Jamani nimeufatilia huu mjadala Kwa karibu sana, wanaume mmefunguka, mmelalamika, Ila Naomba niulize, unalalamika mkeo hakupikii, hapangi nyumba, ni lini ulimsifia mkeo Kwa hizo shughuli? Jamani udhaifu WA mwanamke ni masikio yake, maneno matamu yanaweza kumfanya mke awe mtumwa wako na awakane hata ndugu zake.
Mimi huyu mbaba Kwa kweli nashukuru, anajua kuappreciate....nikimpikia ananisifia, si ofisini kwake, si Kwa ndugu zake wote wanajua mkewe anajua kupika😂...
Pia ananihamasisha, kidogo mara kanisuprise oven, mara mashine ya kusagia Nyama, mara food processor....Kwa nini nisimpikie hata Kama narudi kazini saa Saba ya usiku?
Sasa wewe huna muda WA kununua viamba upishi, unasubiri acheze vikoba anunue kisha unataka upikiwe....😂😂
Wanaume mjiangalie mnajikwaa wapi, wengi mna visirani viso msingi.