Sitaki kusema nimekosea, ila nakiri kuna muda sisi wanaume tunataka na sisi tuwe kama wanawake sasa.
Nilipooa baada ya mwaka nikagundua kumbe kule kulazimisha niheshimiwe ndio naharibu zaid.
Sasa nikuambie mimi napika na kufua mpaka kuogesha watoto tena kwa furaha kabisa...Wajua kwanini?? Mwanamke naye ni binadamu, anachoka, ana mambo kichwani saa nyingine yanabaki kuwa ya kwao mioyoni mwao. Sasa najiuliza mfano mke wangu kutwa nzima kazini kwake kapata matatizo au hata kwao labda kuna matatizo, sasa hizo nguvu za kunifanyia kila kitu atazitoa wapi achili yale ya kitandani?
Sasa ukitaka wanawake wasikusumbue fanya yale ambayo hayataacha upungukiwe na nguvu za kiume.
Mimi mke wangu amefika hatua ananishauri hata nioe mke wa pili mbona vitu vya kijinga sisumbuani naye kabisa.
Utaratibu unajulikana wa ndoa, sasa mimi kuanza kumfunda anifulie na kinipikia ni kujitafutia ugomvi tu.
Mimi hata arudi kesho sitamuuliza yeye kama ana akili atasema, mbona kitendo cha yeye mfano kufanya vitu bila mimi kujua maana yake anatafuta ugomvi na mimi, sasa mimi nampuuza na simuulizi na nitampikia ale kabisa, ukisema atanidharau kwani hajui shughuli yangu tukilala? Sasa kama anatafuta ugomvi hanipati.