cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
Umemaliza kila kitu hapa. [emoji23][emoji23][emoji23]Nimemaanisha vipi kama mwanamke hajisikii kula kwa muda huo? Wewe si ukafunue tu mahotpot ukale?
Teh teh wanaume kuchepuka huwa mnachepuka hata wake zenu wawe malaika uzuri hilo huwa mnalisema wenyewe kwamba hakuna mwanaume rijali asiyechepuka hivyo wala hakuna jipya hapo! Na hiyo ndiyo sababu wanawake wanawafanyia yote haya walau mngekuwa hata mnajiheshimu tungewafikiria!
Halafu huwa nawashangaa sana yaani unamsifia mchepuko wako ambaye kwake unaenda mara moja moja hivyo hata kukupikia anakupikia mara moja moja na kukupa anakupa mara moja moja na bado hakusaidii chochote kiuchumi wewe ndiyo unamhonga na kumpeleka shopping! Then unamfananisha na mkeo ambaye anatakiwa akupikie kila siku akupe unyumba kila siku na bado pesa akusaidie kutoa!
Hebu jaribu kumtwika huyo mchepuko hayo majukumu ya mkeo uone kama naye atabaki hapo! Dooh kumbe ndiyo maana wanawake wengi siku hizi hawataki kuolewa wanang'ang'ania waume za watu ili wawe michepuko tu maana wanajua michepuko inakula good time sawa na au pengine hata zaidi ya hao wake wa ndoa!
Siku hizi tofauti kati ya mke na mchepuko ni pete na kubadilishwa jina tu kitu ambacho kwa wanawake wengine hiyo siyo issue tena kwao wanaona ni mzigo tu! Na tofauti nyingine ni kwamba mke ndiyo ana majukumu mengi kwa mwanaume kuliko mchepuko ila huduma wanapata sawa au mchepuko anapata zaidi dooh ndoa hizi!