Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wadau,

Nimekuja kugundua nilikosea kuoa baada ya kukaa kwenye ndoa miaka 15 na kupata watoto wanne. Dah nilijichanganya nikaoa a Corporate lady ambaye alikuwa mwanasheria kule Arusha, alikuwa ana vihela flani na connections za watu wazito ndani ya bongo....duh acha kabisa!!!

Nilikuja kujuta sana manake kazi zoote na mambo yooote ya nyumbani yalikuwa yanafanywa na mabeki tatu kuanzia Kufua nguo zangu, maji ya kuoga, kupika nk alikuwa hana time kabisa na nyumba yake. Hajui chochote kinachoendelea nyumbani kwake kila kitu anabishana na kushindana.

Mtu wa vikao vya dinner karibu kila siku. Miaka ya mwanzoni nilikuwa namdunda sana sana baadaye nikapataga kesi, wakati mwingine ilibidi niingie hasara ya kumpeleka hospitali na kumhudumia manake alikuwa na watoto wadogo.

Nikaamua kuingia kwenye pombe na michepuko ili nimpuuzie. Nikawa nampuuzia kama vile hayupo na yeye akanikazia, akazidisha kiburi na jeuri nikaanza tena kumdunda nikapata tena kesi kubwa manake ilikuwa nimuulie mbali.

Sasa baadaye nikafikiria sana watoto wangu tukafikia hatua ya kuachana na kukubaliana jinsi ya kuwalea watoto. Sasa tumeweka nguvu zoote katika kuwalea watoto na hali imekuwa shwari kabisa kila mtu anaishi kivyake baada ya talaka.

Najua kuna wale watakaosema tuishi nao kwa akili. Nilijitahidi kufanya hivyo kwa miaka 15 lakini ikashindikana manake ningeishia jela baada ya kumtoa uhai na watoto wangeteseka.

Bora iwe hivi hivi wote tupo wazima wa afya.

ALAMSIKI, DUH USIOMBE KUKOSEA KUOA BORA UKOSEE KUZALIWA

KARIBU NI WADAU WENZANGU MLIOKOSEA KUOA.
Umejitahidi sana miaka 15 🙌🙌🙌🙌🙌🙌wenzio masaa tu washavunja ndoa....
 
Mkuu, hizi changamoto zako zinavumilika na zinafundishika ukitumia akili ndogo tu.
Unaweza hata ukamtafutia sehemu akajifunze mapishi toka kwa wale waliosomea Hotel management kisha mdanganye unataka kumfungulia Mgahawa akimaliza mafunzo. Kisha akimaliza kufundishwa unamuacha nyumbani.

Kesi za uchepukaji ndio ngumu sana kwa mwanaume kuhimili.
Ukishaanza kumdanganya wife mtakosana
 
Yaani unampiga mkeo kisa hajapika au hajafua! Hivi sijui kwanini mnafananisha mwanamke anayetafuta pesa na anayeshinda nyumbani, mkae mkijua hawa ni wanawake wa aina mbili tofauti yaani hawatakaa wawe sawa, kama ambavyo mwanaume tajiri na mwanaume masikini hawako sawa kwenye hii dunia!

Mwanamke anayekusaidia wewe kutafuta pesa usitegemee ataweza kutimiza majukumu yake kikamilifu kama anavyofanya mama wa nyumbani, ninyi wenyewe si ndiyo mmetaka haya mambo ya kusaidiana maisha, kwa kukimbia majukumu yenu! Basi kama vipi oeni wanawake wasiosoma muwahudumie tu!
Tatizo kutafta mke ambaye hajasoma ni mazoezi kwa sasa😅!!! Utampatia wapi labda uende usambaani huko Bumbuli ukalokote goigoi.

Wanawake ni nyie nyie mliosoma tutawaoa ila unajipimia tu size ya kero😂 ambazo unaweza vumilia! If you wanna mistreat your man sababu unaenda kazini then wapo ambao watavumilia mis treatments hizo 😅😅😅! Huwezi kosa boya wako wa kumpelekesha na kumpangia ratiba za papuchi sababu unaenda ofisini!

