Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wewe bado una mpenda mkeo Hadi unafatilia kuwa aliolewa na kuachika huko aliko bado una mpenda rudisheni mpira kwa kipa na muache ujeuri za kijinga na mambo ya ajabu mzeeke pamoja
Simfuatilii kabisa ila kwa sababu tunalea watoto pamoja kila mtu na mji wake na wakija wanakuja na dada yao wa kazi basi baadhi ya taarifa zinafika kote automatically ...nafikiri umenielewa
 
Simfuatilii kabisa ila kwa sababu tunalea watoto pamoja kila mtu na mji wake na wakija wanakuja na dada yao wa kazi basi baadhi ya taarifa zinafika kote automatically ...nafikiri umenielewa
Eeeh kazi kweli kweli
 
Yaani unampiga mkeo kisa hajapika au hajafua! Hivi sijui kwanini mnafananisha mwanamke anayetafuta pesa na anayeshinda nyumbani, mkae mkijua hawa ni wanawake wa aina mbili tofauti yaani hawatakaa wawe sawa, kama ambavyo mwanaume tajiri na mwanaume masikini hawako sawa kwenye hii dunia!

Mwanamke anayekusaidia wewe kutafuta pesa usitegemee ataweza kutimiza majukumu yake kikamilifu kama anavyofanya mama wa nyumbani, ninyi wenyewe si ndiyo mmetaka haya mambo ya kusaidiana maisha, kwa kukimbia majukumu yenu! Basi kama vipi oeni wanawake wasiosoma muwahudumie tu!
Huyu mwanamke alikutwa hana kitu..😷😷😷
 
NGOMEKONGWE2021 - Tupo wengi, kiongozi. Mie pia watoto 4 kama wewe. Miaka 12 ya ndoa. Mama wa nyumbani. Tatizo hawezi kujifunza kitu.

Kila siku ni shida tupu ndani ya nyumba. Mfano, hawezi kutoa magamba ya samaki yakaisha yote kabla ya kumpika samaki. Chakula anavyonunua kwenye supermarket, ndivyo anavyokipika!

Anaweza kupika nyama ya kuku na kinyeo chake ama bado kuna kiasi fulani cha vinyoya!! Hata nikimweleza vipi, akili yake haishiki!! Hataki niwafundishe watoto. Nikiwakosoa watoto kwa namna ya kuwafundisha, anakuja juu.

Watoto wananiona mimi shetani na yeye malaika. Amejenga chuki kati yangu na watoto ambao bado ni wadogo tu. Sijawahi kumpiga ama kuchepuka lakini nilikwisha mwambia kuwa tungekuwa tunaoa mara ya 2, nisingemuoa tena. Sina hamu tena hata ya kulala
Kwahiyo mkuu vinyeo vya kuku wewe hulii??
 
Back
Top Bottom