Nimesoma malalamiko ni mengi humu! Nimeoa hao wasomi level ya masters nani mtumishi wa shirika fulani la serikali nani boss kwenye ilo shirika namaanisha ni wale wakuendeshwa na v8 ma safari kibao lakini niwe mkweli, msichana kiumri ni mdogo ana 32 mimi 36 na mimi sina elimu kama yake ni kijana wa form 6 na nina biashara zangu hapa mjini lakini naweza kusema huyu mke ana nizamu sijawai kuona... Tuna dada wa kazi na mtoto mmoja lakini anaamka sa 11 anandaa chai na cha mchana ndo anaondoka kwenda kazini na jioni lazima aulize mume unataka kula nini....
Tukiachana na hayo sijawai kuona hatimizi wajibu au kinivunjia heshima na ndoani huu ni mwaka wa7!!! Nafikiri kabla yakuoa chunguza uyo mwanamke na anapotokea yani familia yake... Kuna kitu tunasahau nacho ni ushamba! Usiombe kukutana na mwanamke hajui alafu ajifanye anajua au mwanamme wa style hiyo na Hawa ndo wanaitwa wajuaji kwenye ndoa lazima pawe pamoto....!!! Maisha ya ndoa haya husiani na elimu zenu au kipato ila mmoja akiwa vizuri anamuinua mwengine na maisha yanaenda safi!!! Men achana na kuwaza visenti vya hawa wakina mama maana unakuta kamshahara ni ka million 1.3 ila iyo jeuri ni balaa...
Tafuta Pesa yako kama mwanaume tunza familia kama baba kuanzia mke mpe pesa za shopping yake na watoto nyumbani vyakula viwepo vyakutosha sio maharage tu jaza nyama, samaki, kuku weka vile vyakula wanavyopenda nyumbani kwako na ukipata time weekend ingia jikoni mwambie mke leo nyie pumzikeni jumapili napika mimi baba andaa chakula kula mle vyombo dada atamalizana navyo....
Jioni aga mke naenda kuangalia mpira mama nitachelewa kidogo ndo time yakujiongeza sasa hope nimeeleweka hapo!!!!... Hutokaa usikie kelele tatizo hawa tunataka kuwafanya kama beki 3 na ilo ndo tatizo ila mimi pamoja na yeye ana kibunda ila anajua akifika kwangu mimi ni mume na anakuwa na adabu zote