What i mean its irrelevant yani kuunganisha kazi na majukumu yako kama mke kwenye familia. Its never an excuse kabisa😎
 
Hahahahahah ni irrelevant ila ndio vinanogesha ndoa! Hayo unayoita irrelevant ndio yanfanywa na nyumba ndogo ili kutukamata vizuri sababu hamna mwanaume ambaye hapendi kuwa caressed! Tatizo watoto wa dotcom mnahisi kuishi na waume ni kuwafanyia favours yani sababu mnapenda kuitwa mke ila majukumu yanayoambatana na kuwa mke wa fulani hamyataki!

Mke anayekuhudumia kwa hali na mali ndiye anayetengeneza nafasi ya kuwa mtu special zaidi kwenye maisha yako na hata muda wote unamiss na anakuwa akilini mwako. Yani mke akisafiri lazma u feel tofauti sio mke akiwepo na asipokuwepo hamna difference. Inaboa sana!

Wanaume understanding tupo tutaignore baadhi ya vitu ila kuna watu kwao inakuwa ni kama dharau flani! Hakusemeshi ila atatafta anakokuwa treated right.
Kukuhudumia haimaanishi anakua mtumwa kwenye nyumba yake. Ndoa ni kushirikiana na kusaidiana na sio sehemu ya mfalme na kijakazi wake. Kama mke anachoka anastahili kupata muda wa kupumzika, kutoka na marafiki zake maana maisha sio ndoa tu.

Yani kuna nyumba mama akiamka saa 11 asubuhi hadi saa mbili usiku hajapumzika anahudumia familia. There's no trophy in doing all of that na siku mwili umedhoofu huyo huyo unamuhudumia ndio wa kwanza kukusimanga umezeeka humvutii tena
 
Huyo mke anayeamka saa 11 na kumaliza kazi saa 2 usiku atakuwa na ram 500MB!

Wanawake are known for multitasking yani anaweza fanya mambo yake chap chap saa 3 kashamaliza kila kitu nyumba safi na kila kitu kiko on order. Anapumzika zake hadi saa 5 anajipikilisha saa 7 watu washakula!

Anakuja kujigusa saa 11 tena kuandaa cha usiku! Saa 1 kila kitu on point. Wanawake wavivu ndio hamkosi sababu na mara nyingi mke akiwa na mtoto mdogo huwa tunawawekea mabeki 3
 
Wadau,

Nimekuja kugundua nilikosea kuoa baada ya kukaa kwenye ndoa miaka 15 na kupata watoto wanne. Dah nilijichanganya nikaoa a Corporate lady ambaye alikuwa mwanasheria kule Arusha, alikuwa ana vihela flani na connections za watu wazito ndani ya bongo....duh acha kabisa!!!

Nilikuja kujuta sana manake kazi zoote na mambo yooote ya nyumbani yalikuwa yanafanywa na mabeki tatu kuanzia Kufua nguo zangu, maji ya kuoga, kupika nk alikuwa hana time kabisa na nyumba yake. Hajui chochote kinachoendelea nyumbani kwake kila kitu anabishana na kushindana.

Mtu wa vikao vya dinner karibu kila siku. Miaka ya mwanzoni nilikuwa namdunda sana sana baadaye nikapataga kesi, wakati mwingine ilibidi niingie hasara ya kumpeleka hospitali na kumhudumia manake alikuwa na watoto wadogo.

Nikaamua kuingia kwenye pombe na michepuko ili nimpuuzie. Nikawa nampuuzia kama vile hayupo na yeye akanikazia, akazidisha kiburi na jeuri nikaanza tena kumdunda nikapata tena kesi kubwa manake ilikuwa nimuulie mbali.

Sasa baadaye nikafikiria sana watoto wangu tukafikia hatua ya kuachana na kukubaliana jinsi ya kuwalea watoto. Sasa tumeweka nguvu zoote katika kuwalea watoto na hali imekuwa shwari kabisa kila mtu anaishi kivyake baada ya talaka.

Najua kuna wale watakaosema tuishi nao kwa akili. Nilijitahidi kufanya hivyo kwa miaka 15 lakini ikashindikana manake ningeishia jela baada ya kumtoa uhai na watoto wangeteseka.

Bora iwe hivi hivi wote tupo wazima wa afya.

ALAMSIKI, DUH USIOMBE KUKOSEA KUOA BORA UKOSEE KUZALIWA

KARIBU NI WADAU WENZANGU MLIOKOSEA KUOA.
Unaweza kuoa Samaki mwanzoni lakini akageuka nyoka huko mbeleni,hivyo hupaswi kujilaumu kwa sababu wewe ulioa samaki hukuoa nyoka.
 
Hapo kwenye bond na chemistry nmepaelewa aisee...unaweza kuwa na demu mkali had washkaj wanakuonea wivu ila ukawa huna bond nae na chemistry hakuna..ila ukawa na demu wa kawaida tu ila mka connect vibaya mno...yameshanitokea haya mambo
Yes na hyo chemistry na bond ndio watu wengi wanaikosa kwenye mahusiano, Kuna wale watu hutokea mna connect sana, ila ndio huwa watu ka hivo hamdumu
 
Duuh..pole sana.
Ila hapo kwenye samaki na kuku kuna mbadala.
Sidhani kama kuna ulazima wa yeye kukwarua samaki na kukata vinyeo, unless otherwise mnawavua wenyewe..
Wanaowauzia wanaweza fanya hayo mkipenda
Wale wanaouza huwa hawamalizi magamba na manyoya. Lazima uwasafishe wewe mwenyewe vizuri kumalizia takataka zilizobaki then marinate ufanye upendavyo . Hivi mwanamke na akili zake anampika samaki na magamba au kuku na manyoya kweli anaweza hata kufua pichu au kunyoa zivu??
 
Mkuu, hizi changamoto zako zinavumilika na zinafundishika ukitumia akili ndogo tu.
Unaweza hata ukamtafutia sehemu akajifunze mapishi toka kwa wale waliosomea Hotel management kisha mdanganye unataka kumfungulia Mgahawa akimaliza mafunzo. Kisha akimaliza kufundishwa unamuacha nyumbani.

Kesi za uchepukaji ndio ngumu sana kwa mwanaume kuhimili.
Atapoteza ada tu 😅
 
Wale wanaouza huwa hawamalizi magamba na manyoya. Lazima uwasafishe wewe mwenyewe vizuri kumalizia takataka zilizobaki then marinate ufanye upendavyo . Hivi mwanamke na akili zake anampika samaki na magamba au kuku na manyoya kweli anaweza hata kufua pichu au kunyoa zivu??
Humo kuna kilaza Pro Max watoto wa date za KFC na Pizza Hut hao! Anajikojolea mpaka form 6 😅
 
Wale wanaouza huwa hawamalizi magamba na manyoya. Lazima uwasafishe wewe mwenyewe vizuri kumalizia takataka zilizobaki then marinate ufanye upendavyo . Hivi mwanamke na akili zake anampika samaki na magamba au kuku na manyoya kweli anaweza hata kufua pichu au kunyoa zivu??
Usiombe uchokwe mamawe hakuna rangi utaacha ona yaani mtu uishi nae miaka12 na ushee akulishe samaki na magamba[emoji848]we unaona ni sawa hii??unless kuna sehemu amevurunda ma ke akaona isiwe tabu utakula hivyohivyo bora liende
 
Sijaoa ila naishi na pepo juzi nmesafiri tu kauza Friji narudi nauliza naambiwa nmeongezea naagiza cm hiv ndugu zangu ni sawa ..nahitaji kuanzisha Uzi ili mnipe ushauri wakuu...sijui niendapo.
[emoji23][emoji23][emoji23]Hilo kweli pepo....auze fridge anunue simu??? Huo ni mwanzo, siku atauza gari akanunue redio
 
Ndivyo dunia ilivyo mama. Huwa nafikiri ni mgonjwa wa akili japo haonyeshi dalili nyingine za aina hiyo huko nje. Ni mimi ninayekaa naye tu ndiye ninaye mjua.
Sio mgonjwa nakuambia...wapo watu wa hivyo kuna mmoja namfahamu ni msomi kabisa ila mambo yake ndio kama hayo uliyosema sijui wanakuwa na haraka ya wapi
 
Back
Top Bottom