE, AKILI ZA BIASHARA, WAMESOMA WAKO KWENYE TAASISI NYINGI ZA FEDHA,NK


SIFA HIZI ZINAWAPA UPOFU, ZINAFUNGA FAHAMU ZAO HAWAJUI HIZI HOME ACTIVITIES NI KICHOCHEO KIZURI CHA MAPENZI NA UPENDO.UNAOA MKE HALAFU UNAJIULIZA HIVI HUYU KUSIMAMA JIKONI NA KUPIKA HATA CHAI ILIKUWA MWAKA GANI?

NYUMBANI NI WACHAFU, WAVIVU, HAWAJUI KUPIKA, MALEZI YA WATOTO SIO KAZI YAO, KWENDA KUSALI WANAKWENDA KWA AJILI YA KUONEKANA TU, MAPENZI KITANDANI NI MZIGO, WANAPENDA MNO KUISHI KWA KUFUATA MACHO YA WATU, WANAPENDA KUFANYA YA KUWAPENDEZESHA WATU,KIBAYA ZAIDI WANA LUGHA NGUMU SANA SANA. NJE KWA WATU BAKI LUGHA NI NZURI NA LAINI SHIDA IKO KWA WATU WA NYUMBANI KWAO! NA HAWA NDIO WATESI WAZURI WA WAFANYAKAZI WA NDANI.

ZAMA ZETU HIZI KUOA NI RISK!NI HATARI KWA AFYA YA AKILI, MWILI NA ROHO.

KUNA WATU NIKISIKIA WANAOA WATU WA KABILA HIZI, NASIKITIKA SANA KWA SBB SIWEZI KUKUSHAURI UBADILISHE MTAZAMO WAKO KWA SBB TAYARI UKO KWENYE ULEVI WA MAPENZI. NA KUKULEVYA WANAJUA SANA... SASA OA INGIENI NDANI. RANGI ZOTE UTAZIJUA.
 
You pay her to ASSIST, kumbe ni msaidizi si ndio, duties za msaidizi sio unambebesha zigo lote la nyumba yako. Atafua, atapika, atadeki, atafanya kazi Ila kumbuka the "home" is yours, majukumu ni yako sio yake.

Fanya kazi acha uvivu, halafu ujue mwanamke mvivu kufanya kazi za ndani ni naturally mchafu inside out, naturally hata sex hawezi/hapendi, mtu akiwa active na kazi za ndani automatically anakuwa msafi na hata 5x6 anaimudu vizuri.
True 💯
 
Yeye ndo alikosea kuolewa na wewe.

Corporate women are not for the weak men.

Only Alphas can and believe me, a man can change a woman only if he is man enough.
Msimbe na singo maza mwingine huyu. Anajifanya expert wa mahusiano wakati mpaka umri huo anaelekea uzeeni hakuna mwanaume ameenda kwao kutoa mahari na aolewe kwa heshima. Anaishia kuzalishwa tu mtaani...🚮🚮🚮
 
Aisee, hapo alidhamiria kabisa. Shingo ni very sensitive, lazima hisia zije, Ila inategemea mapenzi yenu niaje, wengine hata kushikana mikono hawawezi, sembuse kuchum shingo.

Apite shem Makiwendo aone ulivyoharibu mambo kwa kubusiwa shimgoni[emoji125][emoji23]
Kaendelee na ule uzi wako wa Mmaa.[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani nimeufatilia huu mjadala Kwa karibu sana, wanaume mmefunguka, mmelalamika, Ila Naomba niulize, unalalamika mkeo hakupikii, hapangi nyumba, ni lini ulimsifia mkeo Kwa hizo shughuli? Jamani udhaifu WA mwanamke ni masikio yake, maneno matamu yanaweza kumfanya mke awe mtumwa wako na awakane hata ndugu zake.
Mimi huyu mbaba Kwa kweli nashukuru, anajua kuappreciate....nikimpikia ananisifia, si ofisini kwake, si Kwa ndugu zake wote wanajua mkewe anajua kupika[emoji23]...
Pia ananihamasisha, kidogo mara kanisuprise oven, mara mashine ya kusagia Nyama, mara food processor....Kwa nini nisimpikie hata Kama narudi kazini saa Saba ya usiku?
Sasa wewe huna muda WA kununua viamba upishi, unasubiri acheze vikoba anunue kisha unataka upikiwe....[emoji23][emoji23]

Wanaume mjiangalie mnajikwaa wapi, wengi mna visirani viso msingi.
Teh akusifie? Watakuambia akusifie nini wakati hilo ni jukumu lako ila wao wanataka tuwe na shukurani hata wakitimiza majukumu yao!
 
Siwezi kutoka kazini nimechoka huko eti nianze kuosha vyombo, kupika Hadi saa nne kisa mume never on earth instead ya kutafta mtu afanye nihangaike tu Hadi nizeeke kwa kweli hapana, wote tumetoka tumeenda kazini nirudi nihangaike na yote hayo?
Maisha ni mafupi kujichosha na kazi mara kupika pika jamani Ili kufuraisha binadamu asiye na shukrani
Msimbe mwandamizi.... Singo maza 🚮🚮🚮
 
Aisee, hapo alidhamiria kabisa. Shingo ni very sensitive, lazima hisia zije, Ila inategemea mapenzi yenu niaje, wengine hata kushikana mikono hawawezi, sembuse kuchum shingo.

Apite shem Makiwendo aone ulivyoharibu mambo kwa kubusiwa shimgoni[emoji125][emoji23]
Mimi siuzi mbinu za kivita aisee[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee. Pole sana, Hali ya kuota mapembe huwa inatokea kwa wanawake wachepukaji na kupelekea kuanza dharau kwa waume zao na kupelekea kuangusha ndoa zao.

Msingefikia hatua ya Talaka nina hakika mke wako angekuja kujirudi na kubadilika na kuwa mke baada ya kufikia umri fulani. Maana wanawake na watoto ndio wanaathirika sana mnapotengana
KUNA WAKATI NI HERI WAZAZI WAKATENGANA/TALIKIANA KWA FAIDA YA WATOTO.
 
Umeanza vizuri ila umemalizia hovyo hovyo, unaposema kukosea kuoa bora ukosee kuzaliwa unajua uzito wa hicho ulichokisema?

Usikufuru thamani yako ya kuzaliwa na vitu vya hovyo, unatakiwa kumshukuru Mungu kwa kukupa fursa ya kuzaliwa ukiwa hujakosewa.
 
Unaweza kuwa na harusi nzuri ila usiwe na ndoa nzuri, na unaweza kuwa na ndoa nzuri ingawa hukuwa na harusi nzuri.Harusi ni sherehe lakini ndoa ni maisha. Tuwe makini ambao bado hatujaoa!
 
Back
Top Bottom