LOooh!
Huyo mwalimu, hata kama angekuwa mzuri kiasi gani, hawezi kumudu kuangalia kazi za wanafunzi wake kwenye madaftari yao.
Lakini, mkuu 'Return' hebu niambie, enzi hii kweli, karne hii ya ishirini na moja, wewe kama mzazi utampeleka mwanao kwenye mazingira ya namna hii?
Hawa wazazi wa hawa watoto, wengi wao watakuwa ni wazawa wa baada ya uhuru wa nchi yetu, 1961. Hata kama hawakubahatika kupata kisomo cha kutosha, zaidi ya darasa la saba tuseme; hawa wazazi wanaweza wakasimama na kusema walisoma katika mazingira ya aina hii yanayowakabili watoto wao?
Yaani kiukweli, hawa wazazi hawana sauti yoyote wanayoweza kupaza wakasikilizwa, hata kama wao hawana uwezo wa kuwajengea shule hawa vijana?
Hizi kura zao wanazopiga kila mara kuwachagua viongozi wasioona madhara haya, hawaoni kabisa kuwa kura hizo zina thamani kubwa inayoweza kabisa kubadili hali hii ya hawa watoto?
Ngoja nimwite rafiki yangu Erythrocyte. Picha hii haiwezi kukosa kuingia kwenye maktaba yake. Na kama kweli vyama vya upinzani wana nia thabiti ya kuibadili Tanzania, hakuna mahali pa kuanzia zaidi ya tatizo kama hili la elimu yetu.
Siwasikii wakisema chochote, sijui nao wanayo matatizo gani!
Hapa sio swala la kukosa uwezo wa kujenga shule. Huu ni uzembe na upumbavu wa viongozi na wananchi wanaowaongoza.
Mtu awe mkuu wa mkoa/wilaya, tarafa/kijiji. Uwe ofisa elimu ngazi yoyote katika eneo hilo, hali hii isikustue, wewe ni kiongozi wa namna gani!
Inatia hasira sana